Ukisikia ulivyosemwa kipindi haupo tena na ambao ulijua wangekutetea hata usipanic(hamaki), ndivyo ilivyo kwenye jamii maskini ✍️

Ukisikia ulivyosemwa kipindi haupo tena na ambao ulijua wangekutetea hata usipanic(hamaki), ndivyo ilivyo kwenye jamii maskini ✍️

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
UKISIKIA ULIVYOSEMWA KIPINDI HAUPO TENA NA AMBAO ULIJUA WANGEKUTETEA HATA USIPANIC( HAMAKI), NDIVYO ILIVYO KWENYE JAMII MASKINI ✍️

Moja ya sifa kubwa ya maskini wa fikra ni kuongelea wengine yaani kwa lugha rahisi tuseme Majungu.

Ondoka usemwe huu ni msemo maarufu sana wenye maana kuwa usipokuwepo utasemwa mengi sana tena na wale ambao ulihisi wangekutetea ila hupaswi kupanic( hamaki) wala kufokeana na watu maana ukifanya hivyo basi nawe utakuwa maskini tu wa fikra kama wao na tena utakorofishana na wengi.

Ukirudi ama iwe kazini au kwenye jumuiya flani baada ya kutokuwepo kwako kwa muda fulani utapokea maneno mbali mbali kwa namna ulivyosema sasa hupaswi kupata ghadhabu na kuanza kufoka foka hovyo au kununiana na watu bali fanya yafuatayo:

# Tambua upo na jumuiya maskini ndio maana wana huo muda wa kupiga majungu sasa usipoishi nao kwa akili nawe utafanana nao.

#Usitake kujua ulisemwa nini kipindi haupo na hata ukiletewa habari hizo na rafiki yako mbea usimpuuze wala kumkatisha tamaa bali msikilize ila usiyafanyie kazi la sivyo yawe ya kuhatarisha uhai wako.

#Tambua kuwa ni kawaida kwenye jumuiya maskini mtu kusemwa akiwa hayupo na watakaokuletea habari hizo nao walihusika sema tu wanataka kukuonyesha kuwa wao ni marafiki zako wazuri.

HASARA ZA KUENDEKEZA UMBEA KWENYE JAMII

#unajiongezea mambo mengi ya kufanyia kazi ilihali hayana maana kwa sababu badala ya kufikiria ubunifu wa harakati unakuwa unafikiria tu kwanini flani akuseme vibaya ilihali ni rafiki yako.

#Utakuwa na tabia za kike (kama wewe ni wa kiume) kitu ambacho ni hatari kwa kijana wa kiume kuwa mbea kwa sababu mambo ni mengi ya kufanyia kazi huo muda wa kutafuta na kusambaza umbea unatoa wapi,? La sivyo umbea uwe ndio kazi yako inayokupa kipato .

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#fikia ndoto zako
 
Halafu unakuta ni rafiki wa kuzikana kabisa unaanza kujiuliza huyu mwamba Bora ningemtongoza Tu nimle kiboga
 
Wambea na wadaku mkuje hapa kuna ujumbee wenu, mkisindikizwa na washirika wenzenu Wanafikiii.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unakuwa na wasiwasi mwingi.. hata ukiwa kijiweni unaogopa kutoka kidogo...😁
"Nilivyotoka walisemaje?
"Je wakati narudi walisemaje?😁
Kikubwa ni kuishi huu msemo
"Utachelewa sana kufika safari yako iwapo utasimama na kurusha mawe kwa kila mbwa anayekubwekea ."
 
Unakuwa na wasiwasi mwingi.. hata ukiwa kijiweni unaogopa kutoka kidogo...[emoji16]
"Nilivyotoka walisemaje?
"Je wakati narudi walisemaje?[emoji16]
Kikubwa ni kuishi huu msemo
"Utachelewa sana kufika safari yako iwapo utasimama na kurusha mawe kwa kila mbwa anayekubwekea ."
Nimeupenda huu msemo, [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Kusemwa kasemwa Yesu itakuwa hao mbugila mbugila wa mataifa??!!

Ukisemwa ujue wewe ni kiumbe uliyekamilika.
Halafu “Una kitu” kinachofanya usemwe.!!
“Mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe” Ishi humo
 
Back
Top Bottom