Ukitaka kumuona shetani 'live' funga ndoa

[emoji122][emoji122]
 
Wengi wanaokotana ambao Mungu akuwakusudia mtakosaje kuingiliwa na shetani! Ukitaka kuoa mtafute Mungu vinginevyo unaoa/olewa na uzao wa shetani. Wengi wanaenda kwa wachawi (waganga) kutafuta wenza huwe na uhakika utapewa majanga na mateso!
 
Nakubaliana na wewe lakini pia ujue mazingira yana uwezo mkubwa wa kumlazimisha mtu abadili Tabia yake atake asitake. Kwa mfano mtu mwenye watoto ni lazima awalee wakue, awasomeshe, awapeleke Hospitali wanapougua n.k. Asipofanya hayo kwa hiari; Serikali itamwajibisha, Ndugu na Jamaa watamsuta na kumchachafya vibaya n.k. Akitoroka(Kama wanavyofanya wengine) huko aendako ni ugenini lazima awe na adabu na mpole vinginevyo anaweza kudhuriwa maisha yake n.k.
 
Nawewe hebu achana na sisi,tulioingia ndoani,tunajuaga raha yake,wewe unaeogopa shetani,utaendeleaga hivyo hadi utakapo kuwaga shetani mwenyewe tuache tuendele kujipatia raha.
 
Wengi wanaokotana ambao Mungu akuwakusudia mtakosaje kuingiliwa na shetani! Ukitaka kuoa mtafute Mungu vinginevyo unaoa/olewa na uzao wa shetani. Wengi wanaenda kwa wachawi (waganga) kutafuta wenza huwe na uhakika utapewa majanga na mateso!
Hapa Sasa ndio patamuje...

Yaani mtu ni mzinzi, mshirikina alafu anataka aoe/kuolewa na Mtakatifu [emoji1787]

Hapa akioa au kuolewa anaolewa na shetani mwenyewe live[emoji1787]
 
Ukikua utaelewa...au kama unataka tulia darasani ueleweshwe....
Nikikua au nikizeeka?

Kwamba humu ndani wote kabla hamjaoa/mjaolewa mlikuwa mnaishi kwa raha mstarehe hamna matatizo, hamna changamoto na mambo yenu yamenyooka kama rula sio? I hope this is a joke.

Binafsi maisha yangu yamekuwa ya mapambano kiasi toka nazaliwa hadi leo kwenye ndoa hakuna utofauti.
 
Hata mtoa mada sidhani kama alimaanisha ndoa zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…