..mkuu mtoa mada umeongea ukweli ulio-wazi. Vijana wa Tz tunaangamia sana hasa kiuchumi kwa kuharibu akili aliyotupa Mungu..hatupo makini kwenye vitu basic vya maisha sbbu akili zimeharibika kwa mizaha, ngono, etc..na hili lipo wazi maana hata Biblia imesema hana akili aziniye na mwanamke; usiketi barazani pa wenye mizaha (Zab 26;5), mazungumzo mabaya huharibu tabia njema (1 Corinth 15:33)!
..kurelax ni muhimu sana na social chatting is healthy but vijana wa tz muda mwingi tunaishia kwenye mambo yasiyo na maana kabisa na kuharibu akili zetu. Pia watu wanachanganya kuwa makini ni kujadili mambo ya siasa..this is big NO..hakuna mambo yanayogusa vijana kama uchumi..tuna resources nyingi sana mataifa ya nje yanakuja yanafanikiwa..wahindi&waarabu hawafatilii siasa wao wanakomaa kupeana info na kujadiliana fursa za kiuchumi wanafanikiwa sana. Vijana wa mataifa mengine fikra zao zipo vizuri sana na sisi tunaweza tukibadilika. Social iwepo ila nguvu kubwa tuweke kwenye uchumi na info za fursa.