KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Songesha na mikopo mingine ya simu imepelekea watumishi kunyimwa mikopo wanapoenda bank kukopa, na hii ni kutokana na mamlaka zinazosimamia mikopo kuweka utaratibu wa madaraja high risk, risk na low risk katika kadiri mteja anaposongesha.

Hilo limetokea leo mimi mwenyewe nilipoenda bank na kuingia kwenye mfumo wa ESS Utumishi, bank walivyoingia na kutumia mkopo ukawa rejected, nikaenda Voda nikawalipa Songesha yote lakini bado mfumo ulisoma high risk.

Nawashauri wale ambao hamjaingia kwenye hili jini songesha msijaribu, mbeleni litawaleta shida.

Mamlaka zinasimamia Mikopo hili la simu hasa mikopo ya Nivushe, Songesha, Gold, Bustisha ziwe na term of condition, yaani taratibu za mwanachama kukubali.
Dawa ya deni ni kulipa tu, kulalama hakujawahi kuwa suluhisho.
 
Huku kwetu Rwanda hata kama una deni la maji unawekwa CRB na mkopo huezi kupata sehemu yotote kwa hio siku hizi ni kulipa madeni yako yote hata ya songesha kwa kua iko regulatated na Central bank
Mmmmmmhmn wakileta huu mfumo Tanzania watu hawatakopesheka.
 
Kuna mtu juzi kanikopa laki tano 500000/= anadai TIMIZA mpaka jana hawajamkopesha na hawamdai na ana rekodi nzuri ya kuwalipa mimi nikampa ila mpaka leo anasema TIMIZA hawajampa hela.
Hao timiza ni Bank hao ujue, ukiwakopa ulipe mzee. Wanakuripoti.
 
Boss, huu ujanja ni suala la muda tu utakomeshwa na mifumo. Itafika kipindi jina likiandikwa IFAC mpaka bili za hospitali zilizokimbiwa zinaonekana. Sasa hivi bado Saccos na Microfinance uchwara ndo hazijawa link na CRB, ila huko mbeleni ukikopa utalipa tu au hutokopa tena.
hii imenikuta mama huwa anakopa sana vision fund mm na mdogo wake ndio wathamini wake sasa mkopo umeisha ammenda kukopa tena wamemkatilia sababu wadhamini tunamadeni songesha mgodi na mpawa Loan officer kasema mpk tulipe madeni yote ndio atapewa mkopo.so hii ishu ipo serious
 
nadhani hii itasaidia na watu kutoingia kwenye mikopo ya mabenki wahamie saccos kwenye riba nafuu safi kabisa
 
vinahusiana sana ata mm ishanikuta
Juzi niliongea na rafiki yangu mmoja wa Mikopo pale NMB amenieleza kuhusu hili

Watu wajitahidi kulipa Mikopo yao ya Simu kabla hawajaomba ya Benki, otherwise hawawezi kupata
 
Back
Top Bottom