stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,216
- 26,225
Niliwahi kuwaona hawa jamaa wanajitangaza kwenye TV nikaona kama vile hapa kuna njia nyepesi ya kupiga pesa ndefu,ila baadaye nikajitafakari nikasemaa hihihiiii mwagosha...Kuna ndugu yangu wa karibu alinunua hisa za kampuni inaitwa JATU wakijinasibu kuwalimia watu na kuwauzia mazao yao wao wasubiri faida tu.
Kilichotokea hisa wamenunua mazao wameuza kampuni imesema haina uwezo wa kulipa kila mkulima hela kulingana na mazao walioyouza.
Wakati huo huo wanasema wanahama Dar es Salaam wanaenda Rukwa.
Wakati wana hisa 70% wakazi wa Dar es Salaam.
Kwa kifupi wana hisa wa hiyo kampuni wanakaribia Kupigwa.