Ukisoma,"Coming out by night. Set" nadhani ndivyo kinavyoitwa kile kitabu,utaona "Wanga" wanatajwa.
Kaka mkubwa heshima yako.
Shukurani kwa kutupa reference.
Kuna vitabu vingi vinataja uongo mwingi tu. Kuna hadithi za uongo zimehalalishwa kabisa, fiction. Kuna watu wanaandika non fiction kama biographies zina uongo mwingi.
Professor Yuval Noah Harari muandishi wa "Sapiens: A Brief History of Humankind" na "Homo Deus : A Brief History of Tomorrow", among other books, ameandika sana kuhusu kitu kinaitwa "manufactured reality". Jinsi watu wanavyoweza kujitungia reality yao ya uongo na kuikubali kama ukweli.
Kuna psychology na sociology kubwa sana ambayo inaweza kuwa na maana kiutamaduni na hata practical tu, ambayo inaweza kuelezwa kwa shorthand ya "wanga" na "uchawi" kwa sababu hizo ndizo "mental models" ambazo watu wa sehemu fulani wanaweza kuzielewa tu.
The story is not factually correct, but it is useful and good because it serves a certain purpose.
Nitakupa mfano mmoja niliusoma katika kitabu cha Jean Paul Sartre. Alikuwa anaelezea mfano wa kijiji kimoja kikichokuwa na kisima cha maji. Kisima hicho kilikuwa na matatizo, maji yake yalikuwa na sumu. Sumu inaua. Sasa, wale viongozi wa kijiji hawajui sayansi, hawajui kemia, hawawezi kuielezea sumu ile factually kwamba kisima hiki kina arsenic water, dangerous levels of arsen, mkinywa maji yake mtaugua cancer na kufa.
Lakini, waliweza kuona watu wanaokunywa maji ya kisima wanaumwa, just by simple observation.
Viongozi wale wakaja na maelezo kuwa kisima kile kina majini. Ukinywa maji yake utaumwa na kufa. Watu wanaelewa na kuogopa majini, hawaelewi habari za arsenic water. Hivyo, kuwakataza watu wasinywe maji ya kisima kwa story ya majini kunakuwa effective zaidi kuliko kusema habari za kufundisha somo la kemia la arsen ni nini na inasababishaje matatizo ikipatikana katika maji.
Kwa hivyo viongozi wa kijiji wakaenda na story ya majini. Story inayokubalika. Story inayoeleweka.
Na mpaka leo, habari nyingi za uchawi, supernatural, Mungu, dini, ni kama hivyo, ni habari za kutupa majibu pale ambapo hatukuwa na majibu. Tukipata majibu tunaziacha.
Ukimsoma Dr. Paul Kugel (Harry M. Starr Professor Emeritus of Classical and Modern Hebrew Literature at Harvard) katika kitabu chake "How to Read The Bible: A Guide to Scripture Then and Now" ameelezea vizuri habari za Bible 8livyobadikishwa badikishwa iki ku solve matatizo ya Hebrews. Na hizi stories za uchawi kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya stories za dini tu.
Leo North America huku kuna solar eclipse. Tunajiandaa kutazama kupatwa kwa jua.
Miaka 500 iliyopita huku kuna sehemu tukio hili lilikuwa la kuogopesha sana, walilipa umuhimu wa ki supernatural sana, wengine mpaka wakachinja watu wao katika humannsacrifice rituals, wakiamini kuwa jua lilikuwa linataka kuzimika na hizo human sacrifices zitakuwa sadaka ya kuli appease jua lisizimike. Leo tumejua sayansi ya nyendo za jua, mwezi na dunia, na tunaweza kutabiri kupatwa kwa jua kwa kupatia sana hata kwa maelfu ya miaka yajayo, tukajua mpaka mji ganinutaona totality na mji ganiutakuwa nje ya totality kwa kiasi gani.
Kwa hivyo, hizo habari za uchawi, wanga etc, zilikuwa na purpise yake wakati hatujapata sayansi nzuri ya kuelezea mambo.
Sasa hivi tumepata mfumo mzuri wa kufuatilia mambo kisayansi, tuyafuatikie kisayansi. Tuondokane na habari za uchawi ambazo kwa kweki zimepitwa na wakati dunia hii.