Ni kwel aisee
Ngoja nitoe kastory kidogo namna ndugu yetu mmoja alivyokutana na shetani live
Alikuwa na biashara zake nzuri tu kwa siku hakosi faida ya laki 2 mpaka 3
Akaoa,baadae akawa na pepo la ngono mkewe alipojua akaanza kumkomoa jamaa kwanza nae alianza kugawa kipochi manyoya mpaka vitu vya ndani kama chakula na wakati huo jamaa yupo na familia kubwa tu, maana aliwah kuwa na watoto wengi kabla ya kuoa
Jamaa akajikuta ana matumiz makubwa sana,kuna wakati mke akawa anamuibia pesa za kazi na faida zake,mara unyumba ananyimwa
Katika harakat zao za kuchepuka hatimae wakaunasa, mwanamke akaanza vuguvugu la kuvunja ndoa na akafanikiwa sjui alifanyaje yaan ile kesi ilienda haraka sana maamuz yakatoka yakuachana na wamkagawana mali mbali mbali zikiwemo na nyumba
Hyo kesi ilipoisha mwanamke kaanzisha kesi nyingine yakutaka mahitaj ya watoto watatu kila mwezi na wakati huu hali ya jamaa yetu kiuchumi ni ngumu haswa