Ukipita soko la Buguruni unakumbushwa tamaduni ya mwafrika ni kuridhika na uchafu

Ukipita soko la Buguruni unakumbushwa tamaduni ya mwafrika ni kuridhika na uchafu

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
878
Reaction score
2,014
Yaani kabisa mtu mzima na heshima yake (anaitwa mama nyumbani na hata boss ofisini) anapita kwenye tope linalonuka chakula kilichoharibika (kinyesi pia labda kipo maana harufu mbaya) kwenda kununua chakula ambacho analisha watoto, ndugu na marafiki

Ukiridhika kupata chakula chako katika mazingira ambayo yanafanana na banda la nguruwe tofauti yako na nguruwe inakua ni nini?

Mdau hapa analalamika kuhusu uchafu masokoni huko Mbeya katika uzi wake : KERO - Mbeya: Kabwe hapafai kuwa Soko Jioni, ni pachafu kupindukia, tunakaribisha Kipindupindu

maxresdefault-3109628960.jpg
IMG-20140515-WA0006-353462213.jpg
 
Attachments

  • Soko-3160012958.jpg
    Soko-3160012958.jpg
    97.8 KB · Views: 5
Yaani kabisa mtu mzima na heshima yake (anaitwa mama nyumbani na hata boss ofisini) anapita kwenye tope linalonuka chakula kilichoharibika (kinyesi pia labda kipo maana harufu mbaya) kwenda kununua chakula ambacho analisha watoto, ndugu na marafiki

Ukiridhika kupata chakula chako katika mazingira ambayo yanafanana na banda la nguruwe tofauti yako na nguruwe inakua ni nini?
So waafrika Wote ni wachafu lakini na sio raia wa mataifa pengine ni wasafi Wote!
Ishi na wachina ndio unajua kama mwafrika ni mchafu au ni msafi
 
Ustarabu kwetu bado ni changamotoo.ndo maana unaona ata mambo yakuchaguana nani wakutuongoza hatuwezi.shule tunazosoma zinabaki kwenye makaratasi sio kutusaidia kukabiliana na mazingira ndo maana magonjwa kama kiipindupindu bado yanatusumbua.
 
Hao wazungu mnaowapa sifa kila siku humu kunaanikwa habari zao kwamba ni wachafu kupindukia. Hivi yupi msafi kati ya asiyetumia maji chooni akajipangusa kwa tishu tu na huyu ambaye anajisafisha kwa maji safi chooni?

acha kujidharau mwafrika!
 
Harufu na uchafu ndio imekuwa utambulisho wa masoko yetu mengi, ukisikia harufu tu ujue umekaribia sokoni na ukifika unapokelewa na uchafu baada ya hapo sasa unaanza kutafuta kilicho kuleta hapo sokoni.
Na hili ni tatizo la uwajibikaji wa halmashauri na manispaa zetu kwakuwa wafanyabiashara daily wanalipa ushuru
 
Back
Top Bottom