Ukitafakari mazingira anayopitia Mwalimu kwenye baadhi ya Shule za Private utalia machozi

Jaaaa Kali mujini
 
Mwaka 2006 mwalimu wa Diploma alikuwa analipwa Tsh 146,000/= serikalini. Hiyo 50k kwa serikalini ilikuwa miaka ya 90.
mwaka 2010 mwalimu wa grade A alianza na basic salary 170,000 serikalini, kwa sasa huko private iko chini haizidi laki mbili kwa wa msingi. Wa sekondari ndio analambishwa laki mbili kwa mbinde sana miaka hii tena bila incriment wala posho . Wamiliki wa shule binafsi wengi wao wanaendesha shule zao kihuni na kitapeli kwa walimu, angalau kidogo kwa shule za misheni na taasisi zingine zenye heshima kidogo zinajali maslahi ya walimu. Serikali ndio muajiri bora kwa walimu kuliko hao wengine
 
Inasikitisha sana. Kuna shule zingine mmiliki anampa uongozi toto lake huni lisilo na busara kuendesha shule. Pale Tusiime kuna toto bonge lilikuwa mtu wa dili hadi kwa biashara ya familia yao. Ukiwa supplier lazima umkatie kitu kidogo au anaongeza bei ili ale cha juu.
 
Ili tatizo limeanzia wakati wa Serikali ya awamu ya 5 ilipositisha Ajira za walimu na walimu kuzagaa mitaani kuwa wengi kuliko mahitaji ya Shule Binafsi, lakini Serikali ingekua ina ajiri walimu kama wakati wa awamu ya 4 ilivyokua inafanya, Shule binafsi ingekosa wawalimu na ingewabidi watafute walimu kutoka nchi jirani kama miakq ya Nyumba, Sasa hivi walimu kutoka Kenya hawaji kwasababu Serikali ya CCM haitaki kuajili walimu na kufanya walimu kushuka bei kwenye sekta binafsi, Bidhaa ikiwa nyingi sokoni na wanunuzi ni wachache lazima itashuka bei na itajiuza bei ya kutupa,ndiyo Biashara ya Ualimu ilipofikia chanzo chake ni Magufuli kustopisha Ajira kwa Walimu na uku vyuo vikiendelea kuzalisha walimu, matokeo yake wanakua wengi na unashindwa kuwapa ajira wote.
 
huu mtindo wa kuwapa uongozi wa juu ndugu upo sana tu kwa hizi shule za private. Wakikosa ndugu anapewa mwalimu boya ili awe anapeleka umbea kwa mmiliki kuwa kuna walimu wanajadili mishahara ni midogo. Cha ajabu hizi shule zimejaza walimu wasio na taaluma ya ualimu mradi tu wanaweza kubabaisha wanafunzi kwa kiingereza kibovu
 
Kuna taasisi moja huku tabata ilimbikiza mishahara to mwaka jana ikiahidi kulipa mhura wa kwanza lakini hola
 
Uongo unawasaidia nini?
 
hiyo awamu ya nne na ya tatu walimu walikuwa wa kutafutwa kwa tochi mchana kweupe. Serikali za awamu hizo ilibidi zije na mkakati wa kupata walimu hata kwa kuchukua walihitimu miaka mingi nyuma
 
Ndio maana kila siku nawaambiaga watu msijistress kupeleka watoto wenu shule za Ems . Haya sasa twende kazi, kimbia haraka sana nenda kawatoe watoto wako shule ya Ems warejeshe Kayumba. Thank me later πŸ™πŸ™πŸ™
 
Private sector yetu tasnia ya elimu na afya inaajiri watu waliofell shida iko apo.
 
Awamu za mkapa na kikwete kumpata mwalimu anazagaa mtaani bila ajira ilikuwa shughuli pevu. Walikuja na mikakati yao kupata walimu kwenda kufundisha mashuleni na hawakutosha. Walikuja na crash education maarufu kwa jina la utani voda fasta, zinatangazwa nafasi bure kwenda chuo cha ualimu unasoma miezi nane tu kisha unapangiwa kituo matokeo ya mtihani yatakukuta uko kazini hata ukifeli utarudia pepa ukiwa kazini. Kikwete naye akaja na fursa zake yeye alichukua mpaka waliomaliza sekondari miaka ishirini iliyopita akaruhusu wasomee ualimu na kupangiwa vituo vya kazi mara umalizapo kozi ya miaka miwili au pungufu ya hapo. Matokeo yatakukuta uko kazini. Tofauti na sasa walimu wamejaa mitaani na wamiliki wa shule binafsi wanawapata kwa bei chee, wanawapangia mishahara watakavyo uwe na diploma au degree huvuki laki mbili, ukiringa anachukuliwa mwingine jobless. Thamani ya walimu imeshuka sana
 
100% fact
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…