Ukiwa chanya Katika maisha yako Mungu anaondoa watu hasi kwenye maisha yako

Ukiwa chanya Katika maisha yako Mungu anaondoa watu hasi kwenye maisha yako

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
997
UKIWA CHANYA MUNGU ANAKUONDOLEA WATU HASI KWENYE MAISHA YAKO

Anza kubadilisha maisha yako, kuwa mtu chanya, Mtu chanya ni mtu ambaye anaishi maisha yenye kuona mambo kwa uzuri.

Mtu chanya ni mtu anayependa mafanikio ya wengine, ni mtu ambaye atoi maneno ya kukatisha tamaa wengine, ashiriki umbeya wa kusema changamoto za wengine ili kujisikia vizuri kwenye maisha yake.

Unapokuwa mtu hasi ambaye muda wote ni kulalamika, kucheka wengine wanapoanguka, kuangusha wengine, hii inapelekea ata circle yako kuwa na watu wenye tabia kama zako.

Kuwa mtu chanya ambaye unapambania ndoto zako, unatafuta mafanikio, unataka kuwa na kesho bora.

Ukiwa mtu chanya unafanya kuwa na frequency ya juu(aura) hii inapelekea kuvuta watu chanya kwenye maisha yako.

Ukizungukwa na watu chanya utaanza kuona fursa, kupata tumaini, utaanza kuona kila kitu kinawezekana, watakufanya uchukue hatua kwenye ndoto zako, utakuwa na hamu ya kufanikiwa.

Mazingira yana mchango mkubwa wa kufanikiwa kama upo na kundi ambalo aliamini katika kufanikiwa muda wote ni kulalamika inakuweka katika wakati mgumu wa kufanikiwa.

Matajiri wanajitenga unaweza jiuliza labda wana Lengo baya hapana, matajiri wengi wapo katika frequency kubwa(nguvu) hivyo ukishakuwa katika frequency au energy kubwa afu uka ambatana na mtu hasi hii inapelekea kunyonya nguvu zako au nyota yako.

Hii inaweza kutokea umekutana na mtu muda wote ana lalamika, anaponda wengine unajikuta unajisikia uchovu na kuchoka jua kakunyonga nguvu zako.

Mtu hasi anakuwa na energy ndogo(nguvu) hii inapelekea hata fursa kumkimbia kwenye maisha yake.
 
Back
Top Bottom