Ukitaka kumuona shetani 'live' funga ndoa

Ukitaka kumuona shetani 'live' funga ndoa

Hapa katafutwa mbuzi wa kafara kabatizwa Jina la SHETANI. Kiasili binadamu hajaumbwa amchukue binadamu mmoja duniani kote aishi nae kwa kigezo cha eti kuanzisha familia. Ndo maana hakuna kitu kigumu kama kulala kitanda kimoja na mtu ambaye mmekutana ukubwani kwa muda usiojulikana. Hata mama yako au kaka yako au dada yako mliyeshea ziwa la mama mmoja huwezi kuvumilia kulala naye chumba kimoja milele mpaka kifo kiwatenganishe. Vitabu vya dini vinatuongopea, ndo maana kipindi kitamu na kizuri cha mahusiano ni mkiwa kwenye uchumba, sababu Kila mtu anakaa kwake, mnakutana kwa ishu maalum au outing, saa nyingine weekend nzima pamoja jumatatu Kila mtu kwake. Na kipindi chote hicho kuna vitu huwezi kuvijua hata ufanyeje kwasababu kila mtu anaamkia kwake. Shida huwa inaanza baada ya honeymoon ndo kila mtu anajiachia, hapo mnamuingiza SHETANI kuhusika kumbe ndo mmeanza kujuana vizuri. Ndoa zote zilizodumu ukiacha za kuvumilia tabia za wazee wetu, ni zile ambazo wapenzi wameishi pamoja hata miaka 10 pengine hata na kupata watoto, halafu wanafunga ndoa baadae. Sababu hakuna aliyeigiza kabla ya kufunga ndoa. Hizi nyingine za mtu anaigiza Ili mfunge ndoa, baadae lazima mapichamapicha yaanze mkimbilie kusingizia SHETANI. SHETANI ni kichaka cha kutokukubali ukweli. Na jamii nzima imekubaliana na huo unafiki. Ndoa lazima litaendelea kuwa kaa la moto mpaka siku binadamu akiacha UNAFIKI.
Umeongea ukweli mtupu
 
Mimi ninavo muona wakwangu nikiishiwa pesa hamna hata aja ya kurudi nyumbani na potea mazima, kwasbb naona shetani wake anapendelea sana uchumi mzuri, siku ukipungua kdgo naona shetani anakuja kwa kasi......... loh. Kulea mtu ulio muona ukubwani ni zaidi ya mtihani.
Afu ke walivyo wajinga,apo anadhan Hujui kwamba she's there for money
 
Leo Mama Mchungaji umekuja kivingine kabisa. Hata sielewi ni ujumbe gani unataka kutuambia sisi watenda dhambi ambao hatujaokoka. Tusiingie kwenye ndoa ama? [emoji15]
Hayo ni mawazo yako,

Nawaandaa mjue kuwa adui shetani yupo na ndoa ndio mahali anapopapenda...

Na mambo mengi yatokeayo kwa ndoa yeye ndo huyaleta...

Ili watu waogope ndoa...

Kabla hujaingia kwenye ndoa uwe umekomaa kiimani yaani unaomba haswa.

Bila hivyo utayumbishwa sana na unaweza ivunja ndoa yako...
 
Aiseee kwa hiyo mmekuja kwenye conclusion kuwa vijana wa kataa ndoa mliokuwa mnawaona vijana wa hovyo kumbe ni magenius kabisaaaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Kataeni ndoa na zinaa msiifanye ..

Hata Biblia haijalazimisha mtu kuoa Wala kuolewa ila zinaa ndio hufanya watu waoe au kuolewa, kama utaweza kuwa toashi..
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Kama kuna sehemu ambapo shetani anapenda kukaa basi ni ndoa. Yaani anakusubiria tu uingie kwenye ndoa takatifu aanze kukutesa. Kama sio ugomvi na huyo mkeo au mumeo unayeona ni halali basi ni ngumi. Sasa Yale ambayo ulikuwa hujui kuhusu mkeo na mumeo unayajua.

Hamna rangi ambayo utaacha ona, anaweza shika tumbo na msipate mtoto. Akiona haitoshi anashika na uchumi ili mkome mkomae kabisa. Mbona Bado, akikuachia huku anakimbilia kwenye tendo husika anaweka mazoea, apo unamuona mkeo kama dada yako.

Ukute Sasa amekalia zinaa ni mwanaume na mwanamke wanachepuka. Achana na huo uchumba sugu ambao unajifanya unamchunguza mwanamke na mwanaume ili umjue. Huwezi mjua mkeo wala mmeo.Ingia kwenye ndoa umuone shetani live.

Donatila
Kujambiana mnajambiana wenyewe kwenye ndoa, halafu mkiipata harufu ya ushuzi,mnamlaumu Shetani ambaye hata hayupo kuwa ndiye kajamba!

Vibaya hivyoo.
 
Mnamuonea sana Shetani.

MATENDO YENU WENYEWE MNASINGIZIA SHETANI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Shetani ni chaka la kufichia habari zote za kukosa uwajibikaji kwa watu binafsi.

Yani mtu atafanya ushenzi wowote, ukimuuliza anajitetea kwamba "Shetani alinipitia".

Ndiyo msingi wa thread hii.

Watu wameshindwana wenyewe kwenye ndoa, kwa sababu zao, badala ya kujihoji wamefeli wapi wao wenyewe wajirekebishe, wanamtupia lawama Shetani.

Tutajifunza na kujikosoa kweli kwa style hii ya kufikiri?
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Kama kuna sehemu ambapo shetani anapenda kukaa basi ni ndoa. Yaani anakusubiria tu uingie kwenye ndoa takatifu aanze kukutesa. Kama sio ugomvi na huyo mkeo au mumeo unayeona ni halali basi ni ngumi. Sasa Yale ambayo ulikuwa hujui kuhusu mkeo na mumeo unayajua.

Hamna rangi ambayo utaacha ona, anaweza shika tumbo na msipate mtoto. Akiona haitoshi anashika na uchumi ili mkome mkomae kabisa. Mbona Bado, akikuachia huku anakimbilia kwenye tendo husika anaweka mazoea, apo unamuona mkeo kama dada yako.

Ukute Sasa amekalia zinaa ni mwanaume na mwanamke wanachepuka. Achana na huo uchumba sugu ambao unajifanya unamchunguza mwanamke na mwanaume ili umjue. Huwezi mjua mkeo wala mmeo.Ingia kwenye ndoa umuone shetani live.

Donatila
Inachekssha lakini ni ukweli mtupu
 
Mkuu unatushauri nini vijana tunaotaka kuingia huko? Maana sina muda nataka nifanye yangu
Mtangulize Mungu katika kila hatua,ili uweze kumpata mke mwema,NA katika kila hatua ya maisha yako mshirikishe Mungu,bila kusahau kuishi maisha yenye kumpendeza yeye maana kinyume cha hapo shetani hatakuacha salama...
 
Ingia kwenye ndoa umuone shetani live.
Kabla sijaoa nishaonana na shetani live mara kadhaa kwa hio nilishapiga Tizi la kutosha ndani huko kwenye ndoa Mimi na shetani tutakua tushazoea yaan ni washkaji kabisa tunapiga story vipi wewe bado hujakutana nae live? Namaanisha Mimi na shetani ni washkaji asipopokea simu siku nzima simuulizi yaweza kua muda huo alikua anapiga story na shetani au shetani anamgonga Mimi hainihusu shetani nishamzoea na tabia zake za kishetani Ila tu nisimfume red handed akiwa na mke wangu nitamrudisha motoni

Unasubiri mpaka uingie kwenye ndoa ndio ukutane na shetani? Wenzio kila siku tunapishana nae na tunaishi nae
 
Back
Top Bottom