Ukisikiliza press ya Mbowe na ukisikiliza press ya Mdee pana Igizo la Kanumba

Ukisikiliza press ya Mbowe na ukisikiliza press ya Mdee pana Igizo la Kanumba

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
930
Reaction score
1,300
Wakuu heshima kwenu...ukisikiliza press ya mbowe na ukisikiliza press ya Mdee hapa pana igizo la kanumba.

Nahiisi michezo umechezwa hivii Mbowe amebariki majina kimya kimya au Kamati Kuu imepitisha hayo majina kimya kimya wakayapeleka NEC kwa mujibu wa press ya NEC.

Sasa CHADEMA itaonekanaje kwa wanachama na Wananchi kwa ujumla kwa sababu wamesema hadhalani kuwa wanapinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu hivyo wangepitisha majina wasinge eleweka.

Kama kawaida Mbowe akamtuma Mdee alitibue kwa kwenda kuapa Bungeni baada ya hapo Kamati Kuu itawavua uwanachama, ila wale Wabunge watakata rufaa kwenda Baraza Kuu hapo Baraza Kuu litapinga maamuzi ya Kamati Kuu.

Kwa upande mwingine watashinda wakina Halima Mdee hii italeta hoja mbili, moja itavumisha kuwa CHADEMA kunademokrasia ya ukweli, pili Mbowe na Kamati Kuu watakuwa wamejitoa kiaina kwa kusema Wanachama ndio wamebaliki.

Hivyo yaishe tuangalie Uchaguzi ujao.
 
Mapema sana kujua matokeo ya kesi ingawa kuna mwelekeo wa WIN WIN 50/50
 
Nch hii mko wachawi wengi sana. Elimu haiwasaidii? Toa evidence siyo kuongea kwa kukisia. You have hypothesis then prove with your evidence. Huna evidence usinongee; inabaki kuwa gabbage, metaphor
 
Hao kamati kuu ndio walienda kumtoa Nusrat Hanje ili akaape?Endelea kuota,hao akina Halima wajiunge tu CCM maana CDM ndio kwaheri hivyo!
Mwisho wa match tutaelewa mkuu, haina haja kutumia nguvu kubishana
 
Kama ni hivyo, Spika na Bunge lake pamoja na NEC ndio watakuwa wameuzwa, wao ndio itambidi waende mahakamani kujiosha na Hilo,
 
Mimi nahisi majina yalipelekwa ila orodha ilikuwa kubwa kuliko idadi ya watu 19, kumbuka majina huwa yanazidishwa ili yakae kama akiba inapotokea mbunge amefariki basi anachomolewa anayefuatia toka pale walipoishia kuteuliwa hukohuko NEC bila chama kulazimika kupeleka jina upya; kumbuka alipofariki Regia aliteuliwa mwingine kutoka orodha iliyokuwepo NEC.

Ilitakiwa NEC wateue kuanzia namba 1 hadi 19 kwa kufuata series. Sasa nahisi baadhi ya hawa walioteuliwa hawakuwemo katika series ya 1 hadi 19 ila walikuwa baada ya namba 19. Inaonyesha Mdee alirekebisha series ya orodha kwa kuwachomoa baadhi waliokuwa ndani ya 19 na kuwaweka ambao walikuwa katika orodha lakini mbali i.e. baada ya namba 19. Hapa ndipo kiini cha mgogoro kati yao. Kwa maneno mengine wamezidiana kete.

Mgogoro utakwisha kwa baadhi kutolewa katika orodha na wengine wapya kuingizwa katika orodha ya namba 1 hadi 19. Win win situation
 
Kuna watu mna akili kisoda sana.Siku nyingine ifanye akili yako ifanye kazi ya kufikiria sio ifanye kazi ya kulala kama ulivyoleta majungu hapa.
 
Wakuu heshima kwenu...ukisikiliza press ya mbowe na ukisikiliza press ya Mdee hapa pana igizo la kanumba.

Nahiisi michezo umechezwa hivii Mbowe amebariki majina kimya kimya au Kamati Kuu imepitisha hayo majina kimya kimya wakayapeleka NEC kwa mujibu wa press ya NEC.

Sasa CHADEMA itaonekanaje kwa wanachama na Wananchi kwa ujumla kwa sababu wamesema hadhalani kuwa wanapinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu hivyo wangepitisha majina wasinge eleweka.

Kama kawaida Mbowe akamtuma Mdee alitibue kwa kwenda kuapa Bungeni baada ya hapo Kamati Kuu itawavua uwanachama, ila wale Wabunge watakata rufaa kwenda Baraza Kuu hapo Baraza Kuu litapinga maamuzi ya Kamati Kuu.

Kwa upande mwingine watashinda wakina Halima Mdee hii italeta hoja mbili, moja itavumisha kuwa CHADEMA kunademokrasia ya ukweli, pili Mbowe na Kamati Kuu watakuwa wamejitoa kiaina kwa kusema Wanachama ndio wamebaliki.

Hivyo yaishe tuangalie uchaguzi ujao.
great thinker
 
Back
Top Bottom