Ukistastaajabu ya mafuta na maji ya upako hapa bongo. Pasta Ng'ang'a atupa sadaka za waumini kisa ndogo

Omukisa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
642
Reaction score
1,305
Mchungaji wa Neno Evangelism Centre James Ng'ang'a atupilia mbali pesa zilizokusanywa kama sadaka kutoka kwa waumini wake wakati wa ibada.

Katika video iliyoshirikiwa na Qare Jane kwenye TikTok, mchungaji huyo alionekana akiiangalia kwa dharau sadaka hiyo. Wakenya walioshuhudia video hiyo walionyesha kutoridhika kwao, wakisisitiza kwamba mtumishi huyo wa Mungu hastahili kutupa mbali michango iliyotolewa kwa bidii na waumini wa kanisa.

James Ng'anga ambaye hakufurahishwa na sadaka walizotoa waumini. Mchungaji huyo aliyekasirika aliona jinsi sadaka ilivyokuwa ikikusanywa, na baada ya kipindi hicho kukamilika, aliichukua na kujiuliza kwa nini haikuwa nyingi kama alivyotarajia.

"Wakenya Waduwazwa na Pasta Ng'ang'a Kuudhika na Sadaka ya Waumini Akisema ni Kidogo:"Nini Hii Sasa?" - Tuko.co.ke" Wakenya wachanganykiwa baada ya pasta Ng'ang'a kudharau sadaka akisema ni kidogo
 
Yeye mwenyewe anajua kutafuta pesa ni mziki mzito ndo maana aliona tofali ni zito akakimbilia kushika biblia ili atapeli watu
 
Waumini wamelala usingizi wa pono hawashutuki au ndiyo Ile wanasema wana masikio hawasikii na wana macho hawaoni.
Ngoja waendelee kumchangia tapeli wakija kustuka mwamba ashatajirika zaidi
 
Mchungaji wa Neno Evangelism Centre James Ng'ang'a atupilia mbali pesa zilizokusanywa kama sadaka kutoka kwa waumini wake wakati wa ibada.

Katika video iliyoshirikiwa na Qare Jane kwenye TikTok, mchungaji huyo alionekana akiiangalia kwa dharau sadaka hiyo. Wakenya walioshuhudia video hiyo walionyesha kutoridhika kwao, wakisisitiza kwamba mtumishi huyo wa Mungu hastahili kutupa mbali michango iliyotolewa kwa bidii na waumini wa kanisa.

James Ng'anga ambaye hakufurahishwa na sadaka walizotoa waumini. Mchungaji huyo aliyekasirika aliona jinsi sadaka ilivyokuwa ikikusanywa, na baada ya kipindi hicho kukamilika, aliichukua na kujiuliza kwa nini haikuwa nyingi kama alivyotarajia.

"Wakenya Waduwazwa na Pasta Ng'ang'a Kuudhika na Sadaka ya Waumini Akisema ni Kidogo:"Nini Hii Sasa?" - Tuko.co.ke" Wakenya wachanganykiwa baada ya pasta Ng'ang'a kudharau sadaka akisema ni kidogo
Pasta Ng'a Ng'a na njoo bongo, makondoo wa Kenya wameamka hao, Kondoo wa uku bongo mpaka Leo wanauziwa matope na wananunua.
 
Yeye mwenyewe anajua kutafuta pesa ni mziki mzito ndo maana aliona tofali ni zito akakimbilia kushika biblia ili atapeli watu
Ilibidi nao walipe kodi ya serikali maana hii ni biashara.
 
Back
Top Bottom