Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Esoteric knowledge unaijua!?
 
uganga wa jadi umegawanyika ktk vipande viwili 1. Traditional medicine 2. Spiritual healing ila hivi vyote ni lazima uvikute kwa mganga wa jadi, akiwa na na kimoja hasa hasa namba moja anakua kama kina DR MWAKA, pia mganga anaweza ku diagnose tatizo lako kwa namna mbali mbali bila wewe kusema chochote na akapatia kwa asilimia 100%
 
Umesema ni “kama imani tu”.

Imani ni kitu cha kufikirika tu. Imani siyo uhalisia wa chochote.

Hivyo, uchawi ni kitu cha kufikirika tu.
Mkuu kuna vitu vya kufikirika ambavyo huwezi kuelezea mtiririko wa namna gani kimetokea ila unaweza kuona tu effect(matokeo) yake.
Mfano ni gravitational force.
Ukisoma historia ya mbuga ya katavi kulikuwa na mzungu alienda kuwinda wazee wa pale wakamwambia inabidi akaombe kwa mizimu kwenye mti hapo kijijini umruhusu vingenevyo hata pata kitu, akawalinga akaemda kuwinda na bunduki yake kila akipiga swala wanamuangalia tu huku wamesimama tena karibu risasi haziwadhuru, ikabidi arudi kwa wazee apelekwe kwa mizimu kwenye ule.mti ili auombe ruhusa. Alipoomba akarudi porini alifanikiwa kuwinda na akapata,
Alipoenda ulaya akarudi ndio akaja kuanzisha hiyo hifadhi ya katavi na story yake ipo hapo..
Au kule amboni ni lazima utambile ndio uingie kwenye yale mapango.
Au wale sharman kule bara la america wanatembea bila kukugisa ardhi. Sayansi au hii tdu tionist thinking ya rene descarte inashindwa kuelezea inaishia kupinga tu hicho kitu hakipo
 
Kiranga kuna species zaidi ya elfu kumi za mimea je unadhani mganga anaweza kujua ni mti upi unatibu tatizo fulani bila kuoteshwa? Hayo mambo ya manuizi nimeyashuhudia kwa macho yangu na matokeo nkayaona mimi mwenyewe kitu ambacho sijaona ni kupaa kwa ungo ninacho kiongea nmeshuhudia kwa macho yangu na mm nilikuwaga mbishi sana kipindi cha nyuma nilikuwa mfuasi wako lakini baadae niliamua kuutafuta ukweli
 
Ni kweli mkuu enzi zile papa ndio alikuwa anaongoza kwa sheria za kanisa watu kama bruno, Copernicus, Galileo walipotoa mitazamo tofauti juu ya kanisa walifungwa na kuchinjwa wengine.
Ukweli matokea ya baada ya hayo ndio tukapata reductionist thinking iliyo asisiwa na rene descarte ambayo kwenye hiyo thinking uchawi hauna nyenzo ya kuupima.
Mfano mtu kupaa na ungo angani sayansi itatafta lifting force, energy inayo hitajika kutima huku mchwi hana engine kwenye ungo wake unaouwezesha kupata hapo ndio tuna rudi kwenye esoteric knowledge.
 
Kuna hicho unachokisema, qmbacho kwenye sayansi ya tiba kinaitwa "placebo effect". Ni sehemu ya saikolojia.

Lakini, kwa anayehoji kwa nini kuna sheria na maneno mengi dhidi ya imani ya uchawi, mpaka serikalini, kama uchawi haupo, inawezekana imani ya uchawi ikaleta madhara bila uchawi kuwepo.

Mfano ni wale bibi wazee waliokuwa wanauawa kwa kusemwa wachawi. Mauaji haya yaliwahi kumfanya marehemu Ali Hassan Mwinyi ajiuzuku uwaziri wa mambo ya ndani miaka ya 1970.

Wale wauaji waliamini kuwa wanawake wazee wenye macho mekundu ni wachawi. Kumbe wale kina bibi wengine macho yao mekundu kwa sababu wanapika kwa kuni kwa mida mrefu wanakaa kwenye moshi wa kuni.

Wakawa wanauawa kwa imani za kichawi. Ingawa uchawi haupo, ile imani kwamba uchawi upo inaweza kusababisha mtu auawe.
 
Hiyo spiritual healing ni ujanja ujanja tu wa kutumia saikolojia kuwaponya watu kwa placebo effect. Na wengine wanataka kupewa assurance tu kwamba "fundi kashasafisha nyota" wakiambiwa hivyo wanapata psychological boost wanaenda kufanya kile ambacho hawakuweza kufanya.

Ni kama mtu anayevuta bangi kwa kunuia "bangi nibangue nilime ngwe hii nimalize" analima kweli anamaliza. Sio kwamba bangi inampa nguvu ya kulima, ila ile imani yake kwamba bangi inampa nguvu ya kulima ndiyo inampa nguvu ya kulima.
 
Umeshuhudia nini na unaweza kuthibitisha nini?

Kuota kuna mwanasayansi alishawahi kufikiria sana tatizo la kemia akawa hajapata jibu, alivyoenda kulala kwenye usingizi akaenda kuiota ile chemical compound benzene ilivyo, akapata jibu kwenye ndoto akamuona nyoka anayejiuma mkia, alivyoamka akaliandika lile jibu lika solve tatizo lake.

Ndoto ni processing tu ya mawazo uliyoyafikiria siku nzima at some subconscious level, kwa hivyo unaweza kulifikiria sana tatizo siku nzima, usipate jibu katika conscious mind, lakini, ukienda kulala umetulia subconscious mind bado inafanya kazi, bado unaprocess information zote, matokeo yake unaweza kuota jibu ndotoni.

Sasa, hapo kwa mtu anayeamini uchawi atasema huo ni uchawi kaoteshwa.

Lakini, kwa watu waliosoma psychology watakwambia hiyo ni subconscious mind tu inafanya kazi.

Soma zaidi kuhusu hiyo issue ya ndoto ya benzene

 
Nenda hata mapango ya amboni unapoingia ukataze wale wazee kufanya matambiko yao wambie yashapitwa na wakati kama unavyodai
Sasa huo utakuwa ni uchokozi. Itakuwa ni kuingilia mambo ya watu.

Sina tabia hiyo.

Ninaweza kusema uchawi haupo bila kuingilia mambo ya watu.

Uchawi haupo na wewe pamoja na yeyote yule anayeamini kuwa upo, hamuwezi kunithibitishia.

Halafu, neno la msingi hapo ni ‘kuamini’. Ukishaingiza ‘imani’ tayari unakuwa umeshaingia kwenye anga za kufikiri la tu.
 
Kufanyiwà matambiko ukienda mapango ya amboni kama mtalii unashauriwa ila haulazimishwi kwa kuwa unaamini haidhuru utawambia wasikufanyie uingie ufanye utalii.
Nimekutolea mfano wa mzungu aliye anzisha hifadhi ya mbuga ya katavi hakuamini kwenye kuomba mizimu chini ya miti.
Binafsi sijawahi kushuhudia uchawi ila nakubali kuna mambo ambayo hayafuati sheria za sayansi, logic na reductionist thinking ya rene descarte.
Ushauri watu mnaotaka kuthibitisha uchawi fanyeni research kama sayansi yenu inavyo wataka nendeni sumbawanga, kigoma, bariadi waambie mnatafta mtu wa kuwaroga ili kuthibitisha uchawi
 
Bado
Zama ndani zaidi...utapata ufahamu.
 
Mimi natoka Bariadi, Simiyu. Habari ni ile ile tu. Hakuna uchawi. Na mpaka sasa hakuna aliyefanikiwa kuniroga hapo Bariadi.

Hakuna aliyefanikiwa kuniroga kwa sababu uchawi haupo. Ni fiksi tu zinazotumika kutishia wajinga!
 
Hiyo spiritual healing ni ujanja ujanja tu wa kutumia saikolojia kuwaponya watu kwa placebo effect. Na wengine wanataka kupewa assurance tu kwamba "fundi kasha kulima ndiyo inampa nguvu ya kulima.
twende taratibu umesema ni mambo ya PLACEBO EFFECT na PSYCHOLOGICAL ASSURANCE, kwa mfano mimi na wewe tunafanya kazi ofisi moja mimi nkaamua kwenda sehemu kukutengeneza ww kesho asubuhi uzomewe kwenye kikao cha asubuhi na ufukuzwe kazi na boss pasipo kufanya kosa lolote na kweli ikawa hivyo je unaweza kuelezea mechanism behind ki placebo na ki psychological assurance? Je unajua ili placebo effect ifanye kazi sio lazima uwe kwa mganga tu hata daktari anaweza kukupa kidonge cha sukari bila wewe kujua na ukapona? Je unaweza kunipa mechanism ni jinsi gani placebo inaweza kufanya kazi kwa mgonjwa aliye chizika ambaye katibiwa na mganga wa jadi akapona akarudi kwenye ufahamu wake wa kawaida?
 
Kiranga unaijua definition ya HEALTH according to WHO kwa usahihi? je unawezaje kutenganisha physical, mental, social na spiritual well being ktk afya? tuanzie hapa kwanza
 
Basi wachawi wa JF watajaribu kurusha makombora yao kwa mtoa mada, utupe mrejesho tu mkuu lol
 
 
Hakuna uchawi wewe.

Nyie wote mnaouamini uchawi hamuwezi kunifanya chochote.

🖕
Ngoja nikuulize swali hili unijibu: Una amini kuwa Mungu yupo? Na je, wewe ni muumini wa dini kuu mbili hapa Tanzania yaani Ukristo na Uislamu? Nijibu ili tuanzie hapo
 
Mkuu hiyo michezo mbona hata kwa email tu unafanya, kuna uchawi gani hapo?

Fanya uchawi mtu apae na ungo tuone.

Kesho itoke kwenye TV kila mtu kaona.

Halafu tuje tujadili hapa.
 
Ushirikina ni story za kusadikika zinazotamalaki kwenye jamii za watu wajinga na maskini. Ni rahisi mtu wa Nanguruku kuamini kalogwa akiumwa malaria kuliko mtu wa Masaki.
Unasema wenzako ni wajinga na masikini kwa sababu ya uelewa wako finyu. Vitabu vitakatifu vinataja kuwa uchawi upo. Watu wengi wenye uelewa finyu kama wa nyie watu mnaopinga uwepo wa uchawi umepelekea watu wengi kupata madhara ambayo baadae yalikuja kuwafanya waamini uchawi upo.
Kuna watu kama wewe nawafahamu walikuwa hawaamini uwepo wa nguvu za giza. Ila yalitokea matukio ambayo yaliwafanya waamini uwepo wa nguvu hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…