Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni. Eti Askofu Gwajima anataka kuwapeleka Tokyo Japan wacheza rede wa Msasani

Maigizo ya ufufuo na uzima... uliona wapi yakakoma!?
 
Na kingreza cha kimtindo
 
jumapili yuko mikocheni ,sijui nako atawaahaidi kuwa peleka wapi?
 
Naona kawe wameanza na akina mama kupitia rede kuwarubuni
 
Gwajima ni kama amechanganyikiwa
 
Mama yake tu alishindwa, sembuse Amina Chifupa. Na watu walimsema sana siku ya msiba wa mama yake.
Alianza kwa kudai angemfufua Amina Chifupa na hakuweza. Kisha kwa hadaa akadai kamfufua mtu kanisani kwake na video ya tukio hilo itakuwepo mitandaoni. Lakini mama yake mzazi alipofariki miaka michache iliyopita badala ya kumfufua ili awathibitishie walimwengu kuwa anao uwezo wa kufufua wafu yeye akadai hana haja ya kumfufua kwa vile ameshakuwa mzee sana hivyo amwache tu aende akapumzike kwa baba yaani Mungu! Buswelu sekondari (iliyo mkoani Mwanza) mwaka huo ilikuwa na mkosi sana wa kutoa intake iliyojumuisha watu wawili hatari sana kwenye jamii yaani Gwajima na Baba God (Godfrey Mugyabuso) aliyekuwa na kanisa lake pembeni mwa barabara ya kwenda hospitali ya Bugando na baadae Kangaye huko jijini Mwanza.
 
Yeah nailed it.
 
Amegundua wapiga kula wake wengi, ni mazuzu! Hawana passport, lakini wanaamini wataenda Japan! Hata Iringa, Arusha hawajawahi fika Ila wanaamini Asia watafika?
Kwani ili uende Japan ni lazima kwanza kufika mikoa uliyotaja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…