Ukiumizwa na kutendwa, bado unaweza kutoa msamaha?

Ukiumizwa na kutendwa, bado unaweza kutoa msamaha?

Uchumba sio ndoa Hapo Mungu kakuonyesha ni mtu wa aina gani maamuzi ni yako uingie ndoani au usiingie. Bahati za kuonyeshwa mchumba alivyo kabla ya ndoa wanapata wachache Sana kama wewe. So shukuru, mlinde kisha temana nae kwa amani, maisha sio uadui wema ni akiba kesho uliyetemana nae utamkuta ofisi fulani atakusaida ukiwa na shida
Ataskip tu kesi itaisha kimtindo utaona!! Kaka nimepitia magumu zaidi ya hayo Maisha haya na sijawai kukaa hata nyuma ya nondo!! Ishu ni father alikuwa kamanda jeshini huko na polisi kibao anajuana nao we acha.

Ngoja nikupe ishu fupi! Mwaka fulani nikiwa form one shule fulani sijaitaja!! basi Kuna jamaa nilikutana na Kwa kumuangalia meno na uongeaji wake alikuwa ni mtu wa Arusha alikuwa mtu wa kujiona sana na majivuno... Tulikuwa sawa ila alikuwa kanizidi kama miaka 3 hivi kama sijakosea...Mimi kiasili ni mrefu yeye ni mfupi basi tuliendelea kusoma mpaka tukaanza kufanya paper alhamdullilah Mimi nilisoma pre form one so nilikuwa vizuri sana masomo mageni kwangu nilikuwa ya book keeping na commerce...

Huyu mchzi na Mimi before sikuwai kutamani kujuana nae kwa vile alikuwa mshamba hana ustaarabu na pili alijifanya kwao Wana hela ila sio kweli.
Siku moja baada ya likizo ya mwezi wa sita nilikutana tulikuwa yeye kanipita kinafasi darasani yeye wa 3 Mimi wa nne ila mi hesabu nilikuwa nazifahamu yeye alipata vibaya....mi nilikuwa mkimya sana basi jamaa tukakutana kweny kipind cha dini tulianza kusoma baada y mwezi wa sita nyuma hatukuwa na mwalimu ila ni option sio kila muislamu lazima asome so tulikuwa wachache sana ...Basi tukazoeana sana mpaka nikaja kugundua jamaa alifeli darasa la Saba akarudi yaani mm nikiwa la tano yeye alikuwa la Saba akarudi ndo tukawa nae sawa form one .

Ikawa jamaa anakuja home mi nilikuwa na nguo najibana shule kila weekend niko mtumbani ,milupo kibao haswa vimodo mashati ninayo kibao jamaa akawa kma ananisifia kuvaa alikuwa getto nilikuwa nakaa na bro jamaa kufungua kabati Nina nguo kibao akiomba Nampa kama msela ila hana shukrani kabisa watu wa Arusha roho zao Zina majivuno mno ..siku moja alikuwa akija home hata kama sipo wanamjua wanaweza muelekeza getto akaingia hata kulala mi kama sipo maana sikuwa na simu ...Jamaa alikuwa chukua nguo getto zangu na bro akijua zote ni zangu akaondoka na begi lake bila ya Mimi kurudi ilikuwa msala sana bro kama mwambia father na Kuna nguo bro alikuwa anaficha pesa yaani jeans yake palikuwa na pesa kama elfu 50 miaka iyo pesa ndefu jamaa kasepa...Nakuja mwambia eti kanunua anasema pesa hzipo na nguo eti atarudisha mzee wangu akanipiga kinoma mpaka nikaumwa .

Kipind fulani jamaa form two alikuja kuchukua simu kwa ndugu anaokaa nao then alikimbia bila ya kuaga kwenda kwao Arusha,ile siku alinipa mimi ilikuwa philiphs eti tutawasiliana sasa sijui ya nn? Ndugu wakambana akawaelekeza home kwamba Mimi ndo ninayo na siku fulani nilienda kwao wale ndugu zake waliniona wakaja na polisi kama mi ni mwizi mpaka home nikatoa simu ya watu sijaiba wakati jamaa alinipa nikae nayo mpaka akirudi..
Kufika form 3 nikatemana nae mpumbavu alikuwa anakuja home tunakula fresh nikamwambia marufuku kwanza hauna ustaarabu.
 
Katika maisha haya bado nawaza tofauti ya kuumizwa na kutendwa maana najua mtu kukuumiza ni pale amekuonea au kupoteza imani yake juu yako lakini kutendwa na jua tu labda kwenye usaliti wa mapenzi au umeachwa, ila mimi juzi yaliyonikuta hata nalia kwa uchungu kwani mwanaume niliyechumbiwa naye kwa miaka 2 amenisaliti tena na shangazi yangu na bado kanipora mali zangu na juu ya hapo kinanisikitisha kujua kuwa ni mhalifu kutoka Kenya na anatafutwa na polisi.

Na zaidi ya yote kunifanyia hayo mimi ndo mtu pekee niliyesalia kupelelezwa na polisi kuhusu maficho yake. Kwa moyo wangu nataka nimpeleke polisi lakini ananiambia kasingiziwa na hana hatia na ameniomba na kunitaka sana kumstiri kwa polisi.

Sa sijui nifanyeje?
Shangazi na jamaa yako hawajuani? Je unamwacha au unaendelea naye?
Kumbuka hujaolewa, na hata wanandoa, kuzini ni kigezo tosha cha kutalikiana. Kazi kwako!
 
Shangazi na jamaa yako hawajuani? Je unamwacha au unaendelea naye?
Kumbuka hujaolewa, na hata wanandoa, kuzini ni kigezo tosha cha kutalikiana. Kazi kwako!
Inamaana mfano mke akimfumania mume anazini anastshili kupewa talaka??
 
Back
Top Bottom