Ukitenguliwa tulia, kila jambo lina wakati wake

Ukitenguliwa tulia, kila jambo lina wakati wake

Jokate kahamishwa sijui mara ngapi hadi namwonea huruma.
Kesho yuko korogwe,mala kisarawe mala sijui wapi,mala kwa wamama mala uvccm.
Sasa nashindwa hata kuelewa anafanya kazi saa ngapi?
Wamwache atulie kidogo basi.
Ukiona hivyo kapwaya, au kashindwa ku deliver sasa anatafutiwa sehemu ajifiche naye ale, maana ni ndugu ya wateule.

Angekuwa sisi akina pangu pakavu, ungemsikia Bongo Movie siku nyiingi.
 
Unapotenguliwa fahamu kuwa ni muda uliotimia wewe kuwa mtumishi.
  • Fikiri mengi lakini zungumza machache,
  • Sikiliza wengi lakini jibu wachache,
  • Andika mengi lakini ya ibada na shukurani,
Kuna Mbu Nge kule Nzega apate ujumbe huu
 
Unapotenguliwa fahamu kuwa ni muda uliotimia wewe kuwa mtumishi.
  • Fikiri mengi lakini zungumza machache,
  • Sikiliza wengi lakini jibu wachache,
  • Andika mengi lakini ya ibada na shukurani,

Kama ulivyokaa kimya wakati wa kuteuliwa, vivyo hivyo kaa kimya wakati kutenguliwa.
Hiyo inaitwa hekima. Kujua wakati gani wa kunyamaza na wa kuongea. Kujua wakati gani wa kuupa muda nafasi mpaka pale hali zitakapokuwa sawa, hasa hali yetu ya kiakili.
Kwenye Behavioural studies tunaambiwa kuwa makini kwenye hali mbili, unapokuwa na furaha sana usifanye maamuzi, kutia ndani kuongea. Pia unapokuwa na huzuni au kukasirika sana usifanye maamuzi kutia ndani kuongea. Katika hali hizo tunaweza kufanya maamuzi ambayo si ya kawaida au ya tafakuri, hivi kwamba baadaye tukiwa katika hali ya kawaida tukaanza kujiuliza kwa nini tulifanya maamuzi haya. Kukasirika au kufurahi kupita kiasi zote ni hisia ambazo ni za kudhibitiwa (emotional intelligence). Kwani tusipofanya hivyo huenda tukafanya maamuzi ambayo baadaye tukajutia. Hiyo pia ikaenda sambamba na kujitambua/kujidhibiti tabia zetu pindi tunapokuwa na ufanisi sana au hali ngumu sana (managing success and hardship).
 
Back
Top Bottom