Ukiwa mwanasiasa hakikisha unatenga muda wa kusoma na kuwaelewa wana falsafa wa enzi. Ni hitaji muhimu la maamuzi utakayofanya

Ukiwa mwanasiasa hakikisha unatenga muda wa kusoma na kuwaelewa wana falsafa wa enzi. Ni hitaji muhimu la maamuzi utakayofanya

Asikudanganye mtu hakuna chochote kigeni kwenye hii dunia. Mambo yanayotokea leo hii yalishakuwepo kwenye huu ulimwengu miaka maelfu kwa maelfu iliyopita.

Unaongelea kuhusu rushwa, chuki, wivu, ukatili, kulewa madaraka, magonjwa, mauaji etc etc yote utayakuta kwenye vitabu vitakatifu na ni vitu vilikuwa vinatokea kwenye karne zote za ulimwengu huu.

Maana yake, matukio yote ya sasa kwenye maisha tunayoishi, asilimia kubwa ni marudio tu ya mambo yaliyokwisha kutokea zama za nyuma.

Lakini kuna kitu kimoja watu huwa wanakipuuza, katika zama za enzi zilizopita, kumebarikiwa kuwa na watu wenye akili ambazo ni vigumu sana kuzipata kwenye watu wa dunia ya sasa ya kidigitali.

Maana yake ni kwamba Ukitaka kujifunza chochote kwenye ulimwengu wa sasa, fanya kurejelewa maandiko ya wanafalsafa wa miaka ya zamani. Na huko ndiko busara hupatikana.

Ni kwanini, leo watu wanamuimba Nyerere ni kiongozi bora, ni simply kwa sababu nyerere alikuwa msomi mzuri wa falsafa.

Hakuna mtu anayezijua vema falasafa, akachukua kiboko akamtandika mwenzake hadharani. Ukisoma vema falsafa, utakutana na maandiko ambayo daima yatakufanya uwe mtu mwema sana kwenye jamii, na mtu mwenye mawazo mema na ya busara.

Juzi kati hapa nilikuwa namsoma mwanafalsafa mmoja anaitwa 'Rene Deskates' kuna quote yake moja inasema "Greatest minds are capable of greatest vices and virtues" kwa kiswahili ni kwamba, ' Watu wenye uwezo mkubwa wa kiakili wana uwezo wa kufanya matendo mema na pia wanauwezo wa kufanya ukatili wa kutisha.

Mstari kama huo hapo juu unaweza kumfanya kiongozi kuwa mpole sana wakati wote anapo deal na raia wake, maana huwezi jua huyo unayemnyanyulia fimbo kumchapa ni mtu wa aina gani na anauwezo wa kukufanya kitu gani.

Mambo kama hayo, yenye ufanano huo. Ni kukumbushana tu. Kuzijua falsafa ni kitu cha lazima sana kwa viongozi na wote ambao wana deal sana na jamii.

Wanafalsafa wenyewe ni wale kama kina Plato, Aristotle, soma Bible pia, Quran, Karl Max, wapo mamia kwa mamia, just tenga mda uwe unawasoma hao watu.

Kuna saa huwa nakaa natafakari, najisemea mwenyewe, watu kama kina Magufuli, Makonda, Sabaya na wengineyo, wangekuwa ni viongozi bora sana ikiwa wangezifahamu vyema falsafa.

Hakuna mwanafalsafa atayekushauri kufanya mabovu waliyofanya. Hakuna.

Nahisi kama ingekuwa ni amri yangu, qualification ya kuwa mwanasiasa, ingepaswa kwanza iwe mtu una degree ama cheti cha kwamba umesoma falsafa.

Ni hayo tu.
N. Mushi
Wanasiasa wengi uwezo wao wa kiakili ni mdogo sana matokeo yake hufanya maamuzi yanayowadhuru wananchi ' incompetent leaders act like strong leaders' they make decisions which affect livelihood of citizens
 
Wanasiasa wengi uwezo wao wa kiakili ni mdogo sana matokeo yake hufanya maamuzi yanayowadhuru wananchi ' incompetent leaders act like strong leaders' they make decisions which affect livelihood of citizens
Hiyo nakubali kabisa.. ndo mana tunajaribu kutibu ugonjwa kwa kuwashauri.
 
Back
Top Bottom