PreGE2025 Ukitaka kujua CCM ni wajinga, No Reform No Election ni kwa Faida yao na Taifa ila wanaikataa!

PreGE2025 Ukitaka kujua CCM ni wajinga, No Reform No Election ni kwa Faida yao na Taifa ila wanaikataa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ukitaka kujua CCM ni wajinga sana ni uhalisia kwamba, Kampeni wanayoipinga ya No Reform No Election, kimsingi inawasaidia wao zaidi na inafaida kwao na kwa Taifa.

Kampeni ya No Reform No Election ina faida zifuatazo kwa CCM na Taifa kwa ujumla;

1. Endapo Uchaguzi utahairishwa, Utawala wa Awamu ya Sita utaendelea kuwepo madarakani hadi hapo Katiba Mpya itakapopatikana. Hii inamaanisha Rais ataendelea kuwa huyu huyu, Wakuu Wa Mikoa na Wilaya hawa hawa, Wabunge hawa hawa na Baraza la Mawaziri hili hili. Spika atakuwa huyu huyu na Viongozi wengine wote wataendelea kuwepo kwenye nafasi zao.

2. Endapo watakubali kufanya Reforms saivi, Kiongozi wao yaani Mwenyekiti wao ataingia kwenye rekodi za Tanzania zitakazosomwa na vizazi vyote vya Tanzania kuwa Rais wa kwanza aliyekubali na kuitisha Mchakato wa Katiba Mpya hadi akahairisha uchaguzi. Pia atakumbukwa kama Rais aliyefanikisha kuwepo kwa Katiba mpya na bora zaidi kuwepo Tanzania.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

3. CCM wakikubali kuhairisha Uchaguzi sasaivi na kuanzisha mchakato wa Katiba sasa watajiongezea kuaminiwa mara elfu moja zaidi kwa Watanzania. Hili tu litawafanya kutohitaji wasanii wa filamu au Wanamuziki kujaza mikutano yao. Hili pia litawafanya kuwa na hoja endapo ukafanyika uchaguzi wa kwanza huru na wa haki hapa Tanzania ambapo kutokana na kujenga imani upya kwa Watanzania wanaweza wakapata kura nyingi za halali ambazo zitahalalisha Uongozi wao nchini Tanzania na ukanda huu wa Afrika.


4. CCM wakikubali mchakato wa Katiba Mpya kufanyika sasa, watajenga Chama cha Siasa kweli cha watu wanaotumia akili haswa katika kutafuta ufumbuzi wa Matatizo ya Watanzania sio kama sasaivi ambapo hadi wao wanafahamu kupata nafasi kwenye chama chao ni lazima ujipendekeze au uwekwe kutokana na kujuana na kupendwa na kiongozi fulani au utumie rushwa.

Hitimisho:
Kwa nguvu wanazotumia CCM kupinga ajenda ya No Reform No Election, ikiwemo kutengeneza propaganda chafu dhidi ya Chadema, kutumia hela nyingi kuhonga watu ili walete chockochoko Chadema ni ushahidi kuwa Chama hiki kinaendeshwa na wajinga tena kimejikita kwenye ujinga. Ni bahati mbaya sana Watanzania wanazidi kuamka kila siku na kuelewa ujinga unaofanywa na CCM.

Ni heri wakakubali tuitengeneze upya nchi yetu sasa kwa kuipatia Katiba Bora na Sheria Bora za Uchaguzi kuliko siku wakitokea Wanajeshi na Usalama wa Taifa wenye akili wasiopenda ujinga ambao watawafurusha Ikulu na kuwaweka kwenye Magereza.
Mambo ya 2015 nani anayataka ndani ya CCM???
Upinzani ulikuwa Strong kuliko unavoweza kudhania
 
Comrade, wewe sema tu umeishiwa hoja au umepigwa spana za kutosha. Ila siyo kuwasingizia watoto wa watu ambao ni nadra sana kuwakuta wanachangia mada za aina hii.

Wenyewe mada zao huwa zinajulikana siku zote.
Nimecheka kijinga ,zile za kula tunda kimasiara
 
Tutake radhi! Ushawahi ona wapi mtoto wa 2000 anaweka hoja nzito hapa jukwaani? Tena jukwaa la siasa?
😀 Watoto wa 2000 wenyewe wako zao busy na tiktok huko, pamoja na zile mada za kula tunda kimasihara! Huwa hawapendi kujitesa, au kuumiza vichwa vyao kwa kufikiri sana. Na huwezi kuwakuta wanajadili mambo serious yahusuyo siasa, uchumi, au mustakabari wa Taifa lao.
 
😀 Watoto wa 2000 wenyewe wako zao busy na tiktok huko, pamoja na zile mada za kula tunda kimasihara! Huwa hawapendi kujitesa, au kuumiza vichwa vyao kwa kufikiri sana. Na huwezi kuwakuta wanajadili mambo serious yahusuyo siasa, uchumi, au mustakabari wa Taifa lao.
Upuuzi mtupu yaaani
 
Kimsingi CHADEMA wana hoja tena zenye mashiko, changamoto iko kwa wananchi. Je, hiyo Oktoba wataunga mkono hiyo kampeni? Suala la CHADEMA kujaza raia kwenye mikutano yao na suala la kuunga mkono ni mambo mawili tofauti kabisa.

Mamlaka yanapaswa kuwa chini ya wananchi sio kwenye kikundi cha watu kadhaa. Mwl. John Heche ameelezea kwa ufasaha na kueleweka.
Wananchi wapo tayari shida ni wajinga waliojazana kwenye vyombo vya dola. Wenye akili wakishika hatamu kwenye vyombo vya dola hasa TISS, JWTZ na polisi mbona hili linawezekana asubuhi kabisa.
 
Back
Top Bottom