Ukitaka umtese mbongo, mwonyeshe matokeo ila usimuonyeshe vyanzo vyako vya mapato

Ukitaka umtese mbongo, mwonyeshe matokeo ila usimuonyeshe vyanzo vyako vya mapato

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Wakuu mtaani ukitaka ulete taaruki, ficha vyanzo vyako vya mapato ila onyesha tu matumizi ya kipato chako.

Hapo utagundua mtaani au ukoo wote ni wapelelezi wa kujitolea. Wakipeleleza wakashindwa...

Utaitwa
~ Freemason
~TISS
~Tapeli
~Mchawi
~Jambazi
~Muuza madawa ya kulevya
~Akiugua au akifa mtu tu, utasingiziwa ndio source yako ya income
~Fisadi

FAIDA: Hii itakupunguzia kusongwa na mafuriko ya watu ili upate muda wa kutengeneza financial base yako vizuri.

MAMBO MATATU HAYA UKIYAWEKA PRIVATE YATAKUSAIDIA KUFANIKIWA KWA WEPESI.

1: Maisha yako yakifedha na vyanzo vyako. (YOUR FINANCIAL LIFE)

2: Maisha yako ya mahusiano/Mapenzi.

3: Your Next step ( Hatua unayotaka kuchukua).

Usiwaambie watu unayaka kufanya nini. Maneno ni uchawi, huwa yanatabia yakublock. Waonyeshe ulichokifanya.


Ni hayo tu, wakuu.
 
Hapo kati kuna biashara ya pembe za ndovu huwezi kuambiwa ukweli, utaambiwa ongeza ibada au njoo kwa Yesu.
Kuna jamaa miaka ya flani ninapambana namwambia naomba njia maana huwa namuona mnyonge kifedha lakini anashusha mjengo wa maana na kubadilisha magari tu.

Ananiambia ongeza focus na jifunze kusimamia malengo na ongeza sala, ila hafunguki. Hadi nilipogundua kumbe mlokole mjanjamjanja marketer wa kampuni ya bia flani EA.

Ila anazuga ni mtafutaji na mjasiliamali anayesisitiza watu tumtegemee Yesu.
 
Hatuteseki, ni human nature kujilinda kwa kudodosa mambo, jirani yetu aliishi bwana mmoja haeleweki wiki tatu tu watu tunaulizana huyu ametoka wapi anafanya nini, kumbe jambazi kakamatwa na bunduki ndani kwake. Kwa hiyo madodoso yaendelee, ni ulinzi shirikishi tosha kabisa.
Umeandika kitaalam.
Jamaa mwingine walimtungua anafuga joka kubwa sana ndani ndio linampa pesa, kumbe jamaa alikuwa anaongea tu vitu vikubwa ila ni wakawaida tu. Ila alivyojiweka huwezi kujua kama ni mtu wa kawaida tu.

Nimeelewa hapo kwenye ulinzi shirikishi.
 
Hapa Tz ukijionesha Kwamba una Akili Fahamu utajiletea Matatizo u have to act as a kid in thinking

Vaa kawaida Sana au ukivaa vizuri jifanye mlokole au jifanye shekh vaa Hadi baraghashia tofauti na hapo prepare to be witched.
Hahaha
 
Hapa Tz ukijionesha Kwamba una Akili Fahamu utajiletea Matatizo u have to act as a kid in thinking

Vaa kawaida Sana au ukivaa vizuri jifanye mlokole au jifanye shekh vaa Hadi baraghashia tofauti na hapo prepare to be witched.
Wachache watakuelewa, hasa wapenda bling bling ndio hawatokuelewa kabisa.
 
Back
Top Bottom