Ukitaka kwenda mbali, nenda na wenzako - Mahusiano ya kidiplomasia

Ukitaka kwenda mbali, nenda na wenzako - Mahusiano ya kidiplomasia

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
UKITAKA KWENDA MBALI, NENDA NA WENZAKO - MAHUSIANO YA DIPLOMASIA

Matokeo Chanya ya Ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yashusha neema kwa Watanzania leo tunashuhudia Ujumbe wa Wawekezaji zaidi ya 120 kutoka Nchini Misri hii imetokana na Ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan mwezi Novemba, 2021 Nchini Misri.

Katika Ziara hiyo Mhe. Rais Samia alikutana nao na kufanya mazungumzo na kuwakaribisha kuja kuwekeza Nchini Tanzania.

Namna Pekee ya kupiga hatua ni kutumia DIPLOMASIA vema katika uhusiano na Taasisi na Nchi nyingine

Tangu aingie madarakani tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameshafanya mikutano kwa njia ya mtandao na karibu viongozi wote wa taasisi za kimataifa kwenye maeneo ya Uchumi, uhusiano wa kimataifa na Fedha.

#MamaYukoKazini
#KaziIendelee

Screenshot_20211205-094848.jpg


Screenshot_20211205-094602.jpg


Screenshot_20211205-094527.jpg


Screenshot_20211205-094514.jpg
 
Changamoto ni ile ile umasikini, na mateso kwa wanachi chanzo ni chama cha kijani
 
Hao wawekezaji, wengi wao, wengi sana, asilimia kubwa, ni wamendeaji, wafyonzaji, wavunaji, wanyonyaji, wahonyoaji, wakwapuaji tu wa rasilimali tele za Afrika. ^Ndugu zangu, hakuna mjomba atayetoka huko Ulaya kuja kutujengea nchi yetu,^ ilisikika sauti ya mzalendo mmoja.
 
Misaada tumekuwa tunaipata kwa miaka 60 sasa (yaani mtoto amezaliwa, amekuwa, ameanza primary, secondary, chuo, ameajiriwa hadi amestaafu) bado tumekuwa watu wa kutembeza bakuli halafu tunajisifia!
 
Misaada tumekuwa tunaipata kwa miaka 60 sasa (yaani mtoto amezaliwa, amekuwa, ameanza primary, secondary, chuo, ameajiriwa hadi amestaafu) bado tumekuwa watu wa kutembeza bakuli halafu tunajisifia!
Mbona kuna watanzania wame wekeza kenya? Labda ungetupa maana ya uwekezaji kwa mtazamo wako
 
^Ndugu zangu, hakuna mjomba atayetoka huko Ulaya kuja kutujengea nchi yetu,^ ilisikika sauti ya mzalendo mmoja

Noted
 
Kwa kweli ni jambo zuri lakin bila misingi ya kusimamia huo uwekezaji utasema afadhali wasingekuja maana watachuma vyao na kuondoka navyo sisi tutabaki kujisifia tu tuna wawekezaji
 
Back
Top Bottom