Kumekuwa na maneno, machapisho mitandaoni kwamba, ruti ya mabasi ya Shabiby Line kutoka Dodoma kwenda Tanga kupitia Chalinze imekufa. Siyo kweli hata kidogo.
Ruti hiyo bado ipo palepale na ipo vilevile. Dodoma- Tanga na Tanga- Dodoma kupitia Chalinze kama vibao vya utambulisho mbele ya mabasi vinavyosomeka.
Nje ya Ofisi za Mabasi ya Shabiby Line, Dodoma abiria wamekiri kuwepo kwa ruti ya Dodoma kwenda Tanga kupitia Chalinze wakisema ni wazo bora kwa wasafiri wa maeneo hayo.
Abiria aliyejitambulisha kwa jina la Zuchu ambaye alisafiri kutoka Dodoma kwenda Tanga, alisema kuna nyakati wasafiri wa Dodoma kwenda Tanga walikuwa wanasumbuka kwa kupanda mabasi ya kuungaunga. Lakini baada ya Shabiby kuanza ruti hiyo kwa sasa wana -relax.
"Zamani ilikuwa lazima uunge safari. Utoke hapa (Dodoma) na mabasi yanayokwenda Dar ukashukie Chalinze. Halafu usubiri mabasi ya Dodoma- Tanga. Na unaweza usipate nafasi. Kwangu ilikuwa kazi ngumu sana. Lakini sasa nainjoi kwa kweli," alisema Zuchu.
Ni dhahiri kwa sasa, mabasi ya Shabiby Line yamekuwa yakianzisha ruti kwenye barabara ambazo zina uhaba wa mabasi
Njia hizo ni kama kutoka mkoani Dar es Salaam kwenda mjini Babati, mkoani Manyara, kutoka jijini Dodoma kwenda jijini Arusha. Kutoka jijini Dodoma kwenda jijini Mbeya.
Ukiachia mbali ruti ya Dar es Salaam kwenda Dodoma ambayo Shabiby Line limesimika utawala kwa miaka mingi sasa.
Mabasi yote yanayokwenda Tanga kutoka Dodoma ni Yutong D 14 yenye ubora wa hali ya juu huku abiria wakikaa kwenye viti vyenye starehe na rafiki kwa watu wenye matatizo ya kupata ganzi kwa sababu ya kukaa kwa mtindo mmoja kwa muda mrefu.
Ofisi za Shabiby Line Dodoma zipo mjini kabisa na Tanga zipo Barabara ya 13 jirani na Ofisi za Mabasi ya Mbeya City.
Ni dakika tatu tu kwa mwendo wa miguu kutokea stendi kuu ya zamani ya mabasi iliyopo maeneo ya Ngamiani, Badabara 11 na 12 jijini humo.
Nauli kutoka Dodoma hadi Tanga ni Shlingi 48,000 (bei mpya baada ya mafuta kupanda). Basi huondoka Dodoma kwenda Tanga saa 1 jioni na Tanga kwenda Dodoma vivyo hivyo.