UNA NI NINI UNACHOMILIKI SASA HIVI ?!
Kwa ufupi, Mungu kila kiumbe chake amekipa mtaji wa kitu fulani akifanyie kazi ili kuzalisha apate faida. Kitu iko ni talanta au kipawa kinachotarajiwa kimpe mafanikio mtu hatua kwa hatua, ingawa mwanzo wake ni mdogo, lakini wake utakuwa mkubwa.
Ni vema kila mtu kujitambua yeye anamiliki nini kama mtaji aliojaliwa na Mungu aliyeumba; iwe ni pesa au kitu cha kuanzia maisha kwa kufanyia kazi na kupata faida; iwe katika sekta ya kilimo, mifugo, biashara, elimu, ufundi na kadhalika.
Kuajiariwa si kipaumbele tukitaka faida kubwa; ila mahali pa kuanzia kujipanga kimaisha na kuanzisha miradi mbalimbali midogo kwa ndoto kuwa itageuka kuwa miradi mikubwa tukiifanya kibiashara na kisomi zaidi.
Hivyo kila mtu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha uwezo au neema au Karama au kipaji kama apendavyo aliyetuumba; ili apate kuzalisha na kupata faida katika mpango wa Mungu.
Ukipata nafasi jiunge WhatsApp chanel ya mkufunzi Dr. Peter Mkufya, PhD; ambaye ni mtaalamu wa projects ideas/business ideas.
Hakuna gharama ya kujiunga WhatsApp chaneli kupitia
MKUFUNZI