Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Hili jambo lina maswali mengi sana yanayohitaji majibu ili kuweza kulithibitisha.

Kwa sababu ukijaribu kuangalia unaona kuna watu wanapata matatizo wanaenda kwa waganga na matatizo yao kweli yanaisha. Ukiangalia kuna watu wanatumia ndagu kupata pesa na kweli wanapata pesa na mali zinaonekana, jambo zinakua na mambo mengi ila still watu tunamuona kua flani kapata pesa na kunakua 'na za chini' za kuaminikakua pesa alizopata ni za kishirikina(manake ushirikina umefanya kazi).

Ila still pia kuna kesi mtu kapata tatizo anakimbilia kwa waganga ila ukiangalia tatizo ni la kawaida wala sio hata la kishirikina, kwa namna flani kama havina ukweli.

Kwaio ni maswali juu ya maswali
hicho ulicho andika ndicho kilichosababisha huko australia madaktari wote wawe wanapewa training ya traditional medicine ili kuweza kubaini kama mtu anachangamoto ya upande wa pili na kumpa rufaa kwenda kwa herbarist
 
Ni ngum kidogo kuamini unachosema kwa sababu unakuta mtu huyo ambae anasemwa kua katumia ushirikina kupata mali, ni mtu ambae hakua na biashara kubwa ya kusema imempa mali nyingi ndani ya muda huo mfupi hata kama angetumia elimu ya aina gani kuongoza biashara yake
Hilo ni tatizo kwa wewe tu ambaye unaamini biashara haziwezi kukua exponentially.


Unaamini labda kuwa lazima mtu apate 1 halafu 2 halafu 3,4,5,6..... au aende nara mbili mbili aani 2, 4, 6, 8......

Lakini kwa nini usikubali kuna exponential growth katika biashara mfano 2, 2, 7, 25, 140, 5445 hivyo aaani
 
Kuna uhusiano gani kati ya jamii maskini na yenye elimu duni na uchawi?

Maana jamii zilizoendelea na zenye elimu haziamini huo uchawi.

Kimantiki unaweza ukasema, ili uamini uchawi upo itakupasa aidha uwe mjinga na upeo mdogo wa kufikiri au uwe maskini. Au vyote viwili kwa Pamoja
wachaga unawajua? Ni masikini au sio wasomi? Je kila mwisho wa mwaka hua wanaenda kufanya nini huko kilimanjaro licha ya kuwa ni wasomi wakubwa?
 
Watu wengi wachawi wanapinga kwamba uchawi haupo ili wazidi kuumiza wengine kwa uchawi sasa akilini kichwani mwako ndgu yangu
 
Habari wadau

Binafsi nashangaa sana watu hasa wasomi wenye smartphone wanaoamini story za ushirikina zama hizi

Ukweli ni kwamba ukijipa muda wako kujifunza zaidi jinsi Human physiology na Science of Emotion ilivyo. watajua ukweli mwingi sana wa ubongo wa binadamu unavyofanya kazi na unavyodanganyika

Watu wakijipa muda zaidi na kusoma kuhusu history za uchawi hasa msako wa wachawi (Witch Hunts in the Western World) kwenye karne zilizopita ulikuaje na kwa nini kilisababisha msako huo usitishwe. pia wakasoma kuhusu msako wa wachawi uliotokea marekani pia maarufu kama The Salem Witch Hunt na ilikuaje marekani wakaachana na misako hiyo pia, watajua ukweli kuhusu uchawi.

Kisha wakarudi kwenye youtube na kuangalia video za magic tricks zinavyofanya kazi. watajua waganga na wanaojifanya wachawi wanatumia mbinu gani kuhadaa watu.

Mfano kuna video nyingi za youtube za Sheikh Othman michael akishirikiana na Shehe Jafar kitwana ( mganga mstaafu) wakieleza kila kitu kuhusu uchawi na huku wakionesha na mifano ya jinsi waganga wa kienyeji na wachawi wanavyotapeli watu. yaani hakuna mganga ataeweza kukudanganya ukielewa mbinu zao na mazingaombwe yao.

Nashangaa sana kijana wa zama hizi kuamini ushirikina na kwenda kwa waganga wa kienyeji wakati elimu zinapatikana kwa urahisi sana.

Jamani kwenye internet tusiangalie tu kina mwijaku na diamond. tumieni internet kupata elimu na kuelewa jinsi ya kusolve changamoto zetu.

Walimu ni ma goi goi ndio maana wamefurika kwenye mikutano ya injili kutafuta miujiza ambayo haipo.walimu bwana, ma kenge kweli kweli
 
Lakini je, hayo maneno machache kweli yanatafanya kazi na ntakua superhero?
Kwa sababu kuna dawa tunaona watu wanatumia za kupata wanawake na kwa namna furani unaona kweli zinafanya kazi
Kiukweli umethibitisha maneno yake kuwa anaweza kukufanya superhero.

Hao wanaopewa dawa za kutongoza wanawake, si wanapewa kujiamini mbele ya hao wanawake. Na mwanaume anayejiamini anashindwaje kutongoza na kulala na wanawake atakao.

Ona;
Kabla - hajiamini hata kutongoza hawezi hadi kaenda kwa mganga
Baada - amepewa makonfidensi na mganga kuwa wanawake wanampaparukia, mvuto anao sasa amejiamini na anawapata kweli

Hujaona kama mganga amemtengeneza superhero anayeenda kwa jina la Kitombi saa hii mtaani????
 
wachaga unawajua? Ni masikini au sio wasomi? Je kila mwisho wa mwaka hua wanaenda kufanya nini huko kilimanjaro licha ya kuwa ni wasomi wakubwa?

Kwa nini umetaja Wachagga?
Jamii karibu zote Tanzania robo tatu ya Watu wake ni Maskini. Alafu wenye elimu wachache. Hakuna cha mchagga wala sijui nani.
 
Naomba nipe namba yako nikupeleke kwenye nyumba moja ipo mbagala. Utalala hapo siku moja tu alafu utakuja kutoa humu ushuhuda utakacho kikuta hapo. Kodi ya nyumba tutakulipia wenyewe.
Acha kubishana na watoto wa mama ambao hawaelew dunia inaendaje kila kitu wao wanategemea kugoogle
 
Uju
mtu anapaa na ungo mchana kweupe umemuona wapi ?

kama ni kweli inakuaje hao wachawi wanashindwa kufika marekani na ungo ? Ama wao wachawi hawataki kuishi nchi zilizoendelea ?

ingekuwa kweli wachawi wana uwezo wa kupaa na ungo wazungu wangekuwa wanashangaa kuwaona waafrika wanaongezeka kwa Kasi ya ajabu kwenye nchi zao bila hata kuomba viza (kumbe wamepaa na ungo kwenda kwenye nchi badala ya kutumia njia hatarishi za kuzamia meli)
Ajuaji ukizid mwisho huwa unakuwa ni ushamba shaur yko
 
Mimi niseme tu kuwa watu mnapenda sana kurahisisha mambo pia mnapenda kutafuta habari zinazowafurahisha, mtu anajigamba amesoma PHYSIOLOGY yotn googln na pia amesoma PSYCHOLOGY yote google yaani hii ni dharau kubwa sana watu wanakaa darasani zaidi ya miaka minne wewe uje useme ni umemaliza kila kitu? ungekua umesoma human psychology na kuielewa vizuri usingeanzisha uzi wako maana umetaja mpaka mambo ya COGNITIVE ndani yake kuna PSYCHOLOGY of education na learning theories ungekuwa unazijua usingewaona watu wote wenye smartphone ni wajinga . pia ungekua unaijua history ya medicine vizuri usingeleta uzi wako. hivi ALBERT BANDULA, HYPOCRATES, TO YOUYOU na KEKULE unawajua? tumia simu yako kugoogle sawa! pia uchawi na uganga ni elimu ya siri na ni ngumu kuliko udaktari pia si kila mtu anaweza kufundishwa na shule yake huchukua miaka mitano mpaka kumi ndio maana hao unaowaona mtaani wengi ni matapeli ntaishia hapa wajuvi watakuwa wamenielewag
 
Habari wadau

Binafsi nashangaa sana watu hasa wasomi wenye smartphone wanaoamini story za ushirikina zama hizi

Ukweli ni kwamba ukijipa muda wako kujifunza zaidi jinsi Human psychology na Science of Emotion ilivyo. watajua ukweli mwingi sana wa ubongo wa binadamu unavyofanya kazi na unavyodanganyika

Watu wakijipa muda zaidi na kusoma kuhusu history za uchawi hasa msako wa wachawi (Witch Hunts in the Western World) kwenye karne zilizopita ulikuaje na kwa nini kilisababisha msako huo usitishwe. pia wakasoma kuhusu msako wa wachawi uliotokea marekani pia maarufu kama The Salem Witch Hunt na ilikuaje marekani wakaachana na misako hiyo pia, watajua ukweli kuhusu uchawi.

Kisha wakarudi kwenye youtube na kuangalia video za magic tricks zinavyofanya kazi. watajua waganga na wanaojifanya wachawi wanatumia mbinu gani kuhadaa watu.

Mfano kuna video nyingi za youtube za Sheikh Othman michael akishirikiana na Shehe Jafar kitwana ( mganga mstaafu) wakieleza kila kitu kuhusu uchawi na huku wakionesha na mifano ya jinsi waganga wa kienyeji na wachawi wanavyotapeli watu. yaani hakuna mganga ataeweza kukudanganya ukielewa mbinu zao na mazingaombwe yao.

Nashangaa sana kijana wa zama hizi kuamini ushirikina na kwenda kwa waganga wa kienyeji wakati elimu zinapatikana kwa urahisi sana.

Jamani kwenye internet tusiangalie tu kina mwijaku na diamond. tumieni internet kupata elimu na kuelewa jinsi ya kusolve changamoto zetu.

Wacha masihara wewe kuna jamaa saiv ni kipofu
 
Mtu anakuwa kipofu sababu ya uchawi ?

Hujawai kuona ng'ombe au mbwa amepata upofu. Na yeye anakuwa amerogwa ?
Acha kufananisha mnyama Na ambaye haongei.

Skia mkuu nakupa onyo tu kaa Mbali Na Mali Za watu Na hata ukimuibia boss wako basi usiibe kupitiliza ukataka kuwa kama yeye.

Huo ndio wosia wangu tu mkuu.Yakumbuke. Haya maneno.
 
Imani ya uchawi inaweza kuwa na madhara bila ya uchawi kuwepo, unaelewa hilo?
Yes umesema nilichotaka kusema! Ila umetumia maneno machache sana!

Ni kweli uwepo tu wa imani inatosha kabisa kutibu/kuloga/uponyaji n.k.

Hivo hata kama uchawi wenyewe haupo lakini kwa kujengewa imani na mganga (imani yako inakamilika kwa kumpelekea labda kuku n.k.) imani yako ndio itakuponya! (Kwa yale yanayoponyeka) kama huna imani kwa mganga wa kienyeji hutojoi
 
Akili ukishaijengea kitu Dylan huwa inaamin hivyo. Kuna nyumba niliwahi panga. Na ikiluwa na miaka kama 8 Haina mpangaji kisa Kila mpangaji alikuwa anaingia Ina mauza uza Sana. Lakin Mimi skuwahi kuwambiea Hilo tatizo wanalodai. Nilikaa kwenye hiyo nyumba Kwa mda wa miaka miwili bila kuyaona hayo mauza uza. Nimekuja kupewa taarifa hiyo mwaka wa pili mwishon na nikawambia Mimi siamin uchawi upo.

Nimekaa pale bila shida yoyote na kama ni kipato kiliongezeka mara 2 yake.

Tangu nilipohama Tena wameingia wapangaji kama wanna wanaacha Kodi zao. Kwa mauza uza wanayodai kukuktana nayo. Ila kwangu ni tofauti.

Hivyo basi ukiijengea akili yako Kuna uchawi na ushirikina itakuwa kweli. Lakini akili yako uspoijengea Kuna uchawi na ushirikina haiwezi kufanya kazi. Na uchawi hautamuwepo
Sometimes nyumba unakuta haina mzunguko mzuri wa hewa.

Mtu halali vizuri joto kali

Mtu anadai mauzauza ameona. Kumbe ni ndoto za kumtishia aamke asije jifia tokana na hali mbaya ya chumbani
 
Sawa mzee wa human saikolojy, siku ukitoka hapo kwa shem uje tena humu. [emoji23]

Hoja huwa inapingwa kwa hoja na facts

Wapumbavu Mkiona mmezidiwa hoja mnaanza matusi na kashfa. Hiyo ni kawaida ya watu wajinga.
 
Back
Top Bottom