Ukishawagawa watu hutoweza kuwaongoza

Una maoni gani juu ya sytem ya 'Divide and rule'?
 
Sikuwahi kuona manufaa yoyote kwenye utawala wa JPM zaidi ya propaganda zake tu, Kama mwananchi wa kawaida doa kubwa litakalo mtesa mama ni kudandia kesi ya Mbowe
Hiyo ya mbowe ingekuwa ndogo kama ndani ya chama chake kungekua na nguvu iliyosimama lakini watu wengi ndani ya chama chake wamemchoka ila amebaki na sifa za kwenye majukwaa tu.

Pia huku chini hali ni ngumu biashara haziendi, pesa za shida zaidi kuwahi kutokea vitu bei juu huku watu wake wakitoa kashfa kwa mtangulizi wake na kujitengenezea ufisadi huku wakimsifia.

Kwa sasa ndani ya CCM Kuna kundi la kumshangilia mama hata akikosea na kumtukana magufuli
na kundi la kupamba na watukanaji hao na wale wa chadema wanaotukana magufuli na kwa uchache wakikitetea chama chao
 
Haya ni malalamiko kwa kundi mtoa hoja ameliita Sukuma gang, alipo libariki kundi hili ndipo ulipopoteza hoja yako kwani umeingia kwenye kundi lile wanapigania legacy za serikali iliyopitwa wakati legacy hujitetea yenyewe. Hata wewe ungepata uraisi baada ya Magufuli usingeyakubali yote ungependa kurekebisha hapa na pale. Awamu iliyopita na rais wake walikuwa ni watu wanaweza kukosea vile vile na kukubali kukosolewa ndio ustaarabu ambapo haukuwepo kwenye awamu iliyopita na kupelekea maumivu kwa watu wengi and kuligawa Taifa na ndio chanzo cha makundi haya ya Sukuma gang. Tukubali tu era imepita na hakuna cha zaidi ya kupiga kelele ili wakiona na kuamua kuyachukua ni uamuzi wao. Ila sijaona alipopotoka Rais wa sasa kurekebisha ni haki yake na matarajio ya watu hata kama wachache. Kutokuridhika kwa kundi hili sio mtazamo wa watanzania wote (60 million) bali kikundi which can be ingnore tu unless mtoa mada anihakikishie hiyo research aliifanya lini and what was the sample size iliyompelekea kusema watanzania wengi hawafurahishwi. CCM ni ilele poleni.
 
Wew ulipata teuzi endelea kupambana kusifia na kutetea ila muda unakuja sijui utasifia nani huko mbele
Tunachtaka kwa sasa hali iwe nzuri huku chini vitu vishuke bei namisha yawe nafuu nasio kuendelea kuumia huku nabmagalama makubwa ya kila kitu na pesa hakuna.
 
Mi sidhani kama anawashauri wazuri wa siasa..JPM kwa kiasi kikubwa ni kiongozi amegusa maisha ya watu wengi ingawa alikuwa ni babe, kisiasa kuamua kupambana nae amepoteza wafuasi wengi sana sababu ukweli ni kwamba JK watu hawamkubali. Kipimo kizuri ni chanjo ya corona..ajiulize kwann watu hawachanji kama wanamsikiliza, so yeye suala la magufulia angetumia busara sana sababu linaweza kuwamaliza kisiasa ikitokea kuna kundi likajitenga esp watu wanaotoka kanda ya ziwa na wakawa na ushawishi, uchaguzi utakuwa mbaya sana. Ngoja tuone..tunaokaa mtaani tunajua hisia za watu. Watu hawataki tena viongozi legelege.
 
JPM anakumbukwa kwa kutufanya Watanzania Kufurahi na kuona fahari kuuana Sisi kwa Sisi kwa sababu za tofauti za Kisiasa.
 
Nimepata uteuzi gani?
 
Hana atakachokipoteza ,yy mwenyewe anajua fka ,lazma wajumbe watamla kichwa ,asbh mapema ,kwenye kura za maoni.na hata Kama atafanyiwa support ,wapga kura wa nje wataigeuka ccm,na kutoa support kwa opposition !!
 
Ndani ya ccm ni kweli hatapata kura ila ukweli ni kwamba ndiye atakuwa candidate wa ccm. Hii yote ni faida ya mfumo mzuri unaomlinda mwenyekiti ndani ya chama alioasisi Magufuli.
Ni kweli pia nje ya ccm baada ya kupitishwa wanaccm watamgeuka ila pia atashinda kwa sababu ya mifumo mibovu ya upigaji na uhesabuji kura aliyoasisi Magufuli. Hivyo no way, huyu mama ni raisi wetu mpaka 2025 na akitaka kuendelea zaidi ya hapo hakuna wa kumzuia. Effect ya Magufuli kwa nchi itatusumbua muda mrefu sana vinginevyo Samia aamue kuwa muungwana alegeze mifumo aliyorithi toka kwa mwenda zake
Hana atakachokipoteza ,yy mwenyewe anajua fka ,lazma wajumbe watamla kichwa ,asbh mapema ,kwenye kura za maoni.na hata Kama atafanyiwa support ,wapga kura wa nje wataigeuka ccm,na kutoa support kwa opposition !!
 
Umemaliza kila kitu,,,maisha magumu khaaaa
 
Mwandiko wa la nne B
 
Heri nusu shari kuliko shari kamili
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Uko sahihi mkuu, lakini kuna mtu bingwa wa kutukana wenzie kama Jiwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…