kibobori mahoro
JF-Expert Member
- Dec 12, 2022
- 7,452
- 10,785
Labda kuna mtu kakuchomekea biashara kama ya kwako pembeni na akakuzidi kwa mbinu za biashara.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bila kutaja aina ya biashara ni ngumu mm kutoa ushauriNdugu zangu naombeni mnipe mbinu za kufanya kwa mtua liyeanza biashara alafu WATEJA MWANZONI WALIKUA WANAKUJA TU ILA KWASASA NI WEEK INAENDA WATEJA NI WA KUSUA SUA HASA MWEZI HUU. Nifanyejeeee? Maana biashara ni mpya na sitaki kuifunga
Bei yako ni rafiki au unakomoa wateja?Ndugu zangu naombeni mnipe mbinu za kufanya kwa mtua liyeanza biashara alafu WATEJA MWANZONI WALIKUA WANAKUJA TU ILA KWASASA NI WEEK INAENDA WATEJA NI WA KUSUA SUA HASA MWEZI HUU. Nifanyejeeee? Maana biashara ni mpya na sitaki kuifunga
Hey mbona hujaeka no. Tukasababidha chochote!? Maana hii elimu mtu hupati bureBei yako ni rafiki au unakomoa wateja?
Kuna jamaa kafungua duka jipya Bei zake ni tofauti na Bei za maduka jirani mfano sabuni mche unaouzwa 3500 yeye anauza 4500, mafuta ya kupakaa 1500 yeye anauza 2000, Sigara ya 250 yeye anauza 300, dawa ya meno Colgate ya 2000 yeye anauza 2500, ndala za 4000 yeye anauza 5000, dawa ya meno Colgate ya 4000 yeye anauza 5000, pipi Ivory ya 50 yeye anauza 100, mchele wa 3500 yeye anauza 4000 hadi 4200, mafuta kipimo cha 300 yeye anauza 500, karanga mbichi kilo za 3000 yeye anauza 3800 hadi 4000, mafuta Lita 1 ya chupa wenzake wanapack wanauza 5000 yeye anauza 6500 mpaka 7000
Yaan unategemea mteja gani atakuja huku unataka kumuuzia kwa bei za kukomoa si ataenda kununua penye urahisi?
Kwa mteja hata 50 tu Ina matter kwake yaan duka la pili linauza keki 200 duka lako keki ile ile unauza 150 keki zako zote zitaisha Ila keki za duka la pili hazitatoka na wateja watajaa kwako, biashara ni fumbo Pana sana yaan wanaotoboa ni wale wanaojua kucheza na akili za wateja
Yaan mteja pale kuna duka la jumla na pale kuna duka la rejareja, akienda duka la jumla anaambiwa unga kilo ni 1900 akienda duka la rejareja anaambiwa unga ule ule Chapa sembe kilo ni 2000, mteja atarudi duka la jumla kununua unga kilo 1900 kuokoa shilling 100 tu iliyojaa kwenye shilling 2000 ya duka la rejareja
Mteja hata shilling 20/30/50 zina maana kubwa sana kwake wateja wengi hupenda sehemu yenye gharama nafuu, wateja wengi hupenda Bei za punguzo ili utoboe jua kucheza na akili za wateja wako uza Bei zinazoendana na washindani wako au uza chini ya Bei yao Ila hakikisha haupati hasara
Ila ukiuza km umefungua supermarket mtaani basi utafunga biashara mda sio mrefu maana wateja wa mtaani wanazijua Bei kuliko wewe mwenye bidhaa zako unaeuza, kitu cha 800 unauza 1000 mteja anakuhama anaenda wanapouza 800 kitu kile kile na maisha yanaenda anachofanya ni kwenda kuokoa 200 tu ambayo atanunua kitu kingine hata Kitunguu Saumu atafune, kwa hio jiongoze hapo utapata wateja ukiweka Bei zako za bidhaa sawa sawia
Na mbaya zaidi usichokijua wateja wana kawaida ya kuambizana duka lenye unafuu na duka lenye kutoa huduma bora, utasikia mama anamwambia mwanae nakutuma kitu fulani usiende kununua duka fulani anapunja nenda kwa fulani, na km mtoto akikosea akaja kununua kwako akaulizwa umenunua wapi akitaja ataambiwa rudisha sijakutuma huko Mimi huyu anapunja au anauza Bei juu, sasa km wamama wanavyowaambia watoto wao ndivyo wengine wanavyoambizana kua pale usiende Bei zake sio rafiki au huduma zake sio rafiki, ushaelewa?
Last thing but it is not the end of this essay, wanasema kwa kimombo if you can't smile then don't open a shop, yaan km huwezi kutabasamu usifungue duka, mteja anahitaji tabadamu lako usihudumie mteja ingali umenuna,
Kingine ni jinsi ya kua sharp unapohudumia wateja, wateja wengi hupenda mtu ambae yupo sharp ukimwambia nahitaji kitu fulani anakupa kwa haraka zaidi na kwa wakati au anaweza kubaini unachopenda na unachohitaji kwa kuonyesha hiki au hiki anapoint pale mteja anapotaka sio kusuasua hauijui bidhaa mteja anayoihitaji hapo utapuyanga
Bila kusahau wateja wanapenda uwe msafi sio umetoka kuchota mafuta ya taa hujapangusa mikono mafuta yamekumwagikia mikononi unaenda kuparamia unga au mchele unaanza kumpimia mtu wateja wanakuangalia usivyokua msafi au unampatia mteja Sigara mikono michafu hujanawa au mikono imeloana maji, my friend unakimbiza wateja maintain cleanliness kua msafi muda wote msafi wa mwili muonekano nadhifu na msafi wa ofisi yako na usafi wa huduma unayotoa jua kuelewa kipi kianze na kipi kifuate usikosee step hata moja ukikosea tu mteja kapotea harudi tena
Cha muhimu na Cha kuzingatia zaidi lugha na facial expressions, hivyo vitu viwili lugha yako kwa wateja iwe lugha rafiki iliyochangamka kuendana na eneo husika sifia mteja karibisha mteja mpokee mteja msikilize mteja mhudumie mteja kwa bashasha na kwa kumzingatia, fuata utaratibu hudumia waliotangulia kwanza kisha waliofuatia, usitumie lugha chafu jua kuongea na kila rika watoto hadi wazee masista duu, mabishoo wa kikongo, mabitozi, wagaigai na wahuni jua kuongea nao maana wote hao ni wateja wako, mapadrii makasisi wachungaji na mashehe jua kuongea nao maana wote hao ni wateja wako, kuna makapuku ambao wanakupiga mikopo ya 100 100 usiwakalipie na kuwadharau jua jinsi ya kuongea nao,
Hata km umeudhiwa usikunje sura kukasirika Ila usiruhusu mtu aichezee biashara yako furahi na kila mteja na mhudumie kila mteja kwa wakati na sikio sikivu na kwa umakini mpe kile mteja anachokihitaji kwa wakati usimpotezee muda mteja wako, hudumia mteja mmoja baada ya mwingine usihudumie wateja wawili au watatu kwa wakati mmoja utajichanganya na utapata hasara,
Pia mteja anapenda muuzaji anaeweza kumshauri juu ya kutumia kitu fulani au bidhaa fulani na kuipigia promotion bidhaa fulani kisha mteja anainunua pale pale au unaizungumzia jinsi unavyoitambua bidhaa unayoiuza hivyo pia mteja anapenda maana huoni unauza kitu ambacho hata wewe pia unakitumia na akitumia anakua na amani zaidi km kitakua na mrejesho chanya basi utakua umepata mteja wa kudumu maana atarudi na atarudi na atarudi na atawaalika na wengine waje kununua kwako
Mfano unauza Mo Energy na Azam Energy onyesha kuna tofauti ipi iliyopo kati ya hizo bidhaa mbili sio unauza tu mwambie mteja ukinywa Mo Energy kisha ukatafuna meno unahisi meno yako yanasagika Ila Azam Energy ukinywa hauhisi hivyo kwa hio kwa kukushauri mteja wangu tumia Azam Energy, hapo mteja atakuona wewe ni bonge la Genius unauza Ila pia unazijua bidhaa unazouza hauuzi uzi tu
Cha mwisho sio Cha muhimu km ukiona muhimu ni wewe, Jenga Urafiki na wateja Ila sio Urafiki uliopitiliza au kwa lugha nyingine Urafiki wa mikopo usijenge Urafiki wa kukopesha wateja wateja wengine hukimbia madeni kwa hio jua jinsi ya kuzuia kukopesha wateja, na pia jifunze kutoka kwa wateja kuna wateja wanazijua bidhaa unazouza wanaweza wakakupa 123 na abc kuhusu bidhaa Z Y na X km ukiwauliza na wakawa wanazifahamu kuna kaelimu ka uongo na ukweli watakupatia kwamba sabuni hii nikifulia mimi inanichubua mikono au nikifulia haitoi povu kwa hio ukiona sabuni hazitoki utajua tatizo wateja washalijua na watakupa alternative tuletee sabuni fulani zinatoa povu jingi au hazichubui mikono na maelezo mengine kwa hio unakua umejifunza kutoka kwa wateja wako na unawalete bidhaa wanayohitaji usilete bidhaa isiyohitajika na wateja
Na marufuku marufuku marufuku nasisitiza tena kwa mkazo wa hali ya juu maana hili linawaumiza sana wateja wako na wengine utawakimbiza bila kujijua kwamwe usiuze HAKUNA yaan mtu anakuja anakwambia nahitaji vocha ya 500 unamwambia HAKUNA au anakuambia nahitaji sabuni fulani ya mche, ya kipande au ya unga unajibu HAKUNA, pumbavu sasa si ufunge duka mwehu wewe hivi ni nani yupo tayari kuja kila siku kununua kwenye HAKUNA hata kikiwepo?
Jibu nimeagiza mzigo unakuja ukija baadae utaikuta bidhaa yako, hapo utajenga uaminifu kwa mteja na kujenga uaminifu zaidi agiza stock ya mzigo anaoutaka mteja ili mteja akija baadae bidhaa aikute sio akute HAKUNA, kamwe usiuze HAKUNA yaan unamuuzia HAKUNA wewe utakua ni mwehu na mteja atakukimbia atakuhama
Weka mazaga yote hadi wateja wakija washangae kuanzia bidhaa za watoto pipi biscuits mpaka bidhaa za vikongwe dawa ya mbu na asali mbichi,
Hakikisha duka lako halikosi bidhaa muhimu km kiberiti sasa duka eti halina kiberiti ambacho box 1 lina packets 10 kwa 500 (ambapo wewe utauza kiberiti kimoja 100) ukizidisha 100×10=1000 faida 500 alafu eti dukani huna kiberiti si ufunge duka tu unauza nini sasa hapo wakati hauna bidhaa?
Hakikisha duka lako limeshona likashiba likajaa usiwe na duka lenye njaa baskeli ya miti mbavu za mbwa yaan utaonekana njaa na duka lako njaa umekaa kinjaa njaa tu na utawaambukiza wateja njaa zako, emu jaza takataka zote zinazohitajika na binadamu yoyote uza hadi mifagio ya ndani nje kila uchafu wa bidhaa zinazopendwa na kuhitajika na watu tena vile vidogo vidogo ndio uwe navyo vya kutosha maana testing huanza kwenye vitu vidogo vidogo una chumvi utasikia hapana chumvi hamna, shenzi type sasa si ufunge duka unakosaje chumvi dukani?
SteshenariDesign namna ya kufanya matangazo dhidi ya biashara yako, na kutafuta soko. Ila inategemea na biashara maana hujaweka wazi ni biashara gani.
Tumia muda mrefu kusoma na kupekua mitandaoni ubunifu na mambo kadha wa kadha kuhusu biashara. Utafanikiwa tu ukiwa na uvumilivu pia!
Kuwa na subra na fuata ushauri hapo tafadhali. Usikate tamaa mapema!Steshenari