Ukitaka kuwa tajiri, usiende shuleni

Ukitaka kuwa tajiri, usiende shuleni

Joined
Feb 8, 2012
Posts
29
Reaction score
24
Mpenzi msomaji je ushawahi kukaa chini na kujiuliza ni ma Professor wangapi ma billionaire duniani? Au waalimu, ambao ndo wataalamu wa kufikiri inavyosadikika?

Hawa ndo chanzo cha umaskini..sina maana kwamba nawachukia au nawadharau la hasha ila ni kutokana na mifumo mibovu ya elimu iliyopo nao ndo wanaihubiri au kuisimamia.

Kivipi?
Mara nyingi tumesikia haya maneno. MWANANGU/MWANAFUNZI SOMA SANA PATA MAKSI ZA JUU ILI UJE KUPATA KAZI NZURI YENYE MSHAHARA MKUBWA.

Huu ni ujinga kwa sababu mtu akiajiriwa una kuwa na usalama wa kazi tuu lakini unakuwa hauna uhuru wa kiuchumi{financial freedom}.

Unapoajiriwa na kampuni unafanyia kazi watu wengi ambao mnagawana nao mshahara pasu kama hivi mshahara wako unakatwa haya kabla hujapokea;

- Kodi ya serikali
- Makato ya bima
- Makato ya benki
- Makato ya vyama vya wafanyakazi

Halafu ndo unapokea hela yako. Ndio maana tumesikia wafanyakazi wengi wakilia sana juu ya makato kuwa ni makubwa sana..

Baada ya hapo unakwenda nyumbani na hiyo hela ambapo zinakwenda katika vibobo vya kukutia umaskini ili urudi tena kazini ambavyo ni kodi ya nyumba, maji, umeme na ada za watoto na kama muflisi gari unanunua mafuta na kulipia kodi zake.

Huenda hujanipata vizuri sasa utanipata nachomaanisha.

Ni kuwa huyu mwajiriwa hana vitega uchumi miradi ambayo ingemuingizia pesa za kutosha maisha yake yote ndo maana baadhi ya waajiriwa wanapostaafu hufa ghafla kwa sababu ya ukata.

Embu tumuangalie mwekezaji. Wawekezaji wengi Mabilionea hawana degree, mfano;

- Bakhressa wa Azam
- Patrick Ngowi. Tajiri namba moja Tanzania
- Bill Gate wa Microsoft
- John D. Rockefela wa Standard Oil of America
- Mark wa Facebook
- Na wengine wengi, unaweza ni PM..

Ma investor wote unajua wanakatajwe kodi? Ni baada ya kutoa garama zote za uendeshaji na ile faida iliopatikana ndo inakatwa kodi.

Mpenzi msomaji, bwana HENRY FORD aliwahi kusema. "Thinking is the hardest work there is, that is why so few people engage in it".

Wapendwa wasomaji nimepata PM nyingi sana wakitaka vitabu vya Robert kiyosaki na nimewapatia in terms of softcopy na audio. Kama na wewe unataka, nijulishe nitakutumia kwa e-mail au basi au njia yoyote ile.

Nicheki weyosi@yahoo.com
 
The more educated you are,the higher the risk averse you will be. The less educated the more risk lover you will be. And as the principle goes,the higher the risk the higher the return. Wasio na elimu wanaweza kuwekeza kwenye biashara yeyote bila woja na kujiuliza mara mia mia. Hawaogopi matokeo. Na wengi huwa wanafanikiwa sababu sehemu wanazowekeza wengi huwa wamezikimbia.
 
Lakini kumbuka hawa matajir wanawaajiri wasomi ndio wanamuendeshea biashara yake halafu kila m2 na trend yake ya maisha so be carefully halaf unapofikiria geuz mawazo pia upande wa pili.
 
Lakini kumbuka hawa matajir wanawaajiri wasomi ndio wanamuendeshea biashara yake halafu kila m2 na trend yake ya maisha so be carefully halaf unapofikiria geuz mawazo pia upande wa pili.

YAP.umenipata vizuri kumbe unajua wasomi ndo wanamuendeshea biashara mkuu ni sawa kabisa. ndo nina makala moja inasema.JE UNAJUA KWA NINI WALIOFAULU WANA AJIRIWA NA WALIOFELI?.
WALIO GRADUATE NA ''A au GPA YA FIRST CLASS HUWA WANAAJIRIWA NA WENYE C NA D NA WENYE SECOND CLASS HUAJIRIWA NA SERIKALI.
 
Mimi nafikiri wewe mwenyewe ndiyo unajichanganya! Kusema hakuna Professor Billionea ni makosa maana hakuna mtu alaiyesema unavyozidi kusoma ndiyo unazidi kuwa tajiri bali wahenga wanasema ukisoma unauhakika zaidi wa kuwa na maisha mazuri. Hivyo badala yake hapo juu ungetutajia mfano wa Maprofessor ambao ni masikini ili utushawishi tusisome na sisi.

Kuna Professor masikini unamjua hata mmoja?
 
That is true man, haina haja ya kubisha tangu ln mshahara ukakutosha?
 
mimi nafikiri wewe mwenyewe ndiyo unajichanganya! Kusema hakuna professor billionea ni makosa maana hakuna mtu alaiyesema unavyozidi kusoma ndiyo unazidi kuwa tajiri bali wahenga wanasema ukisoma unauhakika zaidi wa kuwa na maisha mazuri. Hivyo badala yake hapo juu ungetutajia mfano wa maprofessor ambao ni masikini ili utushawishi tusisome na sisi.

Kuna professor masikini unamjua hata mmoja?

hili ni suala mtambuka.labda niseme hivi navyosema masikini simaanishi kuwa ni hana kitu kabisa tena wanalipwa zaidi ya 4miiion.lakini wana financial security tuu .lakini hawana fi
ancial freedom.mkuu ipo tofauti kubwa sana kati ya financial security na financial freedom.
Kwa ufupi sana
financial security -you work for money
financial freedom-let money work for you
 
hili ni suala mtambuka.labda niseme hivi navyosema masikini simaanishi kuwa ni hana kitu kabisa tena wanalipwa zaidi ya 4miiion.lakini wana financial security tuu .lakini hawana fi
ancial freedom.mkuu ipo tofauti kubwa sana kati ya financial security na financial freedom.
Kwa ufupi sana
financial security -you work for money
financial freedom-let money work for you


But your title is too General, Yaani umesha-conclude kuwa ukienda shule basi huwezi kuwa Tajiri. Na kwanza nani kakudanganya kuwa kila Professor hana financial freedom? Au unaongelea Maprofessor wa nchi gani mkuu labda siyo hawa wa Tanzania ambao muda wote wapo kwenye shughuli binafsi, wakiingia darasani wanagawa Hand-out tu na hata kusahihisha wanasaidiwa na wanafunzi wao wa Phd.
 
Nice nakupa like. Tatizo la watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri na hata kufanya kaz. Pia ni waoga sana wa ku take risk. Ndio maana wanaishia kuajiriwa na mwisho kuwa watu wa kipato cha kati kama sio cha chini(wengi wao)
 
Hivi umeshawahi kukaa chini na kujiuliza ni watanzania wangapi ni masikini wa kutupwa sababu tu hawakusoma? anzia na kijijini kwako. sidhani kama ukipewa muda wa kuwaorodhesha utaweza kufanya hivyo kama ulivyofanya kwa hao matajiri. Jaribu tena kujiuliza ni watanzania wangapi waliopata elimu japo ya diploma wana uwezo wa kumudu maisha yao ya kila siku? kwa hili nalo hutaweza kuorodhesha majina. hao matajiri ni asilimia ndogo sana ya watanzania wote haifiki hata 0.00001% ambayo kimahesabu tunasema ni negligible. idadi ya watanzania masikini kwa sababu tu hawakusoma ni zaidi ya 80% sasa hapo unapo conclude watu wasisome kwa akili zako unaona unaongeza idadi ya masikini au matajiri?
 
hili ni suala mtambuka.labda niseme hivi navyosema masikini simaanishi kuwa ni hana kitu kabisa tena wanalipwa zaidi ya 4miiion.lakini wana financial security tuu .lakini hawana fi
ancial freedom.mkuu ipo tofauti kubwa sana kati ya financial security na financial freedom.
Kwa ufupi sana
financial security -you work for money
financial freedom-let money work for you

robert kiyosaki amewaharibu sana watu...hiki kitabu cha rich dady poor dady kinawadanganya sana
 
nakubaliana na wewe kabisa,mimi nina ushuhuda ulio hai,baada ya kumaliza shule ya msingi kuna wenzangu wengi hawakubahatika kuendelea na sekondari wakaamua kutafuta fedha,tulipomaliza kidato cha nne wenzetu wakawa tayari na mitaji inayoweza kuwasafirisha miji mbalimbali kwa biashara,wakati tunamaliza chuo na kukosa ajira wenzetu walikuwa tiyari wana miliki majumba sehemu tofauti hapa tz sisi tuliona haya ya kufanya bishara ambazo ndio ziliwanyanyua wenzetu,......leo hii tuliosoma nao primary wanamiliki viwanda na maghorofa kariakoo,wa sekondari wanafanya shughuli za kipato cha chini,wa chuo wameathirika kwa kutaka vitu vya kufikirika.......wengi huchagua kazi na kudai hakuna, ajira which is not true.
 
Me ninachojua tajiri hata akiwa na hela namna gani kama hana shule hiyo hela itamtesa sana na hatoifurahia kabisa. Tofauti na mtu mwenye hela msomi hela haitamtawala bali yeye ataitawala hela na kufurahia maisha.

Ninachoshauri ni kuwa watu wakitoka vyuoni waache kudharau kazi. Kazi yoyote halali yenye kipato kizuri ingia mzigoni piga kazi.
 
Nadhani anachomaanisha ni kwamba kwa waajiriwa wengi kipato wanachopata kama mshahara hakiendani na kazi wanayofanya pamoja na kiasi cha pesa wanachoiingizia serikali au ofisi
 
Nakubaliana na wewe halo maelezo yako ni mafupi na wengi ambao hawatakuelewa watakupinga,kama wanavofanya wasiomwelewa Robert Kiyosaki ambaye bila shaka ndiye mwalimu wako.

Tofauti na wengi wanavyoamini, Robert Kiyosaki hasemi kwamba tusipeleke watoto shule, lakini anahamasisha mabadiliko katika mfumo wa elimu, maana tunakwenda shule ili tuje kuwa waajiriwa badala ya kujiajiri na kuajiri wengine.

Tupeleke watoto shule lakini pia nyumbani tuwafundishe kitu ambacho shuleni hawajifunzi, "financial education", mtu anaweza kuajiriwa na bado akawa financially free, ni suala la wewe unafikiri nini kuhusu pesa, Kuna rules za pesa, za zamani na za sasa, wewe unafuata rules zipi?
 
Back
Top Bottom