Zero Competition
JF-Expert Member
- Sep 12, 2018
- 347
- 553
Sekta binafsi ndo inaongoza kwa kutoa ajira nchini na hata duniani kote lakini ukiwa muajiriwa wa sekta binafsi amini kwamba kesho asubuhi unaweza amka ukaenda ofisini kisha ukakuta barua yako ya kuachishwa kazi iko mezani inakusubiri
Jambo lingine ni kwamba ukiwa muajiriwa wa sekta binafsi muda wote unakua na wasiwasi na unakosa amani hasa pale ambapo mkataba wako unaelekea kutamatika mana kuna baadhi ya mashirika na makampuni mkataba wako ukiisha unakua huna uhakika wa kuongezewa mwingine.
Kuna rafiki yangu flani yeye anafanya kwenye shirika moja la kimataifa linalojihusisha na masuala ya afya, huyu rafiki yangu aliniambia kwenye shirika lao watu wanakua na presha sana pindi mikataba yao inapoelekea ukingoni mana uhakika wa kuongezewa mingine ni mdogo sana.
Kuna jamaa zetu wanafanya kazi private sector lakini wana maringo utadhani wana mkataba wa maisha, sisi watu kama hao huwa tunawasubiri mtaani mana tushafanya kazi na makampuni mbalimbali na tunajua changamoto za kufanya kazi sekta binafsi.
Kitu ninachotaka kuwashauri wanaofanya kazi sekta binafsi ni kwamba, muda wowote unaweza fukuzwa kazini au kampuni ikafungwa ghafla tu baada ya kujiendesha kwa hasara.Hapa sasa ndo utakumbuka kwamba kuna washkaji mtaani niliwahi kuwaletea nyodo na majivuno sijui nitawaambia nini.
Ukiwa kwenye ajira especially ya private sector jitahidi kuwaheshimu watu wote mana muda wowote unaweza amka huna kazi then ukashindwa kuwaomba watu msaada.