Ukipewa nafasi ya kuwashauri vijana wa kitanzania, ushauri gani ungewapa ushauri kwa manufaa ya jamii inayowazunguka na Taifa pia?

Analog

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2024
Posts
323
Reaction score
618
Hakika vijana ndo taifa la kesho na nguvu kazi kwa taifa na jamii inayomzunguka, tusipowekeza kwa vijana tunaweza kuja kuwa na jamii na taifa la hovyo hapo mbeleni.

Ni upi ushauri wako ungeliwapa endapo ungepewa nafasi ya kuzungumza nao?
 
Nitawashauri wawe na tabia ya kupenda kujisomea vitabu mbalimbali kukuza uwezo wa kufikiri ,kinyume apo vijana waache kujiita ni wasomi kwa vielimu vya kukariri shule.

Pia wajaribu kutafuta fursa hadi njee ya mipaka ya Tanzania kuliko kujifungia tu ndani yaan watoke maghetoni.
 
Ni kweli kabisa Dunia inahitaji watu wanaotafuta maarifa kupitia kujisomea vitabu
 
Wapunguze kulalamikia serikali. Serikali sio baba yako.

Waache kudhani kuna mwanasiasa atakuja kubadilisha maisha yako
Mkuu siasa nazo huwa zina shape standards fulani za kimaisha katika taifa ujue. Mara nyingine vyama tawala Africa hupenda kusema hivyo kama Misleading words tu.
 
Pia wajaribu kutafuta fursa hadi njee ya mipaka ya Tanzania kuliko kujifungia tu ndani yaan watoke maghetoni.
Mipaka gani watoke wakati wananyimwa passport, wanazungushwa mpaka watoe chochote kitu
Yaani kupata passport mpaka uwe na ndugu yako anayefanya kazi uhamiaji.

Wasomi field tu mtu anaombwa rushwa sembuse kazi
Vijana waliochukuliwa kwenda kwenye mradi wa kilimo, wamefika kule wametelekezwa

Tenda nyingi wanapewa watu wa nje vijana watafanya nini?
Basi wameamua kujiajiri bado Tra uchwara mambo wanaleta mengi muda mchache huko BRELA sitaki kuongea sana
 
Wamtegemee MUNGU maana Kama kazi wamefanya Sana na wanafanya Sana Ila matokeo ni 0-0 means we need having the strength of the higher power.
Mungu ndio kila kitu vijana waliokuwa wanafanikiwa miaka ya 2000 mwanzoni walikuwa wakichangua upande yani nguvu ya kiroho katika kufanya mambo yao ya kimaendeleo mana nguvu ya kiroho ni kama engine gari ata ipambwe vipi bila engine haitembea vijana wengi kwa sasa wameamua kuwa neutral hawapo kwa Mungu hawapo kwa shetani wanaamini katika uwezo wa kielimu
 
Mipaka gani watoke wakati wananyimwa visa, wanazungushwa mpaka watoe chochote kitu
Yaani kupata visa mpaka uwe na ndugu yako anayefanya kazi uhamiaji.

Wasomi field tu mtu anaombwa rushwa sembuse kazi

Tenda nyingi wanapewa watu wa nje vijana watafanya nini?
Basi wameamua kujiajiri bado Tra uchwara mambo wanaleta mengi muda mchache huko BRELA sitaki kuongea sana
Huu ujumbe ungeuandika chini ya kila komenti za bwana lukas Mwashambwa ningekuona umeshakua mdogo wangu.
 
Wamtegemee MUNGU maana Kama kazi wamefanya Sana na wanafanya Sana Ila matokeo ni 0-0 means we need having the strength of the higher power.
Unadhani maelfu ya vijana wasio na ajira hawamtegemei huyo Mungu ndio maana hawana ajira?
 
Mungu ndio kila kitu vijana waliokuwa wanafanikiwa miaka ya 2000 mwanzoni walikuwa wakichangua upande yani nguvu ya kiroho katika kufanya mambo yao ya kimaendeleo mana nguvu ya kiroho ni kama engine gari ata ipambwe vipi bila engine haitembea vijana wengi kwa sasa wameamua kuwa neutral hawapo kwa Mungu hawapo kwa shetani wanaamini katika uwezo wa kielimu
Hakuna taifa lililo endelea kwa vijana wake ku base na mambo ya kiroho.

Hebu acheni kutoa mawazo uchwara hapa.

Mifumo mibovu ya nchi ndio ina haribu vijana.
 
Waendelee tu kubet,kumfuatilia Mange kimambi,Diamond,Simba na Yanga,kumsikiliza Zuchu,kula tumbaku,kunywa visungura,kuchat kwenye magroup mpaka mid night,

Maisha bora yatakuja yenyewe tu,kwa kifupi yani watembee na funguo za Magari kiunoni,magari yatakuja yenyewe tu.

Vijana wa leo hawashauriki.
 
Hakika vijana ndo taifa la kesho na nguvu kazi kwa taifa na jamii inayomzunguka, tusipowekeza kwa vijana tunaweza kuja kuwa na jamii na taifa la hovyo hapo mbeleni.

Ni upi ushauri wako ungeliwapa endapo ungepewa nafasi ya kuzungumza nao?
Kuheshimu mamlaka zote, na hasa Mungu
 
Kutembea na mishangazi ndyo mpango mzma tuachane na mitoto ya 2000 ina UTI kali sana
 
Back
Top Bottom