Ukistaajabu ya tozo za mabenki utaona tozo ya kuongeza salio kwenye laini za simu

Juzi niliweka vocha ya 5000 voda,ile namaliza kuweka bahati mbaya

Mteja akaingia nikaweka simu mfukoni nikamuhudumia,sijamalizana nae vzuri

kaja mteja mwingine,kazi zikaingiliana pale ubusy ukatawala,baada ya kitu kama nusu saa

nikakumbuka nimeweka vocha ila sijajiunga,acha nijiunge nikapga menu direct kufata kifurushi changu.

nafika najiunga inakataaa naambiwa salio halitoshi,kuangalia salio nakuta kuna 4,200 nilikasirika sana ila nikapotezea nikaenda nunua vocha ya buku nikaongezea.

leo ndio nakutana na haya ya mwigulu,niki konect dot zangu napatA Majibu hawa wajinga hii system hawajaianza leo, sema sasa hv ndio wameamua kutujulisha kuwa wanatufyekaga vocha zetu.

kusingizio ni kodi kwa kujengea shule.... fresh tutakutana!
 
Utafanya nn?
 
Umenena vema Sana ndio maana majuzi hapa rais wa Zambia kasema hilo kwamba watu wanadai kiongozi ni mzuri lakini anazungukwa na watu wabaya mwisho akasema wanao mzunguka ndio uhalisia wake mwenyewe huyo kiongozi.
Kuwepo na vikundi vya wanafiki wa sampuli hii kwenye kudai haki kunafifisha sana harakati kama sio kuziua kabisa, kwasababu inaboa sana pale unapodhani fulani uko nae pamoja kwenye mapambano...

Kumbe mwenzio anapambana kwasababu adui yenu sio mwenzake, akipatikana mwenzake akafanya kama adui wa mwanzo anamlinda, huu unafiki ni wa kulaaniwa kote duniani mpaka mbinguni.
 
Mtalia sana mwaka huu, na bado
 
Ndiyo, hana uwezi wa kutafakari na kuchanganua. Kila kitu kwaje ni ndiyo.

Mwendazake aliwakatalia mawaziri na watendaji wengine wazi. Kwa mfano mara kadhaa alipotakiwa kuruhusu umeme kupanda alisema hapana. Na ikawa.

Kabla ya Magufuli kuingiza umeme tulifika pabaya. Gharama kubwa na bila hongo bado hujapata umeme.

Samia ameshindwa kuwaambia waandamizi wake ukweli. Kila kitu mkakitizame kisha hageuki kuona wananchi tunavyoumia kwa msalaba wa kodi na tozo.
 
Kaz ipo
Ni dhahiri PhD Mwiguru atapita tena bila kupingwa katika uchaguzi wa 2025 kwa msaada wa NEC
 
Lawama yangu kubwa ni kwa sisi wananchi tuliowachagua hao wapiga meza. Imefikia mahali badala ya wao kuwa watetezi wa wananchi wanyonge, wao ndio wanaonyesha serikali mahali pa kukata tozo (refer zunguzubgu). Hii itoshe kutupa hasira 2025 wabunge wa namna hii wabakie nyumbani tupate wawakilishi sahihi.
 
Wamegundua kuwa baada ya tozo watu wakapunguzuza kutumiana pesa sasa tuone kama salio la vocha hamtaongeza.

Vv
Kwani kuongeza salio lazima? Tunaacha vile vile nafikiri wameona watu wamepunguza kupeleka hela benki Sasa ni vocha kwa vile vocha sio chakula tutapunguza sana matumizi yetu
 
PhD feki katika ubora wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…