Ukisikia komando unafikiri ni mwanajeshi wa namna gani!?

Ukisikia komando unafikiri ni mwanajeshi wa namna gani!?

Mbute na chai

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
564
Reaction score
593
Habari wanajamii.

Nimeona ni shiriki pamoja nanyi kuhusu maana halisi ya neno komando (Commando) na namna linavyotumika jeshini..
Neno komando lilitumika na utawala wa kiholanzi (dutch cape colony) katika nchi ambayo sasa huitwa Afrika ya Kusini. Kulianzishwa vikundi vya kaburu (boers) ambavyo vilitakiwa kuwa vimejiandaa kivita muda wowote vitakapotakiwa kuwa hivyo. Zana zao zilikuwa bunduki aina ya gobole (rifle) na matumizi ya farasi na utekelezaji wa masharti haya ulijulikana kama mfumo wa komando (commando system). Hivyo basi, vikundi vilivyoanzishwa kwa mfumu huu vilijulikana kama komando. Hii humaanisha kwamba komando haikumaanisha mtu bali kikundi. Hivyo dhana halisi ya komando ni kikosi kinachoshambulia kwa kuotea/kuvizia (raid) na kisha kutoweka na ndivyo walivyofanya kaburu wakipigana na Muingereza.

Aidha, maana ya sasa ya neno komando inatokana na kutekwa kwa waziri mkuu wa Uingereza Winston Churchill ambaye alivutiwa sana na uwezo wa vikosi vya komando (commando units) vya kaburu. Baada ya kuachiwa waziri mkuu huyu, kwenye vita vya pili vya dunia, aliamrisha jeshi la uingereza kuunda vikosi vidogo kama vya komando vya kaburu ili viharibu mwasiliano ya wanajeshi wa ujerumani n.k. Hivyo vikosi hivyo vilijulikana kama komando units.

Hivi sasa neno komando halitumiki sana jeshini. Aidha, kwa muktadha wa sasa vikosi vyenye mafunzo maalumu kama vile kushambulia maeneo hatarishi huitwa vikosi maalumu (special forces). Vikosi hivi huwa vya wanajeshi wachache wenye mafunzo maalumu ya intelijensia, matumizi bingwa ya silaha, kuokoa, kuishinda hofu hata ya kifo, kukaa kimya hata kwenye mateso ya mwili na saikolojia, n.k.

Pia mwanajeshi yeyote anayeenda kwenye operation hatarishi huweza kuitwa komando. Hivyo basi komando siyo cheo bali ni aina ya vikosi vya jeshi ambavyo hivi sasa vinaitwa vikosi maalumu (special forces). Kwa dhana rahisi special force ni vikosi vinayoondoa vikwazo kwaajili ya wanajeshi wengine kuendelea na mashambulizi.

Kwa sasa pia komando hutumika kuamsha morari ya wanajeshi wanapokuwa kwenye mafunzo au jaramba ndiyo maana unaweza kukutana na wanajeshi wakiimba komando, komando, komando…
 
Na wale wanaopasua tofali pale uhuru ni kina nani mkuu?? Na wanavyeo gani huko jeshini maana huitwa makomando!!
 
Komandooo komandooo
Special unit/force maranying hutumika kwa baadhi ya task flan tuu. Mfano scout, kufuatilia mambo flan hasa ya kiuchumi na hata kisiasa na raid
Komando hasa hapa tanzania hawatumiki sana ila baadhi huingizwa kwenye special task ambazo huwa na muingiliano wa watu mbalimbali toka majesh mbal mbal
 
Ni Bora niangalie movie ya Bushman kuliko mapicha ya Hollywood
 
Back
Top Bottom