Ukishaona rais Tanzania anaapishwa halafu baada ya hapo hana mpango wowote na katiba mpya huyo si mzalendo

Ukishaona rais Tanzania anaapishwa halafu baada ya hapo hana mpango wowote na katiba mpya huyo si mzalendo

Kkimondoa

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2014
Posts
4,453
Reaction score
4,933
Sisi wote ni mashahidi nchi hii ipo hapa ilipo kwa sababu ya kuwa na katiba ya hovyo ambayo hailengi usimamiz bora wa rasilimali pamoja na rasilimali watu.

Kiongozi yeyote hasa nafasi ua URAIS mwenye uzalendo wa dhati kabisa akisha apishwa tunaamini kabla ya yote ataanza na kutuletea katiba ambayo inatoa uhuru kwa kila idara na taasisi na kila muhimili kujitegemea na kuwa na nguvu ya kujitegemea isiyo pangiwa na muhimili mwingine ninu cha kufanya kwa sababu tu ya hofu ya uteuzi

Kwa maana hiyo kiongozi mwenye uzalendo wa dhati kabisa atahakikisha kwanza analeta katiba ambayo kila muhimili utakuwa na nguvu kubwa ya kuuwajibisha muhimili mwingine kwa mujibu wa katiba bila hofu wala woga pale muhimili mmoja unapo kwenda kinyume na utaratibu tulio jiwekea

Na hapo ndipo nchi hii itaanza kupata maendeleo tunayo yapigia kelele sasa ambayo hayawezi kutekelezwa na katiba hii ya hovyo hovyo ambayo kwanza ina toa mamlaka kubwa kwa mtu mmoja tena kwenye nafasi nyeti kabisa

kitu ambacho huyo mwenye mamlaka hayo siku akiwa mlevi akalewa mvinyo anaweza kuamua kutamka kwa maneno ya mdomoni tu kugeuza jumapili kuwa juma tatu na jumosi kuwa ijumaana kuifuta kabisa jumatano kwenye kalenda ya tanzania na ikawa sheria kwenye nchi yake na hakuna wa kumuuliza wala kumkosoa

kinyume na hapo huyo si mzalendo wa vitendo bali wa maneno na kwa vile kashaon
a madhaifu ya katiba iliyopo na hata rekebisha chochote kwa sababu na yeye itamlinda na maovu yake hivyo anataka nayeye kuficha maovu yake kupitia katiba hii ya kipuuzi inayo mlinda na kumpa madaraka makubwaaa ya kulevya.

Tumeshuhudia leo wakuu wamikoa na wilaya wanavyo jifanyia mambo kama walevi wa komoni na hakuna mamlaka ya kumuwajibisha na ikiwezekana kumtoa kwenye nafasi hiyo hadi mamlaka ya uteuzi iliyo pewa meno na katiba yetu ya hovyo itakapo jisikia kutoa maamuzi

kinyume na hapo wengine mtapiga tu keleee weeeee na bado mkuu wa mkoa au wilaya huyo anaendelea na manyanyaso yake tena huku akiwakejeli na kuwadharau na kuwadhiahaki kwa maanankuna baba yake asiye shindwa kamwe! hahahaaaa.

KATIBA BORA NDIO CHACHU YA MAENDELEO TANZANIA NA SI VINGINEVYO MAANA NDIO ITAKAYO SAIDIA KUZUIA HATA HUO UFISADI KUPUNGUA MAANA MAMLAKA ZA KUWAJIBISHA HAZITAKUWA NA HOFU KUMUWAJIBISHA HATA KAMA NI RAIS NDIYE FISADI KINYUME NA HAPO TUTAENDELEA KUCHEZEWA AKILI HADI YESU ARUDI
.
 
si wote ni mashahidi nchi hii ipo hapa ilipo kwa sababu ya kuwa na katiba ya hovyo ambayo hailengi
siyo kweli, wewe kama ni muumin wa katiba tambua kuwa kuna nchi hazina written katiba na zinatupa misaada
 
mkuu suala la katiba mpya sahau kwa sasa hii ndio Africa nakumbuka alishasema katiba mpya sio ahadi yangu
 
mengine mtalaumu marais bure.. mengine hata uyaundie katiba nzuri kiasi gani kama mtu si mzalendo utafua dafu mpk ukome! uende katiba hlf wasimamia katiba si wazalendo unafikiri tatizo ni watu ama katiba..?
 
Alishasema wananchi hawali katiba na mavyama. Labda tutafute maneno mengine ya kumshauri, ila tena alishasema hapangiwi. Kweli nakosa cha kumsaidia huyu jamaa. Nimechoka nimechoka kabisaa. Nikitoka Zimbabwe ntakuja kufafanua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katiba lazima iwe vichwani mwa watu na watende kufuatana nayo.
Kama watu hao hawawezi kusimamia katiba iliyopo, yafaa nini kudai mpya?
Hata hivyo, kuelekeza lawama kwa mtu mmoja (Rais), wakati kuna mihimili mingine ya dola (Bunge na Mahakama) ambayo kimsingi inawajibika kuhakikisha uwepo wa utawala wa sheria, inathibitisha uduni wa fikra katika taifa.
Kama kuna tatizo kubwa kama kuvunjwa kwa katiba na mihimili mingine hailioni, je kuna haja ya uwepo wake?
Raia wa kawaida wana haki ya msingi ya kuilinda na kuitetea katiba (msingi wa uzalendo), nini wanachofanya?
 
Kuna watu humu nadhani ni elimu ndogo ya uraia walio nayo ana ndio maana hata hawajui katiba ninini! Na inaumuhimu gani ? Na kwa nini iwepo.
 
Alishwajibu juu ya katiba mpya... wapigieni kelele wabunge wenu watende mnayotaka. Lawama zingine mnataka tu kuanzisha uzi nayo muonekane hampo nyuma...
Mtu kuandika ka unajua anachofikiria au kupanga kichwani eeeeeh.. makubwa mjidanganye wenyewe.. wabunge wapo
 
Alishwajibu juu ya katiba mpya... wapigieni kelele wabunge wenu watende mnayotaka. Lawama zingine mnataka tu kuanzisha uzi nayo muonekane hampo nyuma...
Mtu kuandika ka unajua anachofikiria au kupanga kichwani eeeeeh.. makubwa mjidanganye wenyewe.. wabunge wapo
Mmh!
 
Marais hao wakiwa viongozi ndipo watakapotuletea katiba stahiki lkn bahati mbaya Afrika hatuna viongozi bali tuna watawala.
 
Katiba lazima iwe vichwani mwa watu na watende kufuatana nayo.
Kama watu hao hawawezi kusimamia katiba iliyopo, yafaa nini kudai mpya?
Hata hivyo, kuelekeza lawama kwa mtu mmoja (Rais), wakati kuna mihimili mingine ya dola (Bunge na Mahakama) ambayo kimsingi inawajibika kuhakikisha uwepo wa utawala wa sheria, inathibitisha uduni wa fikra katika taifa.
Kama kuna tatizo kubwa kama kuvunjwa kwa katiba na mihimili mingine hailioni, je kuna haja ya uwepo wake?
Raia wa kawaida wana haki ya msingi ya kuilinda na kuitetea katiba (msingi wa uzalendo), nini wanachofanya?
Bunge na mahakama vipo kwa mujibu wa katiba hii hii mbovuu na ndio maana muhumili mmoja unateua kiongoz mkuu wa muhumili mwingine halafu tunadanganywa kuwa ni mihimili iliyo huru hebu elewa vyenpma maudhui ya andiko langu mkuu usiende pupa kwa vile unajua kujibu
mengine mtalaumu marais bure.. mengine hata uyaundie katiba nzuri kiasi gani kama mtu si mzalendo utafua dafu mpk ukome! uende katiba hlf wasimamia katiba si wazalendo unafikiri tatizo ni watu ama katiba..?
Ndugu wewe hivi unajua katiba ninini?? Na kwa nini ipo, unajua umuhimu wake na kazi zake ?? Hao wasio wazalendo kama katiba ikitoa uhuru wa kuwawajibisha walio juu kabisa endapo watafanya ujinga nani huku chini atafanya huo ujinga?? Mfano mdogo, katiba ikiondoa kinga ya rais kushtakiwa unadhani nani atakuwa radhi kuvurunda ili ashtakiwe? Na kila chombo kikawa huru kutekeleza majukumu yake kwa mshtakiw?

Leo mnalalama mikataba inayo liingiza taifa hasara kubwa ambayo ilisainiwa chini ya utawala fulani jee! Unadhani watu hao wangekuwa salama kama katiba ingetoa uhuru kwa vyombo husika kuchukua hatua kwa aliye kuwa kiongozi mkuu wakati huo?mbona wapo wana dunda kwa furaha? Ndugu tanua akili zaid ili uelewe maudhui ya andiko langu sio kujibu kwa sababu una jua kuna swali la kujibu
siyo kweli, wewe kama ni muumin wa katiba tambua kuwa kuna nchi hazina written katiba na zinatupa misaada
Hoja hapa sio kujua aina za katiba iwe written au unwritten, kizuri umekiri kwamba wana katiba inga si ya maandishi je! Umefuatilia vizuri muundo wao serikali ukoje na ugatuzi wao wa madaraka ?? Inama unataka na sisi tuingie kwenye unwritten constitution wakati ni taifa la written constitution?? Hebu fungua akili pia kuelewa vyema maudhui ya andiko langu mkuu usikurupuke kujibu kama hujaelewa mada, hapa sizungumzii aina za katiba bali nazungumzia katiba bora na inayo endana na mazingira yetu , na la muhimu kwako kwanza kasome kazi za katiba na umuhimu wake yawezekana unatoa majibu mepesi kwa sababu huna ulijualo kuhusu katiba za nchi.
 
UKAWA ndio walisusia katiba mpya
Ulitaka wabaki kujadili katiba ipi ya warioba iliyo kuwa na maoni ya wananchi au ya chenge,Sitta iliyo kuwa na matakwa ya CCM?? Tufanye kweli walisusia je walidhuru mchakato kuendelea? Mbona mchakato uliendelea je ulikomea wapi? Maana ukawa wao waliona isiwe shida kwa sababu yaliyo kuwa maoni ya wananchi yametupwa basi hawawezi kukaa bungeni kujadili maoni ya kina chenge na kundi lao
 
Nani anadanganya nani?
Kabla ya yote, wanahitajika watu wajitambue.
Kuandika katiba yaweza kuwa maandishi tu yasiyo na faida kama wananchi hawapambani kwa mujibu wa hiyo dhidi ya wanaoivunja.
Vita ya kutetea katiba ni takatifu kwa wanaoelewa.
Mwanadamu tangu asili ana ubinafsi na kipimo chatofautiana kwa mmoja na mwingine.
Ni lazima siku zote kulinda uhuru wako dhidi ya wengine hasa viongozi kwa ni wao ndiyo wenye mamlaka ya kuishi kwa jasho lako (ngao katika mapambano hayo ni katiba).
Kwanza mapambano kama umeingiliwa, mashambulizi yakijibiwa ngao katiba.
Mawazo au maandishi bila vitendo ni bure.
 
Mapambano pia yana mambo mengi huwezi kupambana na kudai haki ndani ya taifa ambalo vyombo vya dola nikimaanisha jeshi lina nguvu kubwa ya kusikiliza matakwa ya watawala kuliko matakwa ya sheria ni dhahiri wadai haki mtaumia na hapo ndio misingi ya kudai katiba ambayo jeshi linakuwa na mipaka ya kuzingatia matakwa ya watawala na matakwa yansheria na si ilivyo sasa watawala wana full access ya jeshi kama ambavyo ipo tanzania, nadhani wewe ni shahidi namba moja kushuhudia wadai haki wa tanzania huwa wanaishia wapi iwe kwa kuandamana ampna vinginevyo,

Fuatilia mataifa mengine yanayo jinasibu kuwa yakidemocrasia Yanapotokea maandamano au jitihada za wadai haki kwa mujibu wa sheria zao jee! huwa wanajibiwa kwa hoja kidemocrasia au kwa virungu na risasi za moto?
 
Back
Top Bottom