Ukiwa kiongozi wa umma wewe ni mtumishi wetu pokea Simu za Wananchi wako

Kikwava

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2015
Posts
1,741
Reaction score
1,068
Sijui Ni desturi yetu sisi waafrica. Unakuta kiongozi hapokei simu na ukizingatia kabla ya uteuzi au kuwa kiongozi simu alikuwa anapokea Ila baada tu ya kuwa kiongozi simu hapokei.

Viongozi wetu ukiwa mbunge, waziri, DC, RC, au naibu waziri, tunaomba simu ikiita hata Kama huna muda kwa wakati huo Basi ukipata nafasi wapigie waulize walikuwa wanasemaje, utabarikiwa Sana na Mungu.

Kutokupokea simu kunamfanya mtu kwenda kwenye ngazi ya juu zaidi kutoa malalamiko yake ambapo kutakufanya wewe kiongozi ambaye hukupokea simu uonekane huwajibiki kwenye nafasi yako.

Soma Pia: Maxence Melo: Kiongozi ukishakuwa kwenye ofisi ya umma kukosolewa ni haki yako

Nitumie fursa hii pia kuwapongeza viongozi wetu wote ambao wamekuwa wakipokea simu zetu Mara tupigapo kwasabu kupokea simu zetu sisi Wananchi ni kumuwakilisha vema Mh. Rais.
 
Kwa watu gani? Hawa hawa watanzania wanywa gongo? Siungi mkono hoja.
Sawa usiunge mkono lakini jua mwsho wa siku utaonekana kiongoz dhaifu, kwasabu kila Jambo litakuwa linareportiwa juu huku ww
 
Kwa watu gani? Hawa hawa watanzania wanywa gongo? Siungi mkono hoja.
Wengine tunawapigia simu zinaita zinakata Wala hawajari hata kusema nitumie meseji tu hamna sijui huwa ni irresponsibility au dharau
 
Kwa watu gani? Hawa hawa watanzania wanywa gongo? Siungi mkono hoja.
Wengine tunawapigia simu zinaita zinakata Wala hawajari hata kusema nitumie meseji tu hamna sijui huwa ni irresponsibility au
 
Sijui Ni desturi yetu sisi waafrica. Unakuta kiongozi hapokei simu na ukizingatia kabla ya uteuzi au kuwa kiongozi simu alikuwa anapokea Ila baada tu ya kuwa kiongozi simu hapokei.

Viongozi wetu ukiwa mbunge, waziri, DC, RC, au naibu waziri, tunaomba simu ikiita hata Kama huna muda kwa wakati huo Basi ukipata nafasi wapigie waulize walikuwa wanasemaje, utabarikiwa Sana na Mungu.

Kutokupokea simu kunamfanya mtu kwenda kwenye ngazi ya juu zaidi kutoa malalamiko yake ambapo kutakufanya wewe kiongozi ambaye hukupokea simu uonekane huwajibiki kwenye nafasi yako.

Soma Pia: Maxence Melo: Kiongozi ukishakuwa kwenye ofisi ya umma kukosolewa ni haki yako

Nitumie fursa hii pia kuwapongeza viongozi wetu wote ambao wamekuwa wakipokea simu zetu Mara tupigapo kwasabu kupokea simu zetu sisi Wananchi ni kumuwakilisha vema Mh. Rais.
huenda nimetingwa na majukumu,

nitumie ujumbe tu ndugu mwananchi ukieleza kinagaubaga jambo mahususi unalokusudia kunishirikisha. Nikipunguza majukumu haya mazito yalonitinga, kwa wakati muafaka nitakujibu na huenda nikakupigia ikiwa muda unaruhusu...

hakuna dharau, majivuno wala mabadiliko katika kupokea simu, ni majukumu tu, usichoke wala kukata tamaa kunitafuta 🐒
 
Kuna viongozi ukiwapigia simu hawapokei wanaicheki tu sijui huwa ni dharau,
Walishatuovarate raia wote kuwa sisi ni njaa kali, ombaomba na kila simu kwao huhisi ni ya kutaka waombwe ama kutolewa shida.

Ndiyo saikolojia yao ilipigotea huko.
 
Back
Top Bottom