Ukiwa kijana wa kiume jifunze kuishi kama baba kabla ujafikia majukumu

Ukiwa kijana wa kiume jifunze kuishi kama baba kabla ujafikia majukumu

Ni kweli. Mimi kwa upande wangu ni jambo ambalo nilijifunza toka kwa baba yangu. Yeye ana utaratibu hata akirudi saa ngapi za usiku, lazima apite mabandani na kuizunguka nyumba kisha akiingia ndani lazima amuulizie mmoja baada ya mwingine, flani yupo? Kama kuna lolote ataambiwa.


Ni utaratibu mzuri sana.
 
Muhimu sana...umenifanya nmkumbuke mshua..kabla ya kulala lazima azunguke mazingira yote ya nyumba..kuhakikisha kila kitu kipo sawa..mabandani, zizini na kuhakikisha kila kitu kipo ndani..na kuhakikisha milango yote imefungwa vizuri.

Great Father

#MaendeleoHayanaChama.
 
Aisee unataka kujifunza kuishi kama baba sawa ila pia usisahau kutafuta na mwenzi atakaye kupa hiyo nafasi baadae.Naogopa usijefanywa kama mama wa nyumba kama ni mke mbabe na anajua kucheza namba yake.
 
hilo neno “uliyechangamka “ nimecheka sana,kuna mtu humu alisema mzee cheyo ni polepole aliyechangamka
anyway nimekuelewa ujumbe wako mkuu nikiwa kama kijana
Tupo pamoja mkuu🤝
 
najifunza kwa baba jinsi ya kuishi na mke.maana mamazetu hukaa kutujaza sumu kwamba baba zetu wanawatesa sana!!kumbe midomo yao na chokochoko zisizoisha ndio sababu
Ndio kawaida ya akina mama mkuu, watoto wakiwa wadogo wenu...wakianza kukua anawapa sumu na kujidai alipambana mwenyewe! Mim wa mwisho kwa familia yetu,mama alijaribu hizo attempts japo anaweka kama mazungumzo ya kawaida, kwangu aligonga mwamba,naenda kuwatembelea namjaza mshua hela, afu nampa na yeye kwa siri, nikitaka kuondoka naacha 50 hadharani..bas kila mtu anakua happy na kuona ameshinda, lakin kiuhalisia nlikua nahalikisha mzee anapata hela nyingi! Umiliki wa mali na watoto daima ndio azma ya mwanamke yyte na umiliki ndio maumbile ya kike! Ndio maana mara chache sana mama mkwe na mke wa mwanae kuelewana inakua shida kwa kuwa wote wanahangaikia umiliki!

Sent from my SM-N910U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom