Ukitaka kuchonga kinyago kwanza lazima upate mpingo

Ukitaka kuchonga kinyago kwanza lazima upate mpingo

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Mpingo ndio unafaa kwa kuchonga kinyago. Hivyo hivyo,tukitaka kujenga Taifa lazima kwanza tuwe na watu wanaoridhia kuwa Taifa moja.

Vinginevyo, mahusiano katika Taifa yanakuwa kama ndoa ya kulazimishwa.

Modern state inahitaji Kiongozi awe mmoja tu katika mioyo ya watu. Nilipokuwa China, wakati wa Mao,walikuwa wana wimbo mmoja wanaimba,"Mao Tse Tung is the Red Sun in our hearts." Mao ndiye Jua Jekundu kwenye mioyo yetu. Kiongozi wa modern state anatakiwa kuwa Jiwe Jekundu katika mioyo ya watu.

Lakini sasa yapo mazungumzo ya kubadilu Katiba ambapo mkazo wake ni kupunguza madaraka ya rais. Hiyo ni sahihi?

Sheria nzuri zinaweza kutungwa watu waishi kwa mwafaka. Lakini kwanza lazima iwepo the will to build a nation. Azma ya kuwa Taifa moja.

Ukitaka kuchonga kinyago lazima kwanza upate mpingo.
 
Hiyo ndiyo kazi aliifanya Baba wa Taifa kwa uaminifu mkuu na bidii jambo ambalo mataifa ya Afrika mengi hayajaweza lakini warithi wake ama kwa fikra duni au kwa ajili ya nafsi za uchoyo hususan, kudhani ukisha kuwa kiongozi basi umeshakuwa muungu, maono na mtazamo wako au chama chako ndiyo maono na hekima ya Taifa. Tuamini kuwa kuna siku Mwenyezi Mungu Atatuletea tena kiongozi wa kiwango cha Nyerere!
 
kubadilu Katiba ambapo mkazo wake ni kupunguza madaraka ya rais. Hiyo ni sahihi?
Ni sahihi Sana. Jiwe aliwatesa na kuwabagaza wananchi kwa kipimo kisichoelezeka. Ni kwa kupitia yeye jiwe ndiyo maaana hata ccm wameiona ipo haja ya kupunguza madarka ya rais.

Atakuja rais chizi zaidi ya jiwe ataua jamii fulani ya watanzania. Jiwe aliwachukia wachaga sana zaidi ya Sana. Akawatumbua wote toka bitenho nyeti kwa hila tu.

Katiba ungelikuwa bora wamasai wasingeondolewa Loliondo. Rais angezuiwa na mahakama.
 
Back
Top Bottom