Ni kweli tukipenda tunaogopa kuonekana after money na si kwamba hatuombi kabisa ila utaomba kwa nadra sana tena pale unakuta umekamatwa hasa umekopa kote umekosa ndo unaamua kujitoa muhanga kumuomba uyoo mwanaume wa future.
Niliwai kujaribu kua decent kwa mwanaume niliehisi atafaa kua mume sikuomba pesa hata kidogo nilivunja mbaka kanuni zangu nolizojiwekeaga nikawa nafanya kila kitu kwake ni mtu mwenye kazi nzuri tuu cha ajabu labda aliona kapata mseleleko hakuwahi kujiongeza kunipa pesa
Siku nikaamua nimwambie sina nauli akanipa 5000. Mahusiano yaliishia hapo.
Mbaka leo analialia eti yuko tayari kuja kutoa mahari kwetu nikamwambia umekaa muda sana kukuruhusu kunirudia ni kukuonyesha sina chaguo kitu ambacho si kweli..wanaume wengi sana wanaojielewa siku ikifika nitakupa kadi ya harusi yangu, akanikatia cm.
Sasa wewe alipokupa hiyo 5000 si ungemwambia tu kuwa haikutoshi na kwann utegemee mtu ajiongeze na ameshakuonyesha hana tabia ya kutoa?!
Unajua shida yenu wanawake huwa mnapenda sana kuhisi vitu badala ya kuongea mkaeleweka. Unaweza kuta mwanamke anaona mwanaume anachangamoto fulani yeye badala ya kudadisi kwa kuuliza anaanza kuhisi na kujipa majibu, yaani tabia fulani ya kichawi aisee.
Wewe ulitakiwa uketi nae chini umwambie kuhusu tabia yake kuwa maisha hayaendi hivyo, unamshauri kuwa mwanaume unatakiwa kuishi namna hii na mwanamke sio namna hiyo. Asipobadilika hata siku ukisema nimeshindwa anaelewa.
Sasa ona kama huyo ni wewe ndie ulimuacha yeye hakukuacha, halafu alipokutafuta jambo la kwanza amependekeza ni kuja kwenu kukutolea posa akiamini tatizo ni kuchelewa kukuposa sasa atakuwa amedhania kuwa tatizo ni alikupotezea muda ndio ukaondoka kumbe sivyo.
Hivi unaona wanawake mnapochemkaga?! Unaweza kuta jamaa malengo yake ni kutoa kwa mkewe ila sio mwanamke anayeishi nae kisela. Pengine akioa anampatia mkewe hadi password ya kadi ya bank na pesa anashika mkewe.
Nakwambia hii from experience. Nilishawahi kuwa na demu wa akili hizi hizi. Alikuwa anahisi mimi ni bahiri kumbe mimi nilikuwa sipendi arrangements zake namna anaishi na mimi. Na kichwani nilikuwa nimepanga vitu vingi sana maana kidogo kidogo nilishaanza kumuona ni mwanamke ambaye kachagua kubakia na mimi.
Kuweni makini sana kuna wanaume pesa yake utaiona ukishakuwa mkewe wa ndoa maana amejiwekea misingi hiyo na huyo mwanaume hutakuja kuta anahonga wanawake nje ya ndoa jambo ambalo wanawake huwa mnaliogopa sana kusikia mume wako anampatia pesa mwanamke nje ya ndoa yenu.
Sasa wewe unaondoka kibubu bubu ukitegemea jamaa ataelewa. Unamkasirikia kisa amekupa 5000 kwann usingekaa nae chini umpe makavu yeye atajua cha kufanya. Unaweza hisi mtu ni mchoyo kumbe ana madeni lukuki huko nje analipa wewe umemkuta na madeni unahisi ni mchoyo.
Jitafakari sana hiyo tabia yako. Umefanya ubinafsi wa hali ya juu aiseee halafu unahisi umefanya ushujaa. Huo ni ushamba umefanya.