Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Wandugu utu uzima dawa.. Hebu tushauriane kitu kwenye hili la mishe za kutafuta shilingi
Ajira hakuna na changamoto za maisha ni nyingi sana.. Kila kitu ni hela hasa kwa sisi tunaoishi mijini.. Hata kikombe cha maji ni pesa achilia mbali chakula.. Mjini hakuna cha bure! Sasa hata kama hakuna ajira lakini ajira ndogondogo za kujiajiri na kupata chochote hazikosekani...! Ajira zisizohitaji leseni, chumba cha biashara wala kodi ya mwezi na msaidizi..!
Natambua wengi wamekata tamaa na biashara ama wanaogopa kuingia huko kutokana na mlolongo mrefu wa nyaraka na tozo na kodi za kila aina.. Yaani kwa sasa ukiwa na million moja hiyo pesa inaweza kuishia kwenye hayo mambo..sasa ufanyeje ili pesa yako ya msingi ibaki na izalishe chochote?
Mchawi wa hilo uko kwenye 'WASTE' kuanzia
Mifuko ya kila aina
Chuma cha kila aina
Plastiki za kila aina
Mabox ya kila aina
Makaratasi ya kila aina
Chupa za kila aina
Matairi ya kila aina
Oil chafu za kila aina nknk
Kuna pesa huku kwenye waste.. Na unaweza kufika mahali ikawa ni ajira yako rasmi...kuna biashara ya chapchap na pesa yake ni hapo hapo.. Uwekezajia ni mdogo kulingana na uwezoa lakini faida unaiona hapo hapo
Unachotakiwa kufanya ninini?
Wakati wako wa kujiajiri ni sasa..! Mwenzako anapodamka kwenda kuomba kazi sehemu mbali mbali... Wewe damka upite kwenye masoko makubwa wanakopokea na kusafirisha bidhaa sehemu mbali mbali za nchi.. Huko angalia vifungashio tuu, bei zake na upatikanaji wake .. Ziara hii ifanye kwa siku nzima
Siku ya pili damka nenda maeneo ulikoambiwa vufungashio vipatatikana.. Cheki bei zake na upatikanaji wake..hii ziara ya siku ya pili ifanye kwa siku nzima pia
Siku ya tatu damka nenda viwandani .. Angalia wanatengeneza nini na wanatupa nini.. Huko dili na watu wa 'waste' tuuu.. Watakwambia kitu gani kinauzwa wapi na wateja ni akina nani... Hii unaweza kuifanya kwa siku tatu hivi
Kwa siku tano za wiki ikifika Ijumaa jioni utajikuta sio wewe uliyeanza wiki ukiwa hujui hayo yote..hii inaitwa elimu mitaani.com.. Kuanzia hapo anza kutafuta oda ndogondogo kwa mtaji wako.. Ukiwa mtulivu na maono baada ya mwezi utajikuta umetengeneza faida kubwa kuliko hata aliyeajiriwa...!