Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Siamini uchawi, najua it's all psychological games. Ila mleta mada tungeomba utupe resources zaid, au links za kupata hizo evidence ulizoelezea hapo. Like how does it work step to step!
 
Wengi wanaosema hakuna uchawi ndo unakuta ndo wachawi wenyewe au wana interest zao huko

Kuna uhusiano gani kati ya jamii maskini na yenye elimu duni na uchawi?

Maana jamii zilizoendelea na zenye elimu haziamini huo uchawi.

Kimantiki unaweza ukasema, ili uamini uchawi upo itakupasa aidha uwe mjinga na upeo mdogo wa kufikiri au uwe maskini. Au vyote viwili kwa Pamoja
 
Kwanza nini maana ya uchawi,, maana hata kwenye dini tu huyu akiamini hivi akimuangalia mwenzake anaeamini hivi tayari anaweza akasema huyu ni mchawi
 

ukisoma human psychology na ukaelewa vizuri. utapata majibu kwa nini baadhi ya watu wakienda kwa waganga wanapona magonjwa yao. waganga wanacheza na biological, psychodynamic, behavioral, cognitive, and humanistic psychology katika kumfanya mtu ajione amepona ugonjwa wake.

kuhusu kupata pesa ama utajiri waganga wanacheza pia na human psychology ya kukupa masharti ambayo yatakufanya uwe mbahili na unatunza sana pesa na kuwekeza.
ndio maana matajiri wanaoenda kwa waganga ama wachawi huwa wanavaa rafu rafu, wanakula vibaya. ile ni financial education waliyopewa kwa masharti ya waganga bila wao kujijua kama ni human psychology wamechezewa.

ukienda kutazama video za mganga mstaafu youtube utaona ameelezea sana kuhusu hizo mbinu za waganga katika kuwafanya wafanyabiashara wawe matajiri
 
Kwani nini maana ya uchawi
 
Ni ngum kidogo kuamini unachosema kwa sababu unakuta mtu huyo ambae anasemwa kua katumia ushirikina kupata mali, ni mtu ambae hakua na biashara kubwa ya kusema imempa mali nyingi ndani ya muda huo mfupi hata kama angetumia elimu ya aina gani kuongoza biashara yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…