Umesikiliza lakini I doubt kama ulimpata neno kwa neno kwa sababu endapo ungempata neno kwa neno, ungegundua Eymael ameukashifu uongozi wa Yanga, Mashabiki wa Yanga, Simba, TFF, na Tanzania kwa ujumla!!
Kwa mfano kuna sehemu amesema "I'm not enjoying this country. People are uneducated." Sasa wewe usie Yanga unachomokaje kwenye kauli hiyo?! Kwani hiyo "this country" ambayo watu wake ni "uneducated" ni nchi ya Yanga peke yake?!
Kama mashabiki wa Yanga ni wapiga kelele tu kama nyani au mbwa, na wahajui lolote kuhusu soka; je wewe shabiki wa Simba una tofauti ipi na shabiki wa Yanga? Kama shabiki wa Yanga ni sawa na Nyani au Mbwa, wewe unakoseje hapo kuwa nyani au mbwa?! What's so special wanachofanya mashabiki wa Yanga ambacho mashabiki wa Simba hawafanyi?
Kwamba TFF ipo mikononi mwa Simba, na kwamba kazi yao ni kuipendelea Simba, ina maana kwako huo ndio kweli sio?! Kwahiyo unataka kutudhihirishia hapa kwamba ni kweli mnabebwa na TFF?!
Kwamba away pitches ni kama viwanja vya Daraja la 7 au la 8 kule Ulaya; yaani kwa akili yako unaona huo ni ukweli dhidi ya Yanga?! Kwani Yanga ndie mmiliki wa hivyo viwanja?!
Hivi Luc Eymael huyu aliyewahi kufundisha DRC, Rwanda, na Kenya unataka kusema huko alikutana na viwanja vizuri?!
Btw, hivi ni taifa gani lenye mashabiki wa soka wanaojua technical side of soccer hadi aseme mashabiki wa Yanga hawajui lolote kuhusu soka?! Nyie mashabiki wa Simba mmesomea wapi taaluma ya soka inayowafanya muwe tofauti na mashabiki wa Yanga?!