Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Rusha ungo watu wote waone tumalize ubishi.

Wacha longolongo.
jibu maswali! Acha kukwepesha, wewe unaamini uchawi ni kuruka na ungo, hujui kuwa kuna jamii hawajui ungo ni kitu gani. Pia umesema unaijua vizuri saikolojia unaelewa nini kuhusu PSYCHOLOGY OF EDUCATION hasa hasa ktk kipengere cha aina za kujifunza? ukazungumzia habari za KEKULE na benzene nkakuuliza subcounscious mind ni nini na inapatikana sehemu gani ya mwili wa binadamu by anatomical position ? ndoto ni nini? je unaweza kuota kitu ambacho hujawahi kukiona? jibu maswali yote ndo tuendelee maana unaonekana hujui mambo mengi unakimbilia tu kugoogle ukishindwa sitaendelea kujadiliana na ww
 
hujajibu swali nlokuuliza
Swali gani? La placebo inavyofanya kazi?

Mfano nikikwambia sijui, hilo linamaanisha ni uchawi?

Kitu chochote ambacho hatujakijua jibu lake ni uchawi?

Na kama sijui sauti za watu zinakaa vipi kwenye CD ya muziki nayo niseme ni uchawi tu?
 
Thibitisha kuwa uchawi upo.
Kama wewe ni passionate learner tutaanza safari na utajifunza mwenyewe hadi utapata kuelewa uchawi upo na tena kuna parallel unseen world. Ila uwe open minded na unyenyekevu wa kutaka kujifunza.
 
jibu maswali! Acha kukwepesha, wewe unaamini uchawi ni kuruka na ungo, hujui kuwa kuna jamii hawajui ungo ni kitu gani. Pia umesema unaijua vizuri saikolojia unaelewa nini kuhusu PSYCHOLOGY OF EDUCATION hasa hasa ktk kipengere cha aina za kujifunza? ukazungumzia habari za KEKULE na benzene nkakuuliza subcounscious mind ni nini na inapatikana sehemu gani ya mwili wa binadamu by anatomical position ? ndoto ni nini? je unaweza kuota kitu ambacho hujawahi kukiona? jibu maswali yote ndo tuendelee maana unaonekana hujui mambo mengi unakimbilia tu kugoogle ukishindwa sitaendelea kujadiliana na ww
Wapi nimesema naijua vizuri saikolojia?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Unaweza kunipa nukuu nilipoandika naijua vizuri saikolojia?

Au unasoma kitu ambacho sijaandika, ila unachotaka kusoma wewe tu?

Umethibitisha uchawi upo? Wapi?
 
Kama wewe ni passionate learner tutaanza safari na utajifunza mwenyewe hadi utapata kuelewa uchawi upo na tena kuna parallel unseen world. Ila uwe open minded na unyenyekevu wa kutaka kujifunza.
Kama kuna parallel unseen world wewe umejuaje ipo?
 
jibu maswali! Acha kukwepesha, wewe unaamini uchawi ni kuruka na ungo, hujui kuwa kuna jamii hawajui ungo ni kitu gani. Pia umesema unaijua vizuri saikolojia unaelewa nini kuhusu PSYCHOLOGY OF EDUCATION hasa hasa ktk kipengere cha aina za kujifunza? ukazungumzia habari za KEKULE na benzene nkakuuliza subcounscious mind ni nini na inapatikana sehemu gani ya mwili wa binadamu by anatomical position ? ndoto ni nini? je unaweza kuota kitu ambacho hujawahi kukiona? jibu maswali yote ndo tuendelee maana unaonekana hujui mambo mengi unakimbilia tu kugoogle ukishindwa sitaendelea kujadiliana na ww
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Kwa uthibitisho wa kimantiki isiyo na logical inconsistency.

Thibitisha uchawi upo.
 
Imani ya uchawi ni chanzo kikubwa cha ujinga na umasikini.

Ukiamini uchawi huna sababu ya kufanya kazi ili ujiendeleze kiuchumi, utataka kupata maendeleo kwa uchawi tu.

Vivyo hivyo hutakuwa na haja ya kuondoa ujinga, utaamini uchawi utaweza kukubeba.

Hii ndiyo sababu jamii zinazoamini sana uchawi ni jamii za watu masikini na wajinga.

Watu watauana iki wapate ngozi za zeruzeru, wapate vichwa vya vipara, viwasaidie wapate utajiri.

Wakati wenzao wanavumbua sayansi na teknolojia za kutupa maendeleo makubwa.
 
Yawezekana ulikuwa na lengo zuri ila umeteleza kidogo!
Hata hao mashehe uliowataja kama uthibitisho wa hoja yako mara zote wamekuwa wakisema...

"KUNA WAGANGA/WACHAWI WANAOTUMIA MASHETANI KUFANIKISHA MAMBO YAO. Hapa masheikh wanasema kabisa kuwa hawa ni washirikina na atakayeandamana nao ataungana nao motoni. Kuonesha huo ushirikina hawawezi kwa sababu ni kufuru kinachofanywa. Pia maswala ya mashetani ni maswala yasiyo ya kawaida kwa hiyo kwa milango ya fahamu hivi ni ngumu

KUNA WAGANGA/WACHAWI WA KITAPELI AMBAO WANATUMIA UJANJA UJANJA. Hawa ni wajanja wa mjini na hawatumii mashetani na ndiyo maana hata wale maustadh wanaweza kuwaigiza na kuonesha janja janja zao wanazofanya kwa sababu ni mambo yanayomithilika kwa milango ya fahamu

Kwahiyo ungesema watu wangetumia smartphone kuepuka uchawi na utapeli lakini siyo kujifunza kuwa hakuna uchawi!
 
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Kwa uthibitisho wa kimantiki isiyo na logical inconsistency.

Thibitisha uchawi upo.
nakuuliza tena kwa mara ya mwisho kuna aina ngapi za kujifunza ili binadamu apate maarifa au abadiri imani kwa facts? Je unaweza kuota kitu ambacho hujawahi kukiona? Je subcounscious mind inakaa sehemu gani by anatomical position? NB: kila swali nlokuuliza linamaana kubwa sana kwenye huu mjadala ukishindwa kujibu ujue hauna uwezo kujadili hii mada
 
Nyie mnaotuambia ati uchawi haupo nadhani hamjawahi kuushuhudia live. Wacha nikupe story moja ya miaka ya 90 huko nikiwa bado ni mdogo kijijini kwetu.

Nakumbuka kulikuwa na msiba ambapo alifariki Mwanangwa tena ilikuwa kipindi cha masika imepamba moto. Siku ambayo maziko yanafanyika jioni yake kulikuwa na wingu kubwa sana la mvua na radi zilikuwa zinapiga hasa. Kiukweli iliaminika na wengi kuwa marehemu hawezi kuzikwa siku hiyo kutokana na aina ya mazishi yake ila wazee wakasema lazima azikwe.

Majira ya saa 12 kuliaza kama manyunyumanyunyu nikaona wazee na wamama fulani wameitana ndani ya kinyumba kimoja hivi cha nyasi. Baada ya muda nikaona mama mmoja mtu mzima akiwa amejipaka kama unga usoni amevalia kaniki nyeusi ametoka nje akaenda akakaa katikati ya kiwanja akainua mikono juu. Wazee wengine wanne katika haiba kama ya yule mwanamke wakaenda kwenye kila pembe ya kiwanja wakasimama wakiimba na kuchezacheza. Amini usiamini ilishuka mvua kubwa iliyoambatana na radi majira ya saa moja usiku ila hakukudondoka hata tone moja eneo la kiwanja kulipokuwa na yale maziko.

Maziko yalifanyika na taratibu zote ziliisha majira ya saa 3 usiku na wakati huo wote radi ilikuwa ikipiga na mvua ilikuwa inanyesha ya kufa mtu maeneo ya jirani na pale, kiasi mpaka njia zilijaa matope ila nyumbani kwa marehemu kulikuwa pakavu kabisa kwa muda wote. Watu walitawanyika baada ya maziko na hakuna yeyote aliedondokewa hata na tone la maji katika mji ule kipindi chote cha maziko na kiukweli tuliopigwa na mshangao tulikuwa ni wengi tusiamini iliwezekana vipi mvua isinyeshe pale eneo la msiba.

Ile sayansi iliyotumika pale ndio inaitwa uchawi sasa. Huwezi kuona mechanism gani imetumika ila matokeo huwa ni dhahiri.
 
Imani ya uchawi ni chanzo kikubwa cha ujinga na umasikini.

Ukiamini uchawi huna sababu ya kufanya kazi ili ujiendeleze kiuchumi, utataka kupata maendeleo kwa uchawi tu.

Vivyo hivyo hutakuwa na haja ya kuondoa ujinga, utaamini uchawi utaweza kukubeba.

Hii ndiyo sababu jamii zinazoamini sana uchawi ni jamii za watu masikini na wajinga.

Watu watauana iki wapate ngozi za zeruzeru, wapate vichwa vya vipara, viwasaidie wapate utajiri.

Wakati wenzao wanavumbua sayansi na teknolojia za kutupa maendeleo makubwa.
mimi nimejionea kwa macho yangu zaidi ya mara 10 utaniambia nini mkuu? Unataka uthibitishiwe hapa kwa maandishi? Utasubiri sana
 
Hilo ni tatizo kwa wewe tu ambaye unaamini biashara haziwezi kukua exponentially.

Unaamini labda kuwa lazima mtu apate 1 halafu 2 halafu 3,4,5,6..... au aende nara mbili mbili aani 2, 4, 6, 8......

Lakini kwa nini usikubali kuna exponential growth katika biashara mfano 2, 2, 7, 25, 140, 5445 hivyo aaani
Inategemea na ni biashara gani inayofanywa
 
Kiukweli umethibitisha maneno yake kuwa anaweza kukufanya superhero.

Hao wanaopewa dawa za kutongoza wanawake, si wanapewa kujiamini mbele ya hao wanawake. Na mwanaume anayejiamini anashindwaje kutongoza na kulala na wanawake atakao.

Ona;
Kabla - hajiamini hata kutongoza hawezi hadi kaenda kwa mganga
Baada - amepewa makonfidensi na mganga kuwa wanawake wanampaparukia, mvuto anao sasa amejiamini na anawapata kweli

Hujaona kama mganga amemtengeneza superhero anayeenda kwa jina la Kitombi saa hii mtaani????
Haha, inawezekana. Ila kuna kesi unaona kabisa huyu jamaa dawa aliyotumia kweli imefanya kazi. Maana unakuta dem ana respond isivyo kawaida
 
nakuuliza tena kwa mara ya mwisho kuna aina ngapi za kujifunza ili binadamu apate maarifa au abadiri imani kwa facts? Je unaweza kuota kitu ambacho hujawahi kukiona? Je subcounscious mind inakaa sehemu gani by anatomical position? NB: kila swali nlokuuliza linamaana kubwa sana kwenye huu mjadala ukishindwa kujibu ujue hauna uwezo kujadili hii mada
Nakwenda na hiyo statement yako ya mwisho si kwa sababu nimeshindwa kujibu maswali yako, bali kwa sababu nataka kuonesha logical fallacy ya non sequitur.

Tuseme sina uwezo wa kujibu maswali yako yote ya kuungaunga hayo.

Wewe bado hujathibitisha uchawi upo.

Niloge nishindwe kukujibu hapa JF tu tujue uchawi upo.

Nimekupa mtihani mdogo tu ku prove uchawi upo.
 
mimi nimejionea kwa macho yangu zaidi ya mara 10 utaniambia nini mkuu? Unataka uthibitishiwe hapa kwa maandishi? Utasubiri sana

Umejionea nini?

Kujionea kwa macho yako si uthibitisho kwamba kitu kipo.

Unaweza kuona chemchemi ya maji jangwani, kwa mirage, wakati haipo.

Lakini pia, ukisema tu "nimeona kwa macho yangu" hilo hallithibitishi hata kama umeona kwa macho yako.

Thibitisha uchawi upo. Inaonekana hata huelewi uthibitisho ni nini.
 
Waganga wengi wanawapiga pesa misukule ,niliona video za huyo sheikh kweli nikagundua wajinga waliwao.

Mganga anachofanya ni kukujengea imani tu na kuamini kwamba hii dawa itanitibu kumbe hamna kitu.....Sasa Mganga anakwambia ili biashara yako iende vizuri amka saa 11 kabla watu hawajaamka fagia kisha nyunyuzia hii dawa halafu usiku funga wa mwisho then nyunyuzia dawa kwa mantic hiyo ni lazima utawapata wateja wale wa asuhubi sana na wale wa late night hivyo kuboost mauzo.

Au mama ntilie anaenda kwa mganga kisha mganga anamwambia hii dawa inahitaji mtu awe safi yaani mazingira yawe safi hapo ndiyo jini atakaa na kuvuta wateja ,bila kujua wateja wa chakula wanapenda mazingira na usafi wa wapikaji/wahudumu.
 
Ni kweli mkuu.

Hakuna uongo rahisi kumdanganya mtu kama uongo ambao yeye anataka kuusikia.

Kwa hivyo hao waganga wanatumia saikolojia ndogo tu kujua udhaifu wa mtu na kumdanganya humo humo.

Kuna watu wawili walikutwa wanacheza uchi pembeni ya gari Mombasa Kenya.

Watu wakajaa kuwatazama.

Habari ilikuwa ni kwamba wale watu wawili waliokuwa wanacheza uchi, walikuwa ni wezi walioiba gari yenye "alarm" ya kichawi, imewanasa.

Sasa hapo kwa watu wanaoamini uchawi, hicho kitendo kilikuwa ni uthibitisho kwamba uchawi upo.

Lakini polisi wa Mombasa walifanya uchunguzi wakagundua kuwa, ule wote ulikuwa ni mpango wa mganga mmoja wa kienyeji kujutangaza. Wale watu waliokuwa wanacheza uchi walikuwa wamelipwa ili kumtangaza huyo mganga, watu waone mganga fulani ana dawa kali ya kulinda gari.

Sasa hapo kwa mtu ambaye anaamini uchawi huo ni uthibitisho tayari atasema "nimeona kwa macho yangu watu wanacheza uchi", kama alivyosema OMOYOGWANE kumbe ni utapeli wa watu tu.

Story ya hao matapeli wa Mombasa ipo hapa.

Back
Top Bottom