Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
- Thread starter
- #121
UVCCM sawa babaRais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
UVCCM sawa babaRais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%.
Bin Sawia.UVCCM sawa baba
Hizi picha umezipata wapi?Bin Sawia.View attachment 1579641
Apia...!!!Rais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%.
Utajionea mwenyewe baada ya 28 October 2020.Apia...!!!
Tatizo Chadema wanawatesa vijana kwa kuwaambia uwongo kuwa Lissu atashinda.Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Ndugu zangu watanzania;
Ukimtendea mtu wema leo hii, wema huo unaweza usikulipe wewe bali ukaja ukawalipa watoto wako au wajukuu zako miaka ya baadaye. This is my true story.
Mnamo mwaka 2017 nilibahatika kupata kazi katika taasisi moja ya watu binafsi (jina kapuni) ambayo ofisi zake zipo Dar es Salaam mtaa wa Ohio pale posta karibia na British Council.
Kwa kuwa nilikuwa bado ninakaa Pugu kwa kaka yangu mkubwa ikawa inanilazimu kuwa ninapanda treni kila siku nikiwa ninaenda na kutoka kazini kwa maana huo ndio ulikuwa usafiri wangu wa uhakika ukizingatia wakati ule ujenzi wa daraja la juu la Mfugale ndio ulikuwa umepamba moto hivyo usafiri wa daladala usingekuwa ni chaguo jema ukizingatia usumbufu wa foleni hususan during rush hours.
Muda wa kutoka kazini ulikuwa ni saa 16:00 hrs na treni ya kwanza inatoka stesheni ya posta saa 15:55 hrs hivyo haikuwa rahisi kwa mimi kuweza kuwahi route ya kwanza. Ilikuwa inanibidi niombe ruhusa kutoka kwa boss wangu nitoke kazini saa 15:30 hrs ili niweze kutumia hizi dakika 25 nitoke Ohio street/avenue mpaka stesheni ya posta kwa ajili ya kuwahi treni.
Kwa kuwa nilikuwa nimekwisha msimulia boss wangu kuhusiana na masuala fulani ya kifamilia hapo nyumbani kwa kaka yangu ambayo yalikuwa yananilazimu kurudi nyumbani mapema, boss alinielewa sana kwa maana alikuwa ni baba wa makamo wa miaka kama 57 au 58.
Sasa nikawa kila siku ninatoka ofisini ninawahi treni nikiwa ninatembea kwa mwendo wa kasi wa ajabu na kuna wakati ilikuwa inanibidi nikimbie kwa maana ilikuwa mara nyingi nikifika maeneo ya TRA headquarters au Central Police Station ninasikia ile honi inalia pooooh ikiwa inaashiria kuwa inajiandaa kuondoka ndani ya dakika chache zijazo.
Basi hapo mimi nilikuwa ninachanganyikiwa. Nikifika kwa muuza ticket ninatoa pesa ikiwa cash shillings 600 tayari nimechenchi, ninachukua ticket huyo ninakimbilia ndani ya behewa tayari kwa safari
Niliweza kufanya zoezi hilo kwa muda kama wa wiki mbili ila baadaye nikaanza kuona mabadiliko kwa dada mmoja hivi wa makamo kidogo around 36 to 38 aliyekuwa anauza tickets za treni. Ilikuwa nikifika katika dawati la kununulia ticket au nikimkuta amesimama akiwa na zile mashine za kukatia ticket, huku mimi nikiwa ninahema kwa kasi kwa sababu ya mbio za kuwahi treni, ninampa pesa 600 shillings anakataa kupokea ila anaipa ticket ninaondoka.
Nikimuuliza kwanini anasema hiyo ni ticket ya offer imetolewa na TRC. Nikawa ninajisemea kimoyomoyo hala haula la kwata, tafadhali pesa yangu 600 imepona nitatumia kesho asubuhi nikiwa ninaenda job. Hii offer ikawa kila nikifika ninapewa na mimi tu ingawa pale mezani tunakuwa tupo wasafiri kama 6 au 7 kwa wakati mmoja.
Nikawa ninazichukua zile tickets za offer ingawa machale yakaanza kunicheza nikawa ninajiuliza inakuwaje hii offer ninapewa peke yangu na hao TRL ilhali tunakuwa tupo wengi muda wa kuchukua tickets? What might be the reason behind?
Nilasema isiwe tabu ngoja siku moja nitaacha kupanda treni ya kwanza nitajichelewesha ili nipande route ya pili ili nipate muda wa kupeleleza vizuri hili suala.
Sawa bwana. Ilipofika Ijumaa nikatoka ofisini muda ule ule kisha nikaenda kupiga story kwa fundi viatu mmoja rafiki yangu mpaka ilipofika muda wa kupanda treni route ya pili nikaanza safari mdogo mdogo mpaka nikafika kwenye meza ya yule dada akiwa hana abiria wengi kama kawaida nikatoa pesa yangu 600 shillings yule dada akakataa kisha akanipa ticket akasema ni offer imetoka ofisini.
Nikasema kimoyomoyo huyu leo asinitanie. Unaweza kujikuta unalipiwa kumbe ni mtego bila wewe kujijua. Mjini hapa mzee baba. Nikimuuliza kwa ustaarabu wa hali ya juu sana. Nilimuuliza dada inakuwaje hizi offers za free tickets ni mimi tu ndio ninazipata kila nikifika kwako.
Mbona akiwa anahudumia dada mwingine sipewi hizo offers? Yule dada akasema labda nina nyota nzuri kutokana na kuwa mimi ni handsome man (hahahaaaa. I'm joking) nilimbana yule dada kwa maswali mpaka akaamua kufunguka na kusema ukweli.
Kumbe mama yangu aliwahi kumsaidia yule dada kipindi mama anafundisha Secondary School moja hapa Dar. Mama alikuwa anafundisha Secondary school ambayo na sisi tulikuwa tunasoma hapo hapo mimi na dada yangu. Wakati huyu dada yupo form six, mimi na dada yangu (pacha) tulikuwa form one.
Kwa hiyo wakati mama anaenda kazini tulikuwa tunaongozana naye tukawa tunajulikana hawa ni watoto wa mwalimu fulani. Huyu dada akasema wakati anajiandaa kufanya mitihani ya kidato cha sita ule mtihani wa siku ya kwanza asubuhi alidondosha kitambulisho ndani ya daladala na hakuweza kufahamu mpaka alipofika katika geti la shule na kutakiwa kutoa kitambulisho cha mwanafunzi na kujikuta hana.
Anasema mama yangu hakuwa katika zamu ya usimamizi kama mwalimu mwenyeji wa shule, ila alikwenda shuleni kwa shughuli zake binafsi. Mama akaenda akaongea na mlinzi pamoja na wasimaizi wa mitihani ndio akaruhuiswa kuingia getini, ukizingatia mvua ilikuwa inanyesha na mwalimu wa zamu hakuwepo.
Yule dada alisimulia kwa hisia sana mpaka nikajawa na huruma ila ninamwambia hivyo ndivyo maisha yalivyo. Ukimtendea mtu wema leo hii, wema huo unaweza usikulipe wewe bali ukaja ukawalipa watoto wako au wajukuu zako miaka ya baadaye.
KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.
Na "Akiba haiozi"Wanasema "Wema ni Akiba"[emoji4]
Unajitahidi kutabiri mkuu. Mimi nilimaliza chuo kikuu mwaka 2009, sasa jiulize nina umri gani mpaka sasa?...Kama huyo dada ana miaka 36 hadi 38, basi wewe una miaka 30 hadi 32.
Sawa mkuu...Kwa kuwa dada alivyokuwa form six wewe ulikuwa form one.
Marhabaa mdogo wanguShikamoo.
Hahahaha nimeupenda hii ...ila hiyo ya mema ya nchi duh...Daima kwenye maisha, kama upo katika position ya kumsaidia mtu juu jambo lolote na halina athari kwako fanya hivyo haraka!
Miaka 8 iliyopita nilimsaidia dogo mmoja aliekua na maisha magumu shuleni kwa mahitaji yake kwa kuguswa tu na hali yake nikiwa kama mwalimu wake. Miaka kadhaa mbele dogo akafaikiwa kuajiriwa kwenye chuo flan hapa nchini baada ya ya kufanya vzr Bachelor yake, kipindi chote alinichukulia kama brother na akiendelea kunipa updates za hatua zake kimasomo, nami nikajiendeleza na kufanya masters. Dogo akapata SCHOLARSHIP na kwenda kufanya shahada ya pili nje....nami nlikuja muajiriwa chuo kimoja cha private na kuanza kazi. Siku moja nafungua email, nakuta amenitumia forms za scholarship, akisisitza bro jaribu kuomba hizo kuna jamaa angu amenitumia.....mzee nikajipinda, nikatuma..nimeshtuka may 13 mwaka jana nafungua email yangu, dah alhamndullilah, nimepata full scholarship ya PhD, sasa nakula mema ya nchi. Unapoweza kumsaidia mtu fanya hivyo, it pays a lot! Nimejifunza
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeipenda hii ya madereva wa fuso....Kuna wema wengine ni Malaika wanatumwa na Mungu kukusaidia wakati wa shida. Kuna siku niliharibikiwa na gari katikati ya mbuga ya Mikumi na eneo hilo kulikuwa na nyati kibao. Alitokea dereva mmoja wa kampuni ya utalii alinisaidia sana yaani alifuata mafundi mjini wakaja pale wakantengeneza na yeye alikuwepo anasubiri tu na baadhi ya spares za kufuata Mikumi mjini gari yake ndio ilikuwa inatumika. Baadae gari ilivyotengemaa kama saa sita usiku akaja mzee mmoja anamiliki hotel mwanzo mwanzo wa mbuga akaniambia nikaweke gari hotelini kwake na kulala na wote hao hawakunitoza hata shilingi. Niliwalipa mafundi.
Kuna siku nataka nikawatafute wale jamaa wote maana niliishiwa pozi na sikujua la kufanya pale mbugani.
Mbali ya hao wema kulikuwa na baadhi wa wajinga walikuwa wanatutisha (madereva wa Fuso) wakidai kuna simba wanatuvia wamewaona yaani kama wametumwa
Sawa bossNimeipenda hii ya madereva wa fuso....
Hakika mkuu
Kamanda wako JPM utam-miss sana mkuu?Hakika mkuu