Ukiwa na mtaji mdogo ufanyeje ili upate faida?

Ukiwa na mtaji mdogo ufanyeje ili upate faida?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Wandugu utu uzima dawa.. Hebu tushauriane kitu kwenye hili la mishe za kutafuta shilingi

Ajira hakuna na changamoto za maisha ni nyingi sana.. Kila kitu ni hela hasa kwa sisi tunaoishi mijini.. Hata kikombe cha maji ni pesa achilia mbali chakula.. Mjini hakuna cha bure! Sasa hata kama hakuna ajira lakini ajira ndogondogo za kujiajiri na kupata chochote hazikosekani...! Ajira zisizohitaji leseni, chumba cha biashara wala kodi ya mwezi na msaidizi..!

Natambua wengi wamekata tamaa na biashara ama wanaogopa kuingia huko kutokana na mlolongo mrefu wa nyaraka na tozo na kodi za kila aina.. Yaani kwa sasa ukiwa na million moja hiyo pesa inaweza kuishia kwenye hayo mambo..sasa ufanyeje ili pesa yako ya msingi ibaki na izalishe chochote?

Mchawi wa hilo uko kwenye 'WASTE' kuanzia
Mifuko ya kila aina
Chuma cha kila aina
Plastiki za kila aina
Mabox ya kila aina
Makaratasi ya kila aina
Chupa za kila aina
Matairi ya kila aina
Oil chafu za kila aina nknk

Kuna pesa huku kwenye waste.. Na unaweza kufika mahali ikawa ni ajira yako rasmi...kuna biashara ya chapchap na pesa yake ni hapo hapo.. Uwekezajia ni mdogo kulingana na uwezoa lakini faida unaiona hapo hapo

Unachotakiwa kufanya ninini?
Wakati wako wa kujiajiri ni sasa..! Mwenzako anapodamka kwenda kuomba kazi sehemu mbali mbali... Wewe damka upite kwenye masoko makubwa wanakopokea na kusafirisha bidhaa sehemu mbali mbali za nchi.. Huko angalia vifungashio tuu, bei zake na upatikanaji wake .. Ziara hii ifanye kwa siku nzima

Siku ya pili damka nenda maeneo ulikoambiwa vufungashio vipatatikana.. Cheki bei zake na upatikanaji wake..hii ziara ya siku ya pili ifanye kwa siku nzima pia
Siku ya tatu damka nenda viwandani .. Angalia wanatengeneza nini na wanatupa nini.. Huko dili na watu wa 'waste' tuuu.. Watakwambia kitu gani kinauzwa wapi na wateja ni akina nani... Hii unaweza kuifanya kwa siku tatu hivi

Kwa siku tano za wiki ikifika Ijumaa jioni utajikuta sio wewe uliyeanza wiki ukiwa hujui hayo yote..hii inaitwa elimu mitaani.com.. Kuanzia hapo anza kutafuta oda ndogondogo kwa mtaji wako.. Ukiwa mtulivu na maono baada ya mwezi utajikuta umetengeneza faida kubwa kuliko hata aliyeajiriwa...!
 
Wandugu utu uzima dawa.. Hebu tushauriane kitu kwenye hili la mishe za kutafuta shilingi

Ajira hakuna na changamoto za maisha ni nyingi sana.. Kila kitu ni hela hasa kwa sisi tunaoishi

Siku ya pili damka nenda maeneo ulikoambiwa vufungashio vipatatikana.. Cheki bei zake na upatikanaji wake..hii ziara ya siku ya pili ifanye kwa siku nzima pia
Siku ya tatu damka nenda viwandani .. Angalia wanatengeneza nini na wanatupa nini.. Huko dili na watu wa 'waste' tuuu.. Watakwambia kitu gani kinauzwa wapi na wateja ni akina nani... Hii unaweza kuifanya kwa siku tatu hivi

Kwa siku tano za wiki ikifika Ijumaa jioni utajikuta sio wewe uliyeanza wiki ukiwa hujui hayo yote..hii inaitwa elimu mitaani.com.. Kuanzia hapo anza kutafuta oda ndogondogo kwa mtaji wako.. Ukiwa mtulivu na maono baada ya mwezi utajikuta umetengeneza faida kubwa kuliko hata aliyeajiriwa...!

Wabongo walivyo wabinafsi unaweza shangaa ukapewa majibu ya mkato mkato
 
Bro kwa mimi niliyepo Arusha ile biashara ya matairi naweza kuifanya?
Tena kuna mzigo mkubwa huko wa kamba na mabaki ya tairi naambiwa unafika tani 12 utafute nikupe shavu.. Mitaa ya Kijenge hivi
 
Tena kuna mzigo mkubwa huko wa kamba na mabaki ya tairi naambiwa unafika tani 12 utafute nikupe shavu.. Mitaa ya Kijenge hivi
Shukrani bro soon ntakupa feedback, na je hizo tairi unanunua kwa kilo au kwa mfumo upi? na kuna vigezo vyovyote kwenye ubora wa tairi? au ilimradi tu ziwe tairi used
 
Biashara ya taka Mali ukiiangalia Kwa nje unaweza hisi watu wanapoteza muda, lakn binafsi imenifanya nikabadili mindset yangu Kwa muda mfupi sana.

Changamoto zipo tena sana lakini zinakuwa solved mapema ukilinganisha na zile za leseni na tin namba.

Vyuma chakavu ni biashara inayohitaji mtaji na connection pia mana hio inatolewa macho sana na serikali, kuswekwa ndani kama mhujumu uchumi ni kufumba na kufumbua.

Plastic, chupa, pamoja na mifuko ni salama zaidi.
Hivi ukiwa na mtaji kidogo unaweza kuanza changamoto yake ni ukuaji wa mtaji unachukua mda mrefu kulingana na upatikanaji wa material, cost za usafiri.

Nb: Tujifunze kujaribu vitu na tusichague kazi.
 
Back
Top Bottom