Jifunze kuhesabu umri wa mimba/ujauzito wa mkeo kwa wiki na sio miezi
Mtoto aliyeko tumboni huanza kugeuka (kutanguliza kichwa chini) akiw na wiki 28... hii huitwa cephalic presentation... mtoto huishi akiwa katika mkao huu/huo hadi anapofikisha umri wa kuzaliwa.
Wapo watoto wanaochelewa kugeuka hadi wiki 34 then baada ya umri huo kugeuka huwa ni miujiza tu. Hii ni kutokana na ukubwa wa mtoto ambao hufanya room ya yeye kujigeuzageuza kuwa ndogo
Ikiwa majibu ya ultrasound yanaonesha umri chini ya wiki 28 basi hoja ya kugeuka ama kutogeuka huwa inakosa nguvu maana kipindi hicho mtoto anakuwa na mijongeo (movements) mingi tumboni... yaani anajigeuzageuza tu atakavyo