Ukipita Ubungo Flyover lazima umkumbuke Hayati Magufuli

Ukipita Ubungo Flyover lazima umkumbuke Hayati Magufuli

Bado pale Fire foleni ni kali asubuhi, mvua ikinyesha tope linajaa barabarani sehemu ya jangwani unajiuliza uko jijini au kijijini , Tanroads wapo au hawapo na barabara inafungwa na kuleta usumbufu usioelezeka.

Hii nchi ya ajabu sana kama vile haina viongozi.

Magu angejenga flyover pia pale Fire 🔥 kama leo hii angekuwa hai, waliopo hawana habari.

Ubungo flyover ni kipimo cha akili kubwa ya Magu wengine wamejaa kelele tu
Na hilo tope la Jangwani unadhani limesababishwa na nini? Kabla ya kituo cha mwendokasi pale hapakuwa na utata wa tope, maji na mchanga.

Magufuli akiwa Waziri wa ujenzi ndiye aliyesimamia ujenzi wa mwendokasi ya pale Jangwani
 
Jina la John Pombe Magufuli limejikita katika historia ya Tanzania kama kiongozi mwenye maono na utendaji wa kasi. Moja ya alama kubwa za uongozi wake ni Ubungo Flyover, daraja ambalo limebadilisha mandhari na mtiririko wa usafiri katika jiji la Dar es Salaam.

Kabla ya ujenzi wa daraja hili, eneo la Ubungo lilikuwa maarufu kwa msongamano wa magari. Safari za kwenda na kutoka katikati ya jiji zilichukua muda mrefu, na hali hii iliathiri sana shughuli za kiuchumi na kijamii. Watu walikuwa wakipoteza muda mwingi barabarani, hali ambayo ilisababisha hasara kubwa ya kiuchumi.

Magufuli, akiwa rais wa Tanzania, aliona umuhimu wa kuboresha miundombinu kama sehemu ya mkakati wake wa kukuza uchumi. Ndipo alipoanzisha mradi wa ujenzi wa Ubungo Flyover. Ujenzi wa daraja hili haukuwa rahisi. Kulikuwa na changamoto nyingi, ikiwemo uhamishaji wa makazi na biashara zilizokuwa kandokando ya barabara. Lakini kwa maono yake thabiti na ufuatiliaji wa karibu, daraja lilijengwa kwa wakati na kwa viwango vya hali ya juu.

Sasa, unapopita Ubungo Flyover, unakutana na mtiririko mzuri wa magari, mabasi na malori. Muda wa safari umepungua kwa kiasi kikubwa, na watu wanaweza kusafiri kwa urahisi zaidi. Hali hii imechangia kupunguza msongo wa akili kwa watumiaji wa barabara na kuongeza ufanisi katika biashara na shughuli za kila siku.

Kila mara unapopita Ubungo Flyover, ni vigumu kutopata mawazo ya John Pombe Magufuli. Uthubutu wake, maono yake, na kazi yake ya bidii vimeacha alama isiyofutika katika historia ya Tanzania. Daraja hili sio tu njia ya kupita magari, bali pia ni kumbukumbu ya kiongozi ambaye alifanya kazi kwa bidii kuboresha maisha ya Watanzania. Ni ushuhuda wa jinsi kiongozi mmoja anaweza kubadilisha nchi kwa maono na utendaji wa dhati.
Ni kweli, ni kama tunavyoona majengo ya kale ya wakoloni waliyofanya biashahara za watumwa kwa kuwauza mababu zetu kama mifugo. Tukiona tu hayo majengo hatukosi kuwa na kumbukumbu za mateso ya hao wakoloni.
 
Wajinga ndio mliwao.
Ujinga ni kutoelewa. Ubungo Flyover ilifadhiliwa na World Bank wakati wa Kikwete, na design ya ujenzi wake wakati wa Kikwete.
Magufuli alikuta kila kitu kimetayarishwa.
Nani aliyebadili original design?
 
Wajinga ndio mliwao.
Ujinga ni kutoelewa. Ubungo Flyover ilifadhiliwa na World Bank wakati wa Kikwete, na design ya ujenzi wake wakati wa Kikwete.
Magufuli alikuta kila kitu kimetayarishwa.
Utekelezaji nan alifanya
 
Lazima kumkumbuka. Licha ya flyover, barabara ile mpaka leo haijakamilika. Hasa kipande cha airport, wakati ni kifupi tu na wageni wote wanaongia Dar es salaam na kutoka wanakipitia. Viongozi wote wanapitia hapo hapo kila siku. Angekuwepo Magu kingekuwa kimeshaisha.
 
Ni kweli, ni kama tunavyoona majengo ya kale ya wakoloni waliyofanya biashahara za watumwa kwa kuwauza mababu zetu kama mifugo. Tukiona tu hayo majengo hatukosi kuwa na kumbukumbu za mateso ya hao wakoloni.
Leo tunakamata wachawi hapa alafu tunawatag bwana Tindo
 
Na hilo tope la Jangwani unadhani limesababishwa na nini? Kabla ya kituo cha mwendokasi pale hapakuwa na utata wa tope, maji na mchanga.

Magufuli akiwa Waziri wa ujenzi ndiye aliyesimamia ujenzi wa mwendokasi ya pale Jangwani
Yaani Leo tutawajua Huihui2
 
Hata NISIPOPITA darajani namkumbuka Magufuli tu.
Kwani Iddi Amini na Mobutu hawakumbukwi? Au Adolph Hitler na Benito Mussolini hawakumbukwi?

Suala unakumbukwa kwa kitu gani. Mimi nitamkumbuka Magufuli kwa kujenga Airport kijijini kwake na sasa imebaki useless kama Gbadolite ya Mobutu. Nitamkumbuka pia kwa kutuma kikosi cha Makonda kwenda kumshambulia Tundu Lissu.

Na nyie wajinga mna yenu ya kumkumbuka shujaa wenu
Bwana Huihui2 tena
 
Mkuu wewe ni mtu makini sana so nimeshangaa kidogo unaposema JPM ALIANZISHA..... mie nachojua DMDP enzi za JK ndio ilishachora ramani kwenye kipengele cha "decongestion dar es salaam". Humo ndani kulikua na barabara za mwendokasi, flyovers, stendi mpya n.k so labda ungesema JPM aliendeleza ramani za DMDP ambazo tayari zilishaanzwa telekezwa na JK kwa kujengwa mwendokasi na mabasi kuletwa.
Niliteleza kidogo kiukweli wote wamefanya kazi kubwa sana.
 
Unatutisha na kumbukumbu ukidhani tutaona dhalimu magu alikuwa wa maana sana? Alitekeleza hayo kwa nafasi yake ya kimadaraka sio hisani.
Bwana Tindo pole sana ni bora usiwe unapita kwenye ile Flyover pitia njia ya maji chumvi na njia ya mabibo.
 
Rejea hii mada ya JF ujue Ujenzi ulianza lini 2014. Magu alitafuniwa akaachwa ameze

 
Rejea hii mada ya JF ujue Ujenzi ulianza lini 2014. Magu alitafuniwa akaachwa ameze

Umeliweka vizuri kuhusu flyover. Wengi hawajui hivyo
 
Umeliweka vizuri kuhusu flyover. Wengi hawajui hivyo
Ukiondoa bwawa la Nyerere na daraja la Busisi miradi mingine mingi ilishaandaliwa na kusainiwa mikataba kuanzia reli,barabara,madaraja flyover za ubungo,Tazara n.k
 
Back
Top Bottom