NDIYO. Wewe haikubali kwa sababu moja au nyingine imekataliwa, solve kwanza hilo. Mimi niliunga sku nyingi mno, tena ikuwa mpaka ujaze form benki, nilifanya hivo nikawa natumia kununua tu. Baadae kuna biashara nikawa nafanya, ikawa changamoto kupokea pesa, paypal wakasema tatizo ni BOT hawajaruhusu kitu kama hicho kwa Tanzania. Lakini baadae nadhani ilikuwa mwaka jana mwanzoni ikawa imekubalika, tena crdb walitangaza sana tu. Benki nyingine karbia zote hazina complications za kujaza forms, kama una master au visa card ya benki nyingine yoyote jaribu kulink uone mkuu, mimi natumia card zangu za benki nyingine bila shida. Challenge yako ya kwanza kabisa kwasasa na kulink akaunti card yako na paypal, tatua hiyo kwanza, hakikisha akaunti yako ya benki ina pesa kiasi, kwa mara ya kwanza huwa wanakata pesa baadae wanairudisha.