Ukitaka kumuona shetani 'live' funga ndoa

Ushajiuliza kwanini wanaume waliowatoa bikira wanawake wengi huingia mitini?

Na kuwaacha wanawake wakiwa na maumivu, alafu baadae wao wanataka kuoa bikira Tena.
 
Changamoto za kwenye ndoa ni nyingi sana...za kiuchepukaji zipo lkn kuna nyingine mpaka unatamani uzaliwe.... Mtu ulikuwa kiuchumi fresh tu gafla kila kitu kinapuputika huna pa kushika ... Sijui kama unalewa lkn... Usikae kwenye angle moja
Kwani hakuna watu waliobaki 0 wakiwa hawajaoa/hawajaolewa?

Nini kinafanya uone umefilisika sababu umeoa/umeolewa?
 
Huwa mara nyingi wale wanaodhaniwa wenye Tabia mbovu akiolewa au akioa hujirudi haraka sana na kuwa mtulivu esp. wakijaliwa watoto.
 
Shetani wa ndoa ame-graduate..

Ukiwa single Bado ni rafiki yake Shetani ila ukioa ni rafiki wa Mungu..

Sasa sikiliza ule mtanange wa Shetani akiwa anataka ubaki kuwa wake...

Lazima ukione Cha mtemakuni
Kwa hio shetani wa kabla ya ndoa ni tofauti na shetani wa baada ya ndoa au sababu mnakutanisha mashetani wawili pamoja yanaanzisha varangati?
 
Huwa mara nyingi wale wanaodhaniwa wenye Tabia mbovu akiolewa au akioa hujirudi haraka sana na kuwa mtulivu esp. wakijaliwa watoto.
Jichanganye sasa! Kuna kitu kinaitwa red flags ignore hizo halafu urudi kutuambia hapa kataa ndoa.

Labda kwa kukusaidia wahenga walisema tabia ni kama ngozi ni ngumu kubadili, yamkini wahenga hawakujua scientifically walichokisema kinatokana na nini ila experience ndio imewafanya walete huo msemo which is true.

Scientifically, kuanzia mwaka wa 6-12 wa binadamu ndipo anapodevelop tabia na namna ya kudeal na mazingira yake, ubongo wake ndivyo unavyomuelekeza namna ya kudeal na mambo, sasa usifikiri ukubwani mtu anaweza kuadapt namna mpya ya kudeal na mambo, unless apewe msaada wa kuipanga tabia yake upya, kitu ambacho kinahitaji commitment zisizokuwa za kawaida kukifanikisha.

Sasa kama unajipa moyo mtu mzima anaweza badili tabia kirahisi fikiri tena.
 
Kwa hio shetani wa kabla ya ndoa ni tofauti na shetani wa baada ya ndoa au sababu mnakutanisha mashetani wawili pamoja yanaanzisha varangati?
La hasha. Haiko hivyo. Ndoa ni moja lakini inahusisha watu wawili na kila mmoja wenu kaja na Shetani wake. Kwa mantiki hiyo, Ndoa yenu moja inakabiliwa na Shetani wawili au zaidi na lengo ni Kuisambaratisha kabisa hiyo ndoa yenu itokomee mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…