Kila mtu kapewa kipaji na talanta yake,
Wapo watu ni kama wajumbe wa mwenyezi MUNGU kwaajili ya wengine, ndiyo hao unaokuta wameajiri zaidi ya watu elfu tano kwenye makampuni yao, mara nyingi si watu wa starehe.
Wapo watu kazi yao ni kutumia tu pesa tu ndiyo maana unakuta mtu Hana hata kibanda (nyumba) lakini Kila weekend anawapiga watu beer Haina mfano.
Wapo watu ambao baada ya kupata kitu alicholenga basi hujiona kamaliza maisha hivyo, hushindwa kuvumbua miradi mipya. akiwa na sehemu ya kuishi , akiwa na usafiri na uhakika wa kusomesha watoto wake basi anakuwa Hana shida tena Wala hajitumi.
Wapo ambao wanatamani kuwa maboss , yaani wawe na kampuni zao, lakini inakuwa ngumu kwani wamepangiwa kuajiriwa maisha yao yote, (kutumwa) hata wakianzisha biashara na miradi yao basi inakufa tu.
Wapo ambao hawatumii nguvu kwenye kutafuta, haibi Wala hadhulumu lakini mifereji yake ya hela inatiririka tu, Kila analopanga linaenda sawa ,yaani anaweza kuishi maisha yoyote yale anaweza kufanya starehe zote Duniani.
Wapo wanaotamani kuwa juu zaidi ya juu lakini mwenyezi MUNGU hajawapa riziki waitakayo, hata waibe na kupora vipi , bado huishia kuwa na maisha magumu.