KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kama hili halipo basi ni hatari sana na pengine wamechelewa tu kunganisha. Kwenye mikopo, inatakiwa system iliyokuwa intergrated, yaani ukitaka kukopa institution A, wawe na uwezo wa kuona kama umeshakopa au una mkopo sehemu nyingine zote zinazokopesha. Bila kuwa na uwezekano wa namna hii, mtu mmoja anaweza kukopa sehemu nyingi na akakimbia na fedha. Ndiyo maana nchi zilizoendelea kuna kitu kinaitwa credit rating, yaani ni namna ya kuonyesha mkopaji ni mtu wa aina gani, ana mikopo mingi? Ana tabia ya kulipa madeni?
Ni jambo zuri Kwa Ulinzi wa mitaji ya Mabenki na Taasisi za kifedha

Kwenye upande wa Mikopo ya Benki, tayari mifuko inasomana

Nadhani tunapoelekea ni Pazuri zaidi
 
Aaagh wapi kuna mahali walisema hivyo wakati wanakukopesha au hujui kuna haki ya mkopiaji pia?
Songesha ni brand name ya taasisi ya tanzu ya fedha iliyosajiliwa Benki kuu yaani Microfinance

Wamesajiliwa Benki kuu Hao .Ukikopa taarifa zako zinaenda kwenye Credit bureau ya nchi inayohifadhi record za wakopaji

Wewe unapokopa unakopa ujue unakopa kwenye taasisi ya kifedha iliyosajiliwa Benki kuu kama ulikuwa hujui.Hawakopeshi kienyeji

Wewe ulidhani songesha ni wahuni wa mitaani unaweza kuwakopa na kujifanya mjanya wa mjini na kutokomea mitini na pesa yao
 
Mwigulu Nchemba alishasema hatambui kampuni za simu kukopesha wateja.. 😁
Na kampuni za simu hazikopeshi fedha Bali Kuna kampuni za kukopesha fedha zinazotumia mitandao ya simu

Kampuni za Simu zinakopesha Salio la vocha tu
 
Kwa maana hiyo ulikuwa unadaiwa Songesha ila hutaki kuwalipa Vodacom . Badala yake ukaenda kukopa kwingineko ili nao usiwalipe.

Kama ambavyo Vodacom wameshauri wakopeshaji wenzao wasikukopeshe maana una udhaifu wa kutolipa deni.

Ina maana Songesha walikukopesha hela bila wewe kukubali?

Hukuwa umeomba, au uliomba ila "haukukubali"?

Hela hiyo uliyosongobekwa kwa lazima ulitumia au hukutumia?
Iko hivi mikopo ya mitamdao ya simu inatolewa kutoka benki fulani.

Tigo- CRDB (kama sikakosea)
Airtel -(baclays zamani sijajua kwa sasa kama wako na ABSA)

Voda -FINCA microfinance/TCB
 
Ndio,ukiwa na mkopo ukapitisha siku Moja unapelekwa Kwenye mamlaka ya wadaiwa sugu unakoswa sifa za kukopa bank
Hahahaha..............hatari 😅

Kuna watu Wana mtindo wa kukopa na kuvunja laini zao za simu

Unakuta mtu Kila baada ya wiki Moja analaini nyingine ya Simu 🙌
 
Nilidhani hiyo Mikopo ya mitandao ya Simu ni mitaji ya Kampuni husika za simu
Mfano tu cheki maelezo ya Songesha kutoka kwenye site ya Vodacom tz.
 

Attachments

  • Screenshot_20240524_180153_Chrome.jpg
    Screenshot_20240524_180153_Chrome.jpg
    79.8 KB · Views: 28
Hahahaha..............hatari 😅

Kuna watu Wana mtindo wa kukopa na kuvunja laini zao za simu

Unakuta mtu Kila baada ya wiki Moja analaini nyingine ya Simu 🙌
Record hazipitei Sababu alisajili Kwa Namba ya NIDA deni litabako na kukukua siku akienda Benki hakopesheki na siku wakimuibukia Waweza Nadi Mali zake kwenye mnada Sababu deni linazidi kukukua na riba
 
Naona watuwa wa Finca mmejikusanya kuja tutisha raia humu. Raia washavunja laini.
Kifupi benki yeyote hutakopesheka si ulisajili laini Kwa kitambulisho cha taifa .Unadhani rekodi zako zitapotea hata ukienda kukopa popote watakudai kitambulisho Cha taifa wakiingizia tu huyu hapa wanakuona tapeli wa kukopa alishakopa kabla akiingia mitini
 
Back
Top Bottom