Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Hakika nakuambia, amini usiamini, kila penye mafanikio hasa yale ya ghafla, ushirikina upo. Unakumbuka nabii Issa alipomtoa mtu mapepo kisha yakakimbila kwa nguruwe, moja kwa moja mpaka baharini? Huo ndio uchawi ulioshuhudiwa na Yesu. Watu wanaishi kishirikina kwa siri na kuwahadaa watu! Acheni hizo!! Kuna mmoja alikataa kabisa mambo ya uchawi, akapigishwa chura tumboni, sauti ya chura ikawa inatoka tumboni, akaaguliwa na hao aliowadharau. Sasa hivi yupo makini na anaamini uchawi.
unaleta story za biblia. hata ulaya waliachana na kuwinda wachawi baada ya kugundua biblia ina ujinga mwingi,

mfano biblia imeandika nyoka anaongea na binadamu, wewe kwa akili yako ya kawaida unaamini nyoka anaweza kuongea na binadamu kweli ?


Why did witchcraft trials begin to decline in the mid-seventeenth century?

Short answer….. Society was sick of the Church breeding fear into everyday life
 
Mtu akimkuta ng'ombe mbele yenu mita 5. Akamgeuza kuwa mbuzi. Hiyo ni trick isiyo ya kiuchawi? Kwamba ametumia speed? Kamchukua ng'ombe kampeleka like kisha kaka na mbuzi fasta?

usitoe mifano ya kujitungia tu, weka ushahidi nani amewai kumgeuza ngombe kuwa mbuzi ?

uhalisia ni kwamba hakuna Mchawi, Mganga, nabii na wala mwana mazingaombwe anayeweza kumgeuza ngombe kwa mbuzi
 
Ta

Tanzania kuna Sheria inayoharamisha uchawi/ushirikina. Kama ingekuwa uchawi haufanyi kitu Watu wangeruhusiwa tu waendelee nao

sheria hiyo ilitungwa mwaka 1928 kwa lengo la kudhibiti watu kujihusisha na imani potofu na vitendo vya kichawi lakini ni vigumu kuvithibitisha mahakamani.

Sheria hiyo imefanyiwa mapitio mara tano yakiwemo ya mwaka 1935, 1956, 1998, 2002 na mwaka 2022

kwa sheria inayotumika leo hii ya mwaka 2022 mahakama haiwezi kuthibitsha uchawi . hukumu za kesi za uchawi zinafutwa

1712142137188.png
 
Mtu
sheria hiyo ilitungwa mwaka 1928 kwa lengo la kudhibiti watu kujihusisha na imani potofu na vitendo vya kichawi lakini ni vigumu kuvithibitisha mahakamani.

Sheria hiyo imefanyiwa mapitio mara tano yakiwemo ya mwaka 1935, 1956, 1998, 2002 na mwaka 2022

kwa sheria inayotumika leo hii ya mwaka 2022 mahakama haiwezi kuthibitsha uchawi . hukumu za kesi za uchawi zinafutwa

View attachment 2952747
Mtu akikiri je? Maana Umesema ni ngumu kuthibitisha. Mfanya uchawi ikiwa akakiri na anaomba asamehewe,hatarudia. Hakuna Sheria ya kumfunga?
 
Hili jambo lina maswali mengi sana yanayohitaji majibu ili kuweza kulithibitisha.

Kwa sababu ukijaribu kuangalia unaona kuna watu wanapata matatizo wanaenda kwa waganga na matatizo yao kweli yanaisha. Ukiangalia kuna watu wanatumia ndagu kupata pesa na kweli wanapata pesa na mali zinaonekana, jambo zinakua na mambo mengi ila still watu tunamuona kua flani kapata pesa na kunakua 'na za chini' za kuaminikakua pesa alizopata ni za kishirikina(manake ushirikina umefanya kazi).

Ila still pia kuna kesi mtu kapata tatizo anakimbilia kwa waganga ila ukiangalia tatizo ni la kawaida wala sio hata la kishirikina, lakini waganga wanamwambia ni la kishirikina na mtu anawaamini, wanaishia kumpiga tu hela na kufanya kweli ionekane kua waganga na ushirikina kwa namna flani kama havina ukweli.

Kwaio ni maswali juu ya maswali
 
habari wadau

binafsi nashangaa sana watu hasa wasomi wenye smartphone wanaoamini story za ushirikina zama hizi

ukweli ni kwamba ukijipa muda wako kujifunza zaidi jinsi Human physiology na Science of Emotion ilivyo. watajua ukweli mwingi sana wa ubongo wa binadamu unavyofanya kazi na unavyodanganyika

watu wakijipa muda zaidi na kusoma kuhusu history za uchawi hasa msako wa wachawi (Witch Hunts in the Western World) kwenye karne zilizopita ulikuaje na kwa nini kilisababisha msako huo usitishwe. pia wakasoma kuhusu msako wa wachawi uliotokea marekani pia maarufu kama The Salem Witch Hunt na ilikuaje marekani wakaachana na misako hiyo pia, watajua ukweli kuhusu uchawi.


kisha wakarudi kwenye youtube na kuangalia video za magic tricks zinavyofanya kazi. watajua waganga na wanaojifanya wachawi wanatumia mbinu gani kuhadaa watu


mfano kuna video nyingi za youtube za Sheikh Othman michael akishirikiana na Shehe Jafar kitwana ( mganga mstaafu) wakieleza kila kitu kuhusu uchawi na huku wakionesha na mifano ya jinsi waganga wa kienyeji na wachawi wanavyotapeli watu. yaani hakuna mganga ataeweza kukudanganya ukielewa mbinu zao na mazingaombwe yao.


Nashangaa sana kijana wa zama hizi kuamini ushirikina na kwenda kwa waganga wa kienyeji wakati elimu zinapatikana kwa urahisi sana.

jamani kwenye internet tusiangalie tu kina mwijaku na diamond. tumieni internet kupata elimu na kuelewa jinsi ya kusolve changamoto zetu.


View attachment 2952643
Aisifuye Mvua, imemnyea.
 
Back
Top Bottom