Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu, Udhamini wa m.bet uliosemwa na simba kuwa ni b.26 kwa miaka 5 inakuwaje wanapewa b.2.5 kwa mwaka?

Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu, Udhamini wa m.bet uliosemwa na simba kuwa ni b.26 kwa miaka 5 inakuwaje wanapewa b.2.5 kwa mwaka?

Sikushangai huelewi !Kwani akili za kuelewa na kuchanganua mada huna.Upo kwenye lile kundi la wasio na akili.Hata kufikia kuchaguliwa kiongozi.
 
Sasa hapo mbumbumbu ni nani ikiwa wewe mwenyewe umeshasema hujaelewa na tena ukaja na hitimisho la kuwaita Simba "Mbumbumbu"!!!
Badala ya kuishia tu kuwa huelewi hivyo uombe kuelewesha, wewe umeshahukumu tayari. Watu mnakwama wapi?
Unajua maana ya ripoti ya mapato na matumizi? Unajua tarehe ya kusainiwa kwa mkataba na fedha kuanza kuingizwa kwa ajili ya kuanza kutumika? Unajua modalities za kuingiza fedha kwenye timu? Maana kila mkataba una taratibu na makubaliano ya namna kuingiziwa fedha.

Na pengine huenda kukawa na error eidha ya matamshi au kiuandishi kati ya 2.5 na 5.2!! Yote yanawezekana.

Mimi siwatetei, Ila jaribu kuwa na subira kabla ya kulaumu au kuhukumu. Mihemko mibaya sana.
Au ni yale yale ya Haji Manara kuwa huko wenye akili ni wawili tu? NI SWALI TU usije ukahamaki.[emoji124][emoji124][emoji124]
Mkuu inawezekana kwenye 2.5b ukawa sawa kutokana na lini mkataba umesainiwa, lakini hapo kwenye matangazo ya Mo kidogo kuna maswali ambayo hayana majibu
 
Mkuu inawezekana kwenye 2.5b ukawa sawa kutokana na lini mkataba umesainiwa, lakini hapo kwenye matangazo ya Mo kidogo kuna maswali ambayo hayana majibu
Jaribu kuwaelewesha na wenzako.Kuhusu matangazo ya Mo anatoa pesa zaidi ya thamani ya hayo matangazo.Na ni mwekezaji.
Una swali nyingine?
 
Tatizo ni kweli hujaelewa. Mkataba ulisainiwa lini.Fiscal year iliyofanyiwa kufunga mahesabu ni July 2022 mpaka December 2022 kwa pesa ya mkataba wa M bet.Hivyo pesa zilizotolewa ni kwa nusu mwaka 2.5 bilioni.Nusu nyingine ni January to June 2023.
Sishangai wewe kutoelewa kwani Manara alishasema huko nyuma wenye akili huko upande mwingine ni baba yake mzazi na mzee Kikwete.
Sishangai.
Unaweza ukawa sahihi, au mleta mada akawa sahihi.
Tuanzie kwanza kwenye kauli ambayo imetolewa na mleta mada akinuu taarifa
Kauli yenyewe ni hii "udhamini wa m.bet ni b.2.5 kwa mwaka"
Binafsi sijabahatika kusikiliza namna uwasilishaji wa ripoti ulivyofanyika, hivyo naomba kujua je muwasilishaji alitamka kuwa udhamini wa M bet kwa mwaka ni b 2.5 ?
 
Nope.Hakutamka udhamini wa M Bet kwa mwaka ni 2.5 bilioni.
Hiyo ni tafsiri potofu ya mleta mada.
 
Nope.Hakutamka udhamini wa M Bet kwa mwaka ni 2.5 bilioni.
Hiyo ni tafsiri potofu ya mleta mada.
Sawa. Je ni kipi alichotamka hadi kutaja hiyo figure ya mapato?
 
Alitaja udhamini Mbet 2.5 bilioni .
Ilinibidi nitafute video ili nami nijue nini kilichosemwa naomba ninukuu

" Katika bajeti yetu mpya ambayo ni ya mwaka 2022/2023, katika kipengele cha kwanza tumeona katika sponsorship. Kwenye sponsorship tunatarajia kupata sh bilioni 3 milioni mia tisa sabini na tano, ambazo kwenye bilioni tatu hizi kuna M bet ambaye ndio main sponsor atatoa biliion 2 milioni mia tano na hamsimi. Huyo ndiyo mdhamini wetu mkuu"

Naomba niishie hapo.

1) Kwenye kauli hii kuna neno 2022/2023 maana yake hapo ni msimu mzima wa 2022/2023

2) kuna neno "tunatarajia kupata" maana yake imepigwa hesabu ya jumla kwa msimu mzima, ingekuwa ni bajeti iliyolenga hesabu ya nusu muhula basi kauli ingekuwa tumepata na sio tunatarajia.

Pitia video dakika ya 7:15 hadi 7:54

Msimu wa 22/23 unaanza lini na kuishia lini?Ungepata budget in details ndio ungeelewa.Mkataba wa MNet umesainiwa lini?Go deeper.
 
Msimu wa 22/23 unaanza lini na kuishia lini?Ungepata budget in details ndio ungeelewa.Mkataba wa MNet umesainiwa lini?Go deeper.
Na ndio maana hapo msoma ripoti kasema tunatarajia kupata na hakusema tumepata. Kama ingekuwa ni hesabu ya nusu mwaka maanake wangesoma kilichowekwa na m-bet na sio hadi kitakachokuja kupatikana mbeleni
 
Kuna siku nilisema uhalisia wa hii mikataba utakuja kuonekana sasa wameumbuka wenyewe, Yanga analamba b.4.11 kwa mwaka sport pesa kwa mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya b.12.33 na hii timu ya propaganda inalamba b.2.5 kwa mkataba wa miaka 5 wa m.bet wenye thamani ya b.12.5, Njia ya muongo siku zote ni fupi
Kwahiyo hao Yanga ndo wakweli sio... Halaf kuna jambo naona hapo mfungua uzi hajaliweka wazi kua kwa mwaka wa kwanza kuna kiasi kinalipwa kwa SSC kutoka kwa M-BET, na kitaendelea kuongezeka mpaka mwaka wa mwisho kulingana na mkataba na sio kama wengi wadhaniavyo kwa ni kuchukua jumla kuu (TShs B 26) gawia kwa muda wa mkataba (miaka 5) ambayo inikupa almost TShs B 5.2/Mwaka, nadhani hili liliwekwa hivi kutokana na mambo ya kibiashara zaidi (Yaani kulingana na ukuaji wa soko lilivyopigwa kimahesabu). Na ndicho kilichofanyika na kitaendelea kufanyika kulingana na mkataba.
 
Sikushangai huelewi !Kwani akili za kuelewa na kuchanganua mada huna.Upo kwenye lile kundi la wasio na akili.Hata kufikia kuchaguliwa kiongozi.
Nenda darasani wewe mbumbumbu ukajifunze namna ya kuandika kwa mpangilio?
 
Kuna siku nilisema uhalisia wa hii mikataba utakuja kuonekana sasa wameumbuka wenyewe, Yanga analamba b.4.11 kwa mwaka sport pesa kwa mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya b.12.33 na hii timu ya propaganda inalamba b.2.5 kwa mkataba wa miaka 5 wa m.bet wenye thamani ya b.12.5, Njia ya muongo siku zote ni fupi
Watasema "wanachoangalia ni matokeo ya uwanjani"! Maana hata zile bilioni 20 zenyewe tu ni kizungumkuti.
 
Utopolo kwenu kunauungua hamuoni.Mizengwe mpaka mchezaji anagoma nyie mmekalia kuirekebisha Simba.
Mgosi shamba la pears halitoi matunda mnakazia macho shamba la jirani.
Aliyewaloga nani?Migongowazi!
 
Labda mimi mwenyewe ndio sijaelewa vizuri leo wakati mapato na matumizi yakisomwa wanasema udhamini wa m.bet ni b.2.5 kwa mwaka ndiyo wanayopewa wakati thamani ya mkataba waliyowatangazia wanachama wao ni b.26, Sasa inakuwaje wanapewa b.2.5 kwa mwaka wakati walitakiwa wapewe b.5.2 kwa mwaka kwa mkataba wa miaka 5 waliyodhaminiwa? Kwa maana iyo walidanganya thamani halisi ya mkataba wao ambao ukipiga hesabu una thamani ya b.12.5 kwa miaka 5 kama wanapewa 2.5 b. Kila mwaka, Mzee Rage apewe heshima yake bwana maana neno "mbumbumbu" linaakisi mambo mengi sana
Inategemea na makubaliano ya kutoa pesa yalikuaje kama kwa miaka mitano ni bilioni 26 haimaanishi kwamba itatolewa sawa sawa kila mwaka kwaiyo tujue kwanza mkataba unasema pesa inatoka kwa ratio gani kila mwaka
 
Back
Top Bottom